Kitabu cha Mwanzo katika Bible ndio msingi wa mambo matatu duniani! Intelijensia, Sayansi na Uchawi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,597
Jina huathiri muktadha, asili, chanzo na uhalisia wa kitu..... Kitabu cha MWANZO katika Biblia takatifu ndicho kitabu msingi kinachosomwa zaidi duniani... Tena na imani na dini zote...
Nukuu na rejea nyingi kwenye malumbano mijadala, tafiti za kisayansi, tafiti za kilozi na kishirikina, ulimwengu wa nguvu ya 'supernatunal powers (nguvu zisizomithilika) na hata maandiko mbalimbali yahusuyo asili na chanzo cha ulimwengu... Huwezi kuacha kutaja kitabu hiki....

Masomo ya sayansi, fizikia, baiolojia, historia, kemia historia, filosofia uchawi na ulozi.. Yote haya katika ujumla wake unayapata katika kitabu hiki cha MWANZO....
Unaposoma... MUNGU AKATAMKA NA IKAWA... hii ni aina ya ushirikina, imani katika nguvu za asili na uwezo wa kuumba na kuunda kwa matamshi tu... Sayansi iwayo yote haina uwezo huu... Mambo hayo kwasasa ni ya manabii mitume na wachawi(wanga na washirikina)
Mungu anapotamka kuwa kaumba viumbe vyote... VINAVYOONEKANA NA VISIVYOONEKANA... mpaka leo hii sayansi imeshindwa kutoa jibu sahihi juu ya hivyo VISIVYOONEKANA!

Hapa ndipo inabidi turudi kwenye rejea ya kitabu cha MWANZO na kuona nini kilisemwa na kikawa halafu kikawaje! Na ndipo tunapata ufunuo wa ajabu na ugunduzi kwamba hii tunayoita SAYANSI YA ITHIBATI si chochote bali ni njia tu ya mwanadamu kujaribu kutafsiri kwa njia yake kile ambacho kilishaandikwa na kufanyika kwenye kitabu cha MWANZO
Hakuna kipya chini ya anga na kwa hakika bado hatujaweza kuvumbua kila kilichomo na kilichoandikwa kwenye zile kurasa chache za kitabu cha MWANZO
World encyclopedia, volumes kwa volumes za sutras, misahafu kwa misahafu, maandiko na mavitabu makubwa ya wanafilosofia maarufu kuwahi kutokea duniani... SUMMARY yao iko kwenye kitabu cha MWANZO

Kuna wenzetu wenye mawazo mbadala kuhusu Bible na kitabu cha mwanzo.. Ukiwa mwepezi wa tafakuri wanaweza kwa HAKIKA kabisa kukuteka na hoja zao mahiri kabisa lakini zisizo na hakika.. Ni wajenzi wazuri wa hoja zinazoteteresha kama wewe ni legelege lakini ukitulia na kutafakari hawana mwendelezo na hawaendi zaidi ya kilipokomea kitabu cha mwanzo...
Wataandika na kuchagiza kwa maneno mengi na misamiati huku wakiweka nukuu za wengine ambazo nazo zinaishia kwenye kuakisi kile kilichomo kwenye kitabu hicho cha mwanzo....

Tukirudi hapa JF hata jukwaa hili la intelligence kwa sehemu kubwa linatawaliwa na maandiko toka kitabu cha mwanzo...

Ni kwa Muktadha huu kitabu hiki cha MWANZO kinabaki kuwa chanzo kikuu, msingi, chimbuko na asili ya kila kitu katika maisha yetu ya kila siku... Iwe sayansi uchawi imani ama intelijensia....!!!
 
Mkuu inawezekana hata wale "Wasiojulikana" ni miongoni mwa vile VISIVYOONEKANA!
Hawa ni kwa tafsiri za matabaka tu... Kule marekani hakuna kitu kinaitwa SIRI bali kuna kitu kinaitwa CLASSIFIED INFORMATION.... yaani habari fulani kwa watu fulani mpaka muda wake wa matumizi ya nyakati unapofikia kikomo hujulikana kwa wengine wote

Hawa wetu wasiojulikana sasa kuna siku itafika watajulikana tuu.... Binadamu hawezi kutunza siri maisha yake yote.... Kama SHETANI alishindwa ni nani mwingine atakayeweza?
 
Jina huathiri muktadha, asili, chanzo na uhalisia wa kitu..... Kitabu cha MWANZO katika Biblia takatifu ndicho kitabu msingi kinachosomwa zaidi duniani... Tena na imani na dini zote...
Nukuu na rejea nyingi kwenye malumbano mijadala, tafiti za kisayansi, tafiti za kilozi na kishirikina, ulimwengu wa nguvu ya 'supernatunal powers (nguvu zisizomithilika) na hata maandiko mbalimbali yahusuyo asili na chanzo cha ulimwengu... Huwezi kuacha kutaja kitabu hiki....
Masomo ya sayansi, fizikia, baiolojia, historia, kemia historia, filosofia uchawi na ulozi.. Yote haya katika ujumla wake unayapata katika kitabu hiki cha MWANZO....
Unaposoma... MUNGU AKATAMKA NA IKAWA... hii ni aina ya ushirikina, imani katika nguvu za asili na uwezo wa kuumba na kuunda kwa matamshi tu... Sayansi iwayo yote haina uwezo huu... Mambo hayo kwasasa ni ya manabii mitume na wachawi(wanga na washirikina)
Mungu anapotamka kuwa kaumba viumbe vyote... VINAVYOONEKANA NA VISIVYOONEKANA... mpaka leo hii sayansi imeshindwa kutoa jibu sahihi juu ya hivyo VISIVYOONEKANA!
Hapa ndipo inabidi turudi kwenye rejea ya kitabu cha MWANZO na kuona nini kilisemwa na kikawa halafu kikawaje! Na ndipo tunapata ufunuo wa ajabu na ugunduzi kwamba hii tunayoita SAYANSI YA ITHIBATI si chochote bali ni njia tu ya mwanadamu kujaribu kutafsiri kwa njia yake kile ambacho kilishaandikwa na kufanyika kwenye kitabu cha MWANZO
Hakuna kipya chini ya anga na kwa hakika bado hatujaweza kuvumbua kila kilichomo na kilichoandikwa kwenye zile kurasa chache za kitabu cha MWANZO
World encyclopedia, volumes kwa volumes za sutras, misahafu kwa misahafu, maandiko na mavitabu makubwa ya wanafilosofia maarufu kuwahi kutokea duniani... SUMMARY yao iko kwenye kitabu cha MWANZO

Kuna wenzetu wenye mawazo mbadala kuhusu Bible na kitabu cha mwanzo.. Ukiwa mwepezi wa tafakuri wanaweza kwa HAKIKA kabisa kukuteka na hoja zao mahiri kabisa lakini zisizo na hakika.. Ni wajenzi wazuri wa hoja zinazoteteresha kama wewe ni legelege lakini ukitulia na kutafakari hawana mwendelezo na hawaendi zaidi ya kilipokomea kitabu cha mwanzo...
Wataandika na kuchagiza kwa maneno mengi na misamiati huku wakiweka nukuu za wengine ambazo nazo zinaishia kwenye kuakisi kile kilichomo kwenye kitabu hicho cha mwanzo....
Tukirudi hapa JF hata jukwaa hili la intelligence kwa sehemu kubwa linatawaliwa na maandiko toka kitabu cha mwanzo...
Ni kwa Muktadha huu kitabu hiki cha MWANZO kinabaki kuwa chanzo kikuu, msingi, chimbuko na asili ya kila kitu katika maisha yetu ya kila siku... Iwe sayansi uchawi imani ama intelijensia....!!!
Kweli sana
 
Biblia imetungwa tu na watu kwa madhumuni yao maalumu
Mfano watu mnadanganywa kwamba nyoka alimshawishi Hawa ......hivi inaingia akilini nyoka awe na uwezo wa kumshawishi mtu ?
Huyo nyoka alikuwa anatumia lugha ya alama ?
Au alizungumza English ?

Ni stori za kutunga tu
Vipi kile kitabu kingine kilicho sema kuna mtu alienda mbinguni go and return, kwa usiku mmoja..!
 
Umesahau kitabu unachokiamini na yule aliyekuletea alishushiwa maandiko na kumbe mengine yalitoka kwa shetani pale yalipotafisiliwa na waandishi.maana yeye yalimshinda,maandiko hayo mnayasoma na kuzunguka nayo huku mkipunga mapepo ovyo mkiambiwa navyo ni viumbe rafiki
 
Kuna hoja matata sana inapatikana kwenye kitabu cha Mwanzo.
Hoja hiyo ni pale Mungu alipomzuia Labani mjomba wake Yakobo asitamke neno jema au baya kwa Yakobo.

Hii inatoa picha kabisa kuwa kuna watu wana midomo mikali sana yenye nguvu za kiroho, akikulaani unalaanika kweli, akikubariki kwa kinywa chake unabarikiwa kweli.

Mpaka kufikia hatua Mungu anakataza mtu asimtamkie neno mtu mwingine, usifikirie Mungu hajui uwezo wa huo ulimi kiroho.

Biblia ina siri nyingi sana aisee, hasa kama unataka kukaa chini na kujifunza.
 
Back
Top Bottom