Kitabu cha Malaki: kitabu kinachoonyesha kuzaliwa kwa Yohane mbatizaji na ujio wa Yesu Kristo ulimwenguni

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,206
2,000
Kitabu cha Malaki ni cha mwisho kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh, yaani Biblia ya Kiebrania. Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo, na kwa kuwa humo vitabu vya manabii vinapangwa baada ya vitabu vya hekima, kitabu cha Malaki ni cha mwisho kabla ya vitabu vya Agano Jipya.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi na jina lake

Kwa kuwa jina la nabii aliye asili ya kitabu hiki halijulikani, limetumika lile la neno lake muhimu zaidi, "Malaki", lenye maana ya "Mjumbe wangu" (kwa Kiebrania מלאכי).

Muda ambao kitabu hiki kiliandikwa

Yaliyomo yanawezesha kukisia kiliandikwa lini, yaani baada ya Hekalu la Yerusalemu kuwekwa wakfu (515 K.K.), na kabla ya katazo la ndoa za mseto kati ya Wayahudi na mataifa mengine lililotolewa na Nehemia (445 K.K.); sanasana ni karibu na mwaka huo.

Muhtasari wa kitabu hiki

Kitabu kinaundwa na sehemu sita za namna ileile: Mungu (au nabii wake) anatoa kauli ambayo inajadiliwa na waamini na makuhani wao, halafu inafafanuliwa katika hotuba inayochanganya vitisho na ahadi za wokovu.

Mada kuu ni mbili: makosa ya makuhani na waamini wengine katika ibada, halafu makwazo yanayosababishwa na ndoa za mseto.

Nabii anatabiri siku ya YHWH atakayetakasa makuhani, ataangamiza waovu na kuwapa ushindi waadilifu.

Mistari ya mwisho, ikitabiri ujio wa pili wa nabii Eliya, ilivutia sana tumaini la Wayahudi; ndiyo sababu ilijadiliwa sana kuhusiana na Yohane Mbatizaji na Yesu Kristo, kama inavyoonekana katika sehemu mbalimbali za Injili ya agano jipya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom