Kitabu cha "dr. Slaa mjenzi makini wa taifa" kinawakawaka channel ten leo jioni

Ukweli utabaki kuwa ukweli tu milele! Na kama huwezi huwezi, unaweza! Unaweza tu! Bila kuogopa vitisho! Proff kaongea ukweli hata dr lweitama kalisema!
 
Slaa ni 'demagogue' of our time.


Mwaka 1995 kuna mtu alimtungia kitabu Augustine Mrema. The rest is now history on what happened to Mrema.

After this election Slaa will dissappear politically, although gradually.
 
Henry Muhanika ni "mmoja wa wasomi maarufu"? Who knows this idiot anyway mpaka awe msomi maarufu? Crap!
 
! Haya, kazi ni moja tu hapo kiwandani, chapeni vitabu hivyo usiku na mchana ili watanzania tumtambue vema Dr.Slaa!! Copies copies please!
 
Muhanika azindua kitabu cha Dk. Slaa

na Chalila Kibuda

NYOTA ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, imeendelea kung’ara baada ya mmoja wa wasomi maarufu nchini, Henry Muhanika, kuzindua kitabu kinachoeleza maisha ya mgombea huyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho, mjini Dar es Salaam jana, mtunzi wa kitabu cha “Dk. Willibrod Slaa, Mjenzi Makini wa Taifa”, Henry Muhanika, alisema kama viongozi wakiweka misingi imara na kuwa waadilifu michango yao itaendelea kuthaminiwa.
Alisema, kuandika kitabu hicho, kumetokana na msukumo katika mchango wake kwa taifa; kusimamia maslahi ya Watanzania na kuchukia vitendo vya ufisadi vinavyolitafuna taifa.
Alisema kitabu cha Dk. Slaa, kimejikita zaidi katika mambo ambayo ameyafanya katika nyanja zote kwa uadilifu na uwazi kwa wananchi katika kusimamia maendeleo na kupambana na vita dhidi ya umaskini.
Alisema kitabu hicho, kamwe hakikuzinduliwa kwa ajili ya kumsadia Dk. Slaa wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Alisema kitabu hicho ni mfululizo wa vitabu ambavyo ataviandika kwa viongozi waliofanya vizuri katika nyanja mbalimbali kwa faida ya Watanzania na sio kwa maslahi binafsi.
Alisema akiwa mbunge wa Karatu, aliweza kutatua kero za maji na elimu ambazo zilikuwa changamoto kwa wananchi wake kuweza kujikomboa.
“Kuandika kitabu hicho sio kila mtu ataandikwa, tutaangalia uadilifu wake kwa wananchi na kuamua kuandika na haombi mtu aandikwe katika mwendelezo huu wa vitabu vya kuwakumbuka kwa michango yao,” alisema Muhanika.
Alisema katika sera zake, anaonekana kutaka kujenga Tanzania yenye mabadiliko ambayo yatawakomboa wananchi kutoka dimbwi la umaskini ambao umewafanya kuwa tegemezi.
 
Ziko library na sehemu za wazi wanazouza vitabu kama posta mpya nk; sh 3500 simple; ni kizuri sana kwa mstakabali wa nchi yetu
 
Nampongeze Rafiki yangu Henry Muhanika kwa kuandika kitabu hiki. Ni wakati muafaka. Nilisoma na Henry Muhanika Carleton University, na namjua ni mtu muadilifu siku zote.

Mara tu nitakapotua Dar mwisho wa mwaka nitakitafuta hicho kitabu nikisome. Saa hizo Slaa atakuwa ndiye Rais (la sivyo hata kuja sitajisikia kufanya hivyo).
 
Bravo Muhanika.. you are a true Tanzania

Slaa is our president and if we buy this book his popularity will increase form 82% & to 99%....

Slaa Slaa Slaa ale ale ale... Go Go Go ale ale ale....
 
Channel ten leo jioni imeonyesha uzinduzi wa kitabu kiitwacho "Dr. Slaa mjenzi makini wa Taifa."

Kitabu hicho kinazungumzia mchango wa Dr. Slaa katika ujenzi wa taifa hili changa.

Utoaji wa vitabu vya aina ya "memoirs" ni jambo la kawaida sana ikumbukwe Barrack Obama alitoa kitabu cha "Dreams from My father" na "The Audacious of Hope" ambavyo vilisaidia sana kumweka kwenye chati katika chaguzi za nchi hiyo.

Kwetu hapa watu hawana tabia ya kujisomea vitabu, hivyo ufanisi wake kwenye kampeni hii unatarajiwa kuwa ni kiduchu ukilinganisha na mchango mkubwa utakaojitokeza kwenye kampeni zake ambazo zinakwenda vizuri mno kuliko matarajio ya wengi.

Kama kitabu hicho kitawekwa kwenye internet basi wengi tutaweza kukisoma kabla ya uchaguzi au kama watakisambaza mapema mikoani itasaidia kwa haswa sisi wapashaji watu wengine habari.

Kitabu hicho kimehaririwa na mwandishi wa siku nyingi Bw. Henri Muhanika.

Mara nitakapokisoma kama itakuwa kabla ya uchaguzi nitakichambua kwa manufaa ya wale ambao hawataweza kukisoma kwa sababu moja au nyingine
Je kinaweza kupatikana elekronikali au kupitia ununuzi mtandao? Au ukiwa mtu anakihitaji atakipata vipi?
 
Henry Muhanika ni "mmoja wa wasomi maarufu"? Who knows this idiot anyway mpaka awe msomi maarufu? Crap!

Unaweza ukawa msomi maarufu na bado ukawa mpumbavu wa kulamba miguu ya mafisadi, hata kama sio msomi maarufu, Henry Muhanika ana uwezo unaokubalika, wewe una uhalali gani wa kuhoji uwezo wake? wewe ni nani na umefanya nini japo kwenye mtaa wako? Tusipoteze muda kuuliza ni nani bali tuangalie amefanya nini. Your argument or question is too low to be in this forum.
 
God Bless you Professor Mhanika,
...

Sina uhakika kama Henry Muhanika ni professor; I may be corrected, huyu ni mwandishi wa habari mkongwe na siku za nyuma aliandika makala nzuri DailyNews baadaye akajiunga na siasa za mageuzi enzi za Lyatonga Mrema.
 
big up prof. Muhanika keep on reminding fellow tz the past truth. hakuna kuchakachua.
 
Jamani wana Familia ya JF, mimi kichenchele naomba kutoa yaliyo yangu maoni juu ya huu uwanja ambao tumekuwa tukipata taarifa/habari juu ya maswala mbalimbali yahusuyo maisha yetu kama Watanzania, Waafrica, wasomi, weledi, na watu wa kada mbalimbali, nashukuru sana kwa hilo, inaniwia vigumu sana kuamini, kama tunataka kuugeuza uwanja huu kuwa mahala pa kutoa matusi na kutukanana bila haya na kusahau kuelimishana na kuwasaidia wale wanaohitaji msaada wa kimawazo. ukweli haiingii akilini kuona mtu anadiriki kuandika lugha isiyo na nidhamu kwa mwanachama mwenzake, nafikiri kama mtu amekosea tumsaidie kumwelewesha juu ya kile alichokosea, naamini hapa kuna watu wazima na waelewa wa maswala mbalimbali yanayozunguka jamii yetu na jamii za kimataifa, ila kama tutaonekana kutothamini umuhimu wa watu kuwa ktk huu uwanja ukweli wengi watashindwa kutoa misaada yao kimawazo kwa kuwa wataona watu tuliomo JF wengi ni wahuni kitu ambacho si kizuri hata kidogo, nachofahamu mimi JF ni sehemu nzuri sana ya kupata taarifa za kila aina za matukio yanayotokea kila siku za maisha yetu, hali ambayo inamsaidia hata yule asiyeweza kununuwa gazeti kupata taarifa sahihi au kama umesahau kununuwa gazeti JF inaweza ikakuhabarisha. Watanzania wenzangu nawaombeni wale wenye tabia ya kutukana wenzao tuache jamani si vizuri kutukanana hadharani, hata kama majina yetu si halisi lakini ukishazoea kuutukana ukuta wa nyumba ipo siku utakuja kutukana kiumbe aina ya mwanadamu, tupendane, tusaidiane, tushirikishane, tueleweshane, tusahihishane,tuelimishane ili mwisho wa siku tuweze kuwa na jamii elevu na yenye kupata taarifa zilizo sahihi.Watanzania wengi tunahitaji kupata msaada wa kimawazo toka kwa watu mbalimbali waliomo JF, tuitumie kwa manufaa. matusi si mazuri, ukimtukana mwenzio ni sawa na kumvua nguo hadharani.
 
It will help him raise additional cash for the work ahead. Also, I think we gonna have a reasonable perspectives on some issues. sometimes its hard to follow a campain trails, people say all kind of things to get votes. I think the culture of book writing is a good presentation if someone get a good editor who knows what the audiance is looking for in a candidate. Thanks Rutashubanyuma for bringing this forward.
 
Back
Top Bottom