Kitabu cha baba wa taifa katika mjadala Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam 26 Mei, 2022

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
1653495332618.png
1653495374858.png
1653495465205.png

Kulia Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman Yahya, Dr. Ng’wanza Kamata katika mahojiano na Mohamed Said (out of sight) kuhusu Mwalimu Nyerere wakati wa utafiti wa kitabu chake.
 
Huyu mzee ndio aliyebaki pekee anayelialia mitandaoni kuhusu hao babu zake wasio enda shule.

Hataki kutambua kuwa kwenye movie kuna main character na minor characters..sasa unapotaka minor characters wapate umuhimu kuliko main character utakua unaharibu movie.

Namshauri akae kutulia alee wajukuu..historia ya nchi hii ilikwisha andikwa hizo story zake feki akaweke kwenye makabati yake watasoma wajukuu zake.

#MaendeleoHayanaChama
 
Je unaweza kuandika BIOGRAPHY ya mwalimu bila kuzungumzia mchango wa chama cha TANU? Na kama utazungumzia chama cha TANU basi huwezi kumkosa Abdulwahid Sykes!
Mohamed Said anataka Abdul Sykes apewe sifa kubwa kuzidi Nyerere! Wakati hakuwahi kuwa kiongozi wa TANU!
 
Bila shaka hakitaandika chochote kuhusu mwalimu kunyang'anya shule za kanisa lake ili na Waislamu wasome, hi story nina hakika haitakua inclusive
Mazindu...
Nyerere hakutaifisha shule ili Waislam wasome.

Ingekuwa hivyo Waislam ungewaona wengi kwenye vyuo.
Takwimu zinakataa hili.
 
Mohamed Said anataka Abdul Sykes apewe sifa kubwa kuzidi Nyerere! Wakati hakuwahi kuwa kiongozi wa TANU!
Vito...
Abdul Sykes hawezi kufikia sifa za Nyerere hata siku moja.

Laiti ningeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kwa nia hiyo kitabu changu kingekufa miaka mingi.

Abdul Sykes uzito wake upo kwanza kwenye historia ya baba yake Kleist Sykes kiasi yumo katika Dictionary of African Biography (DAB).

Abdul Sykes sifa yake kubwa na ndiyo iliyowashangaza wengi waliposoma kitabu ni ule mchango wake kwanza kwa Julius Nyerere kama rafiki ndugu na mzalendo aliyeunda TANU akiwa na kadi No. 3.

Kadi No. 1 ikiwa ya Nyerere na No. 2 Ally Sykes.

Historia hii ndiyo inayomnyanyua Abdul katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini kubwa lilimweka Abdul Sykes juu sana ni kule yeye kufutwa katika historia ya chama alichounda na historia ya kupigania uhuru.

Sijui unakusudia nini unaposema Abdul hakuwa kiongozi wa TANU ilhali mikutano yote ya siri ya chama ikifanyika nyumbani kwake.

Mufti Sheikh Hassan bin Ameir hakuwa na nafasi yoyote ya uongozi katika TANU lakini yeye alikuwa mmoja wa nguzo iliyosimamisha TANU na kumpa nguvu Nyerere.

1653543943458.png
 
Kuna kizazi cha 90s kuhusu Mwalimu hawamjui kabisa, kitabu kitaleta mageuzi kwenye historia ya nchi.
 
Huyu mzee ndio aliyebaki pekee anayelialia mitandaoni kuhusu hao babu zake wasio enda shule.

Hataki kutambua kuwa kwenye movie kuna main character na minor characters..sasa unapotaka minor characters wapate umuhimu kuliko main character utakua unaharibu movie.

Namshauri akae kutulia alee wajukuu..historia ya nchi hii ilikwisha andikwa hizo story zake feki akaweke kwenye makabati yake watasoma wajukuu zake.

#MaendeleoHayanaChama
Jiwe...
Tujadiliane kwa heshima na adabu misemo kama "kulialia," "feki," haipendezi.

Abdul Sykes hakuwa "minor character," katika mchezo huu.

Movie imeharibika kwa kudhani tunaweza kuwa na historia itakayoweza kusimama kwa kujaribu kuifuta historia ya kizazi kizima na kupachika historia mpya.

Ndiyo maana leo kupitia kitabu changu watu wanasoma historia mpya na ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Hii historia unayoisoma kutoka kwangu ina miaka 100 nami ni sehemu ya historia hii.

Kitabu changu kinakwenda toleo la tano.
Hii haijapata kutokea nchini petu.

1653543790045.png
 
tungewaona wengi vp wakati wao wenyewe walikua bize madrasa na elimu akhera,kwani hao maprofesa waislamu walisoma shule na vyuo gani
Fogo...
Siko hapa kufanya ubishi.
Unaweza kuamini upendavyo.
 
Mazindu...
Nyerere hakutaifisha shule ili Waislam wasome.

Ingekuwa hivyo Waislam ungewaona wengi kwenye vyuo.
Takwimu zinakataa hili.
Taja nchi 10 za Kisslamu duniani halafu zinao wasomi wengi. Kwa asili uislamu una aleji na ELIMU, hilo linajulikana, sema kama unataka kubishana tu mzee wangu. Libya ya Gadaff ilifadhili elimu from the scratch to higher level, nambie Walibya wangapi walikua na degree walau moja? Nenda kote Qatar, Saudia kote huko kunako itwa Mataifa tajiri ya Waarabu, angalia think tank wao ni kina nani? Sio Wazawa mzee. Njoo mikoa ya pwani hata sasa hivi, angalia idadi ya watoto wanao maliza form 4 hasa wa kike ni wa ngapi? Na hili nalo Nyerere anahusika kwenye hu ulimwengu wa elimu bure? Kumsingizia mtu ni DHAMBI kubwa, hata kama sio wa dini yako. Mwinyi akiwa rais alizifanya shule karibu zote za Nyerere kua day schools ili watoto wengi wasome, idadi ya waislamu kipindi hicho walikua wangapi? Mlipenda zaidi madrasa na sio elimu dunia, kuweni wakweli mzee
 
Huyu mzee ndio aliyebaki pekee anayelialia mitandaoni kuhusu hao babu zake wasio enda shule.

Hataki kutambua kuwa kwenye movie kuna main character na minor characters..sasa unapotaka minor characters wapate umuhimu kuliko main character utakua unaharibu movie.

Namshauri akae kutulia alee wajukuu..historia ya nchi hii ilikwisha andikwa hizo story zake feki akaweke kwenye makabati yake watasoma wajukuu zake.

#MaendeleoHayanaChama
It is team work, without the minor characters you cannot have a complete movie!! It is important to know our true history ili tuweze kutambika vizuri!!!
 
Back
Top Bottom