Kiswahili ni lugha bora kwa wanafunzi wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili ni lugha bora kwa wanafunzi wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ibnu Ayoub, Mar 7, 2011.

 1. Ibnu Ayoub

  Ibnu Ayoub Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Napendekeza masomo yote yanayofundishwa katika mashule na vyuo vyote Tanzania yafundishwe kwa lugha ya taifa ili kuongeza idadi ya wanaofaulu na uelewa juu ya wanachojifunza. Kusoma kwa kiswahili kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba halafu unapoingia kidato cha kwanza unaanza kusoma masomo yote kwa kiingereza huku ni kuumizana na kupotezeana muda wana Jamii, Mnapoandamana kuhusu Maisha bora msilisahau na hili.Hakika wanafunzi wanaumia sana kwa kukariri kuliko kuelewa.
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hapa ninakuunga mkono Mkuu. Sera ya Tanzania ya lugha imepotoka. Nakumbuka tangu mwaka 1969 Serikali ilitangaza nia ya kukifanya Kiswahili sio lugha ya Taifa tu bali lugha ya kufundishia, alkini sera hii daima haikutekelezwa badala yake tunawasumbua wanafunzi. Tunawaumisha vichwa wanafunzi wetu ambao inawabidi wafikirie katika Kiswahili wakati wanapokumbana na swali katika lugha ya Kiingereza. Mtoto hujifunza zaidi katika lugha yake ya kwanza. Faida yake watoto wanakuwa wepesi wa kufahamu na wabunifu kwa kutumia lugha yao kuliko kutumia lugha ya kigeni. Hapa hatusemi kuwa Kiingereza kiwachwe, bali kisomeshwe kama lugha ya pili tangu miaka ya mwanzo ya elimu.

  Wanaotetea Kiingereza wanadai kuwa Kiswahili hakijitoshelezi. Hii si kweli. Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili imekuwa ikisanifisha Kiswahili kwa muda mrefu katika nyanja zote na tayari kuna makabrasha kwa makabrasha ya maandishi yaliyokaa katika makabati bila ya kupelekwa kwa watumiaji.

  Kiswahili kina utajiri mkubwa na ulaini wa kulibadilisha neno lolote la lugha ya kigeni (hasa kutoka Kiingereza tunachoking'ang'ania) na kulitohoa kukidhi matamshi, maana na maandishi ya Kiswahili.

  Wakati umefika kukifanya Kiswahili lugha ya kufundishia viwango vyote vya ellimu.
   
 3. Ibnu Ayoub

  Ibnu Ayoub Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Umesema kweli Mamamia
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Pia wakumbuke kuwa hata Kiingereza wanachokikomalia huko Ulaya zama hizo hakikuwa lugha ya vyuo. Mpango mzima ulikuwa Kilatini... Waingereza wakaona haja ya kubadili mfumo ili uwafae, nashangaa sisi. Unakuta kutwa kucha wanafunzi wanakariri point, ukisoma maelezo, utumbo mtupu!
   
Loading...