Kiswahili ni Ishara ya kujikomboa kifikra Watanzania

mkwapuaji

Member
Jan 6, 2012
49
20
Kwa mfumo huu wa elimu usiowafanya watu kufikiri ni vigumu sana kumwelewesha mru umuhimu wa kiswahili akuelewe.
Vijana wanashindana kukariri masomo na kuyatapika kwenye mitihani na mbobezi basi ndio huwa kinara. Tunasahau kuwa elimu inatakiwa ikukomboe kifikra, kiufanisi na hata kimahusiano.

Niliwahi kukutana na aliyejiita Tanzania One kwakuwa tu kawa kinara wa kurejelea aliyo kariri basi anaamini yeye ndiye mjuzi.
Kijana huyu anasahau kuwa yupo mtu aliyegundua helkopta na sio kinara....
Wako walioweza kuzalisha umeme vijijini na wakautumia kuzalisha nao sio vinara....
Kinara ni yeye aliyekimbilia ofisi ya watu wakimtumikisha ... ???!!!!....

Ujerumani ndiye kinara wa uchumi ulaya na sio uingereza mnayokimbilia kujifunza na kuitumia lugha yao....

Vietnam, malaysia, japan, thailand wanatumia lugha zao na wametuzidi sie tunaotaka kuonekana bora mbele ya waliobora kisa tu kiingereza....

Afrika nguvu tuliyonayo kimasoko na kiuchumi kwenye dunia ya sasa ni kubwa sana lakini hatulitambui hili tunaamua kuuza utu wetu kwao.

Elimu inayopaswa kutolewa kwa mwafrika ni elimu yenye kumkomboa mwafrika kifikra sio hii tuliyorithi kwa wakoloni ambayo haikuhitaji fikra ya mwafrika kwani asingetawalika.
Elimu itakayomfanya kijana wa kiafrika awaze kesho na hata mtondogo kuliko hawa wa sasa waliojawa uwoga wa maamuzi hasa kiuwekezaji pindi anapoona yeye hatiweza kuwa mlaji wa faida bali wajukuu.
Elimu itakaouondoa ujinga ambao kila siku unalindwa na baadhi ya wanaojiita wasomi huku wakiuita ujinga utaalamu na kulisababishia hasara kwa vizazi na vizazi sababu tu ya maamuzi yao mabovu.

Elimu ni msingi wa maisha.
 
Back
Top Bottom