KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Hivi ni kweli mlio Tanzania hamuwezi kueleza kinagaubaga maana ya neno hili ambalo Mwalimu Kichuguu ameuliza?
 
Ninajaribu kutoa maoni yangu.

Kulingana na "Kamusi ya Kiswahili Sanifu", maana yake "-nyanyapaa" ni: "-epuka mtu kwa dharau na kumwona mtu kama kinyaa au mchafu". Kamusi inatoa minyambuliko ifuatayo: "-nyanyapalia, -nyanyapalika, -nyanyapaza".

Mimi ningesema:

1) Jumui(y)a imemnyanyapaa mgonjwa
2) Mgonjwa amenyanyapawa na jumui(ya)

Kwangu sentensi hizi si sahihi:

1.b) Jumuia imemnyanyapaia mgonjwa
1.c) Jumuia imemnyanyapaisha mgonjwa
2.a) Mgonjwa amenyanyapaa na jumuia
2.b) Mgonjwa amenyanyapaaiwa na jumuia

Je, mnaonaje?

Nino
 
Masatu, Dua na Nino nawashukuruni sana kwa msaada wenu. Unajua kiswahili kimekuwa kinapata maneno mapya haraka haraka sana, wengine tusiopojihadhari tutajikuta tumeachwa mbali sana.

Hata hivyo kama kuna mwenye ufafanuzi zaidi, tafadhali asisite kuutoa.
 
Unajua kiswahili kimekuwa kinapata maneno mapya haraka haraka sana, wengine tusiopojihadhari tutajikuta tumeachwa mbali sana.

Ndugu Kichuguu, nakubaliana nawe! Lakini naogopa kwamba Kiingereza kitaendelea kuharibu Kiswahili. Zaidi ya hayo ninahisi kwamba Kiswahili kitakufa mapema kwa sababu katika shule ya sekondari wanaendelea kufundisha kwa njia ya lugha ya Kiingereza :(, na Wakubwa (wanasiasa, matajiri, nk) hawapendi watoto wao wafundishwe kwa njia ya Kiswahili.

Asante,
Nino
 
Salaam;
Kesho ninatoa mada kuhusu dawa za kupunguza makali ya ngoma/HIV kwa kiswahili.
Machache nitakayoongelea ni pamoja na zipi dawa ni first line na zipi ni second line!
Swali: naomba waswahili mniambie first line kiswahili chake ni kipi? Nikishapata hicho, second line haitanipa taabu, nitanyambulisha tu, au sio.
Asanteni.
 
Salaam;
Kesho ninatoa mada kuhusu dawa za kupunguza makali ya ngoma/HIV kwa kiswahili.
Machache nitakayoongelea ni pamoja na zipi dawa ni first line na zipi ni second line!
Swali: naomba waswahili mniambie first line kiswahili chake ni kipi? Nikishapata hicho, second line haitanipa taabu, nitanyambulisha tu, au sio.
Asanteni.

Nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kukusaidia. Ila jibu hili siyo final, ukikutana na mganga atakusaidia vizuri zaidi kwa vile mimi ni kichuguu tu.

First-line treatment drugs ni dawa anazopewa mgonjwa yeyote mara baada ya kujulikana kuwa na ugonjwa fulani. Second-line ni dawa wanazopewa wagonjwa ambao hawakuwasaidiwa na dawa za fisrt-line.

Kwa mfano zamani zile first-line dawa ya maralia ilikuwa ni chloroquine, ila kwa wale ambao chloroquine ilikuwa haiwasaidii walikuwa wakipata second-line madawa kama Quinine drip au fansidar etc.
 
Nafikiri Kichuguu upo sahihi. Pia kwa lugha ya kienyeji kuongezea toka hapo ni kwamba dawa za First line ni zile ambazo mgonjwa anapewa ikiwa ni mara ya kupatwa na huo ugonjwa, na second line ni zile ambazo mgonjwa anapewa baada ya dawa za first line kushindwa, hivyo hizi huwa kali kidogo ukilinganisha na zile za first line. Na mara nyingi madaktari wanashauri mgonjwa atumie dawa kulingana na mlolongi huo, ili kuepuka mwili kuwa sugu kwa kutumia dawa kali zaidi kabla hajajalibu dawa za kawaida ambazo nyingi zipo kwenye first line.
 
Wataalamu,
mimi ni shabiki wa neno AJUA, lakini mara ya mwisho kulisikia likitumika ni mwaka 1995,sitanii! Ilikuwa kwenye mechi moja hivi ya mpira ambapo refa aliamua kulitumia ili kutoa pingamizi fulani hivi,sikumbuki sawa sawa, ila hilo tukio liko kichwani mwangu mpaka leo hii. Kumbukumbu yangu nyingine niliyo nayo ya matumizi ya neno hilo ni kushuhudia watu walio kuwa wakiwafundisha wananchi fulani hivi mafunzo ya mgambo...walikuwa wakitumia neno hilo ili kuwa kuwatawanya wanamafunzo hao,sikumbuki vizuri kwa kweli.

Basi, naomba mnifafanulie maana halisi ya neno hili, naomba pia mtoe mifano kadhaa hapa ya matumizi yake kama inawezekana katika maongezi ya kawaida tu. Na cha nyongeza, nitafurahi sana kama nikipewa tafsiri yake kwa Kiingereza na mfano angalau mmoja.

Ahsanteni.

SteveD.
 
Ajua ni neno lililotokea jeshini likiwa na maana ya kughaili tendo lilifanywa na kundi la watu: chimbuko lake zaidi ni kwenye kwata za kijeshi. Kwa mfano kama wakati wa kwata, kama kamanda akitoa amri ya kuwataka askari watelesha silaha zao kutoka begani iitwayo "telemsha silaha" halafu askari wakawa hawakuzitelemsha kwa pamoja kama inavyotakiwa, basi kamanada huyo huwaambia "ajua" kwa maana ya kuwa ameghaili jinsi walivyotekeleza amri hiyo kwa hiyo warudishe silaha zao begani kusudi atoe amri nyingine.

Neno hili limetoka kwenye kiingereza ambapo makamanda walikuwa wakisema "as you were" kuwaashiria askari warudi katika position waliyokuwa nayo kabla ya amri.
 
Jamani kiwahili...

Kuna siku moja nilihudhuria shughuli ya kufunga ndoa ya rafiki yangu. Kadi ya mwaliko iliandikwa neno "ARUSI". Hilo neno likazua mabishano katika meza yetu. Kundi moja lilisema hilo neno limeandikwa sahihi "ARUSI", Lakini kundi lingene lilipinga kwa kusisitiza kwamba maandishi sahihi yalipaswa kuwa "HARUSI". Binafsi nilikuwa upande wa "HARUSI".

Mnaonaje wataalamu?
 
Kwa kiarabu (lugha ya asili yake) neno [H]ARUSI linaanza na herufi "'ain", ambayo ni tofauti kabisa na "h" yoyote ya kiarabu. Zamani tahajia sahihi ilikuwa ARUSI, lakini siku hizi watu wengi hutumia HARUSI, hata Kamusi Sanifu ya TUKI ina "arusi taz. harusi". Tungefuata mifano na maneno mengine yenye asili hii hii tahajia "arusi" ingekuwa na mantiki zaidi. Neno la ELIMU kwa kiarabu linaanza na herufi ile ile, lakini HELIMU si sahihi!
 
Waungwana naomba msaada wa Tafsiri na maana ya maneno haya yafuatayo: "CONSPIRACY" na maneno ya kiswahili "HAFIDHINA" na "FISADI"
 
Waungwana naomba msaada wa Tafsiri na maana ya maneno haya yafuatayo: "CONSPIRACY" na maneno ya kiswahili "HAFIDHINA" na "FISADI"

Conspiracy ni NJAMA, Hafidhina ni HAFIDHINA kwa kiingereza ungesema conservative, Fisadi ni FISADI, labda kwa kiingereza ungesema crook.
 
Nashukuru Mwl Kichuguu!,Lakini naomba unipe utofauti kati ya NJAMA na HUJUMA.Kwa sababu kuna Muungwana aliniambia Tafsiri ya Conspiracy ni HUJUMA!
 
Nashukuru Mwl Kichuguu!,Lakini naomba unipe utofauti kati ya NJAMA na HUJUMA.Kwa sababu kuna Muungwana aliniambia Tafsiri ya Conspiracy ni HUJUMA!
  • Njama ni mipango ya siri inayofanywa dhidi ya mtu au kikundi cha watu bila wenyewe kujua ili kusudi baadaye mipango hii iwasababishie maumivu fulani walengwa. Maumivu yakusudiwayo na njamayanaweza kuwa ni physical au moral.

  • Hujuma ni kitendo cha kuharibu mali au mipango ya mtu au kikundi cha watu kwa makusudi ya kusababisha maumivu ya aina fulani kwa wamiliki; kwa kiingereza inaitwa "sabotage." Maumivu yatokanayo na hujuma pia yanaweza kuwa ni physical au moral.

  • Njama ndiyo inasababisha hujuma.
 
1. Fala

2. Nyomi

3. Mdebwedo

4. Mswano

5. Tinginya

6. Chelea pina

7. Msela

8. Mneli

9. Msuba

10. Fyatu

(Naomba na mifano kwa sentensi ikibidi).

Ahsanteni
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom