Kiswahili na wana-TEKONOHAMA au mabingwa wa ICT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili na wana-TEKONOHAMA au mabingwa wa ICT

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Iga, Aug 28, 2008.

 1. I

  Iga Senior Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HILI ni wazo langu kwa fikira zangu dogo.

  Labda niliweke katika swali. Je JamiiForums ina watu wenye mapenzi na Kiswahili kiasi cha kutosha kujitolea muda wao kuanzisha kitu kitakachoitwa KISWAHILI DEVELOPMENT COMMUNITY FORUM?

  Je Forum hiyo inaweza kuwa na makundi mbalimbali ya watu hususan kulingana na hapa chini:

  . Wana Istilahi za Kemia
  . Wana Istilahi za Fizikia
  . Wana Istilahi za Jiografia
  . Wana Istilahi za Historia
  . Wana Istilahi za Commerce
  . Wana Istilahi za Book-keeping
  . Wana Istilahi za Introduction to Computers
  . Wana Istilahi wa Programming
  . na kadhalika na kadhalika.

  Je, makundi haya yanaweza kujitolea kuanzisha uundwaji istilahi katika fani yao mtandaoni kwa kutumia nadharia ya Open Source. Katika kila fani watu watachangia tafsiri ya maneno ya Kiingereza kwa Kiswahili kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila somo lina tafsiri ya msamiati wake wote kwa Kiswahili?

  IKUMBUKWE KWAMBA TAYARI MCROSOFT wana hazina ya maneno laki 7 yaliyokwishatafsiriwa kwa Kiswahili.

  Baada ya kuundwa kwa Istilahi, je, sisi wenye uchungu na lugha yaetu ya Kiswahili tunaweza kuanzisha Kiswahilipedia?

  Katika kiswahilipedia wakuu wa forum katika fani mbalimbali watawagawia wanachama wetu sura za kuandika katika kila somo. Sura hizo zitasomwa na kushahishwa na wengine bila kuharibiwa kwa mada asilia.

  Baada ya miaka miwili tu hivi hatutakuwa na elimu zote zinazofundishwa Tanzania hivi sasa kwa Kiswahili?


  Wale wanaodhania kwamba ni WANASIASA AU SERIKALI ndiyo inayoweza kutuhamisha toka kutawaliwa na kulemazwa na Kiingereza cha kubabaisha wanakosea. Ni sisi wenyewe. Na tumshukuru Muumba kwa teknolojia hii ya habari na mawasiliano ambayo leo inaweza kuigeuza kazi ya kuwa na vitabu vya kiswahili katika kila somo kuwa rahisi kama vile mchezo. Tuanze. Na wakati ni huu. Maprofesa, madokta na walimu wa Kiswahili. Wakina Ikbal Shaaban Robert Karibuni, Mobhare Matinyi na na David Fisadi Marekani na kina Katunzi India na China ilipeni jamii mlichopewa bure!

  Asilimia 95 ya Watanzania hawawezi kuelimika kwa Kiingereza wanataka masomo na mafunzo kwa Kiswahili. Je, hii kazi ikifanyika si tuna soko kubwa tu la masomo ya Kiswahili kwenye mtandano. Twendeni hatua moja mbele ya forum za k ujiburudisha na blogi za kukashifiana tuanze kuaandaa vitabu mtandaoni kwa ulainiiiiiiini!!!!!

  Na ninaiomba UFALME WA NORWAY uliochangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa Microsoft Office na Windows XP/Vista kwa Kiswahili wasisite kutoa msaada wao kwa KISWAHILI DEVELOPMENT COMMUNITY FORUM punde itakapoanzishwa.
   
 2. c

  changamoto Member

  #2
  Aug 28, 2008
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Udhaifu wetu sisi Wazazi na walimu ndio unaochangia kudumaza uwezo wa watoto kushika lugha kwa tasihili inayostahili.

  Halafu kuna hili la njaa na lishe bora-ni lazima tuhakikishe kuwa sio tu kuna madarasa na shule bora bali pia hata lishe bora ili uwezo wa kiakili wa watoto wetu uweze kuhimili matakwa ya kujua lugha tatu au nne kama sio zaidi na kukamata masomo mengine kama kawaida.

  Wanaoingilia mada hii katikati wajue kwamba hili sio suala la Kiswahili au Kiingereza. La hasha.

  Ni suala la Kiswahili kwanza ili tukamate dhana na nadharia mbalimbali vyema na kwa wepesi zaidi. Kisha lugha mbili, tatu au nne zinazofundishwa kwa kutumia TEKNOHAMA kiasi ambacho watoto wataona ni mchezo na starehe kujifunza lugha na sio kama hivi sasa ambapo kujifunza lugha ngeni inaonekana ni adhabu.

  Na nilishawahi kusema kama tunataka watoto wajue Kiingereza kweli kweli basi tuwalete angalau vijakazi wa malikia kuja kujifunza hapa.

  Na Kiarabu lazima tuwalete Waarabu wanaojua Kiswahili au Kiingereza kuja kuwafundisha watoto wetu.

  Aidha Kifaransa na Kireno lazima tupate mzungumzaji toka Ufaransa au Cote D'Ivoire au Msumbiji au Cape Verde aje awafundishe watoto wetu. Iwe mwiko kumpa mwalimu Mtanzania kufundisha lugha ya Kigeni labda kama ana digrii angalau moja kwenye lugha hiyo. Hili linawezekana, maana, ukitaka kuondokana na umasikini jaribu kutosishi kama masikini. Na kama unataka maendeleo usiishi kama mtu asiye na maendeleo, ishi kama mtu aliye na maendeleo.

  Dunia hii sio kwa ajili ya wanaoangalia nyuma, bali wanaoangalia mbele kwa kukaa vyema hapa tulipo.
   
 3. P

  Prince Member

  #3
  Aug 28, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iga,

  nakuunga mkono kwa asilimia 100 kuhusu hoja hii. Mimi niko tayari kujitolea muda na utaalamu wangu katika kufanikisha hili. Inaniuma sana ninapoona wengine kama Wamarekani (kamusi projecy ya Yale) nk wakichangia ukuaji wa Kiswahili halafu sisi tumekaa pembeni. Ukipitia baadhi ya maneno utagundua kuna makosa mengi lakini ni kwa sababu watz tunaojua lugha hii zaidi tuekaa pembeni.

  kwa kuanza tusiangalie uwingi wa watu. wengine watadandia baadae. Kitu muhimu ni kuanzisha mwendo kwa kuchukua hatua ya kwanza.

  naomba kuunga mkono hoja
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Oct 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  tangia tangazo hili limetolewa umefanya jitihada gni kuhakikisha unatumia ujuzi wako katika kufanikisha yale uliyoyasema au umewahi kukumbushia chochote ? au uliandika kujiburudisha tu
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
   
Loading...