Kiswahili kuwa lugha rasmi ya mawasiliano UDSM

mzungukichaa

Member
Nov 8, 2010
57
27
Juni 16, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa bungeni alisema Serikali inatarajia kuanza kutumia Kiswahili katika mikutano yote ya kimataifa itakayowakilishwa na viongozi wake baada ya kutuma wataalamu watakaokitafsiri kwa watumiaji wa lugha nyingine duniani.

Katika kuunga mkono juhudi hizo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetangaza kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano chuoni hapo ikiwa ni kuunga mkono kauli hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Tawi la UDSM, Salifius Mligo jana alimpongeza Majaliwa kwa matumizi na kukuza matumizi ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

Alisema katika kutekeleza agizo hilo, UDSM kupitia baraza lake lililokutana Machi 30, mwaka jana lilipitisha makubalino ya kutumia lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano chuoni hapo.

Akizungumzia faida ya kujifunza lugha ya Kiswahili kama taaluma, Profesa Aldin Mutembei alisema inaongeza wigo wa ajira kutokana na kupanuka kwa matumizi ya yake katika nchi nyingi.

Alisema uamuzi wa kutumia lugha hiyo katika mikutano ya ndani na nje ya nchi utalitangaza Taifa.

Taratibu Minyororo ya kitumwa inaanza kulegea.
 
Good move!

Nimewahi kuhudhuria mkutano wa Watanzania , wakizungumza masuala ya maendeleo ya Watanzania lakini eti kwa Kiingereza. I was dissappointed !
 
  • Thanks
Reactions: ora
Good move!

Nimewahi kuhudhuria mkutano wa Watanzania , wakizungumza masuala ya maendeleo ya Watanzania lakini eti kwa Kiingereza. I was dissappointed !

Ndo tabia tumejengewa na mkoloni, kujidharau na kuona chako si kitu. Matokeo yake tumekuwa malimbukeni. Kibaya zaidi hata hicho kiingereza hatukijui...ovyo kabisa.
 
Chuo Kikuu cha Sokoine kifuate, maana huko ndiko wataalam wengi wa kilimo na mifugo wanakopikwa na kwa kuzingatia pia Watanzania wengi ni wakulima na wafugaji.

Serikali iweke utaratibu wa pembejeo zote za kilimo maelezo yaandikwe kwa Kiswahili ili hawa wataalamu waweze kusaidia wakulima matumizi sahihi.

Ufaulu utaongezeka kwani wanafunzi wengi wanashindwa kujieleza kwa Kiswahili kwenye mitihani ingawa wanaelewa kilichoulizwa.
 
Good move!

Nimewahi kuhudhuria mkutano wa Watanzania , wakizungumza masuala ya maendeleo ya Watanzania lakini eti kwa Kiingereza. I was dissappointed !
There is no good move wala good news hapo mkuu. Zaidi nikujiangamiza tu. Kwanza hatujajiandaa, tumekurupuka tu. Vitu kama hivi huhitaji maandalizi. Unajua tunahitaji vitu vingi ili hili suala liwezekane. Labda kama haitakuwa ya kufundishia. Kwa ulimwengu huu wa sayansi na technolojia unaongelea kuwa na lugha yako? kwa mfano termilogies za udakitari na ICT zitawafanya mshindwe tu. Mataifa yaliyo endelea yana embrace lugha zao kama lugha za mawasiliano vyuoni na mashuleni kwa sababu nyingi tu. Wanauwezo wa kuzalisha/kutengeneza vitu vyao ambavyo operational manuals zinakuwa na maelezo ya lugha zao. Je, sisi tunaotegemea ku import kila kitu hasa electonic equipment tunapo embrace kiswahili ni kweli tutaweza? Wanasiasa wetu na viongozi wetu wanakurupuka tu hata bila kufanya tafiti na kujilizisha faida na harasa za kuachana na lugha inayotumika kwa sasa. Wasomi wetu nao wamekuwa watu wa ndio Bwana mkubwa. Kila anachosema kiongozi wa siasa badala ya kumshauri kitaalamu ili ajue faida na hasara wao wanakupuka tu nao kusupport so long Bwana Mkubwa kishasema. Tutakuwa taifa la hovyo duniani kwani hakuna chochote tutakachoanzisha kikazaa matunda chanya.
 
Nitamuhamishia mwanangu Makerere au JKU! Siwezi kuzika kichwa changu kwenye mchanga mithili ya mbuni.
 
Ni lugha ya mikutano yaani mikutano ya Wafanyakazi, Haimaanishi kuwa ni lugha ya kufundishia. Jifunzeni kuelewa mada
 
Juni 16, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa bungeni alisema Serikali inatarajia kuanza kutumia Kiswahili katika mikutano yote ya kimataifa itakayowakilishwa na viongozi wake baada ya kutuma wataalamu watakaokitafsiri kwa watumiaji wa lugha nyingine duniani.

Katika kuunga mkono juhudi hizo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimetangaza kutumia Kiswahili kama lugha rasmi ya mawasiliano chuoni hapo ikiwa ni kuunga mkono kauli hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Tawi la UDSM, Salifius Mligo jana alimpongeza Majaliwa kwa matumizi na kukuza matumizi ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

Alisema katika kutekeleza agizo hilo, UDSM kupitia baraza lake lililokutana Machi 30, mwaka jana lilipitisha makubalino ya kutumia lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano chuoni hapo.

Akizungumzia faida ya kujifunza lugha ya Kiswahili kama taaluma, Profesa Aldin Mutembei alisema inaongeza wigo wa ajira kutokana na kupanuka kwa matumizi ya yake katika nchi nyingi.

Alisema uamuzi wa kutumia lugha hiyo katika mikutano ya ndani na nje ya nchi utalitangaza Taifa.

Taratibu Minyororo ya kitumwa inaanza kulegea.
Ni kuua elimu,
 
Ni lugha ya mikutano yaani mikutano ya Wafanyakazi, Haimaanishi kuwa ni lugha ya kufundishia. Jifunzeni kuelewa mada
Mkuu vijana wa Tanzania hawana akili ya kuelewa mambo! Wakishaona kichwa cha habari huwa wanakimbilia kwenye hitimisho! Aibuuuuu! Kumbuka upimaji wa virus ulivyopotoshwa!!
 
Sema tu ni kwasababu fulani lugha haipandi!
Siku graduate watakapoingia kwenye chumba cha usaili na kukumbana na ung'eng'e ndipo watagundua kwamba kumbe walikuwa wanapishana na gari la mshahara chuoni. Pamoja na haja ya kuutukuza utaifa wetu kwa lugha ya kiswahili lakini ukweli unabaki kwamba dunia ya leo tayari kuna lugha zilizoteka soko hivyo tufanye juhudi za kuenzi kiswahili kwa njia pana na siyo nyembamba. Kumbuka mchina alilazimika kuandika kiingereza...MADE IN CHINA bila kupenda.

Pia, kuna harufu ya unafiki juu yetu wenyewe maana kuna kila dalili kwamba wanafunzi wanaokwenda chuo kikuu mwaka huu hususani wanaokwenda kusomea lugha ya Kiswahili hawana nafasi kubwa ya kupewa mkopo hivyo huwezi kukuza lugha kwa kuongea tu mawasiliano ya kawaida tu maana hayo hata Manzese tumezoea. Lugha inahitaji utafiti, kuandikwa na kushupaliwa kupitia sanaa na taaluma
 
Back
Top Bottom