Kiswahili kutumika kama Lugha ya Kazi Umoja wa Afrika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali umeridhia na kupitisha ombi la Tanzania la kutaka Kiswahili kuwa lugha ya kazi katika Umoja huo, Dkt. Mpango amewasilisha ombi hilo la lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kazi katika mikutano ya Umoja wa Afrika.

Dkt. Mpango ameongeza kuwa Kiswahili ni miongoni mwa lugha za kiafrika zenye wazungumzaji wengi barani Afrika ambapo takribani watu milioni mia moja wanakitumia Kiswahili pamoja na wazungumzaji kutoka nje ya Bara la Afrika.

Kutokana na umuhimu wa lugha hiyo Makamu wa Rais amesema tayari inatumika katika jumuiya mbalimbali ikiwemo jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na kufundishwa kwa lugha hiyo katika nchi nyingi za Afrika Mashuleni.

Amesema tayari Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni limetangaza tarehe saba Julai ya kila mwaka kuwa siku ya maadhimisho ya lugha Kiswahili Duniani, Mkutano huo pia umeichagua Tanzania kuwa mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU)

Source: Milard Ayo
 
Safi sana
Ni hatua nzuri ktk kukikuza kiswahili
Ni muhimu sana taasisi zetu za Lugha ya Kiswahili kujikita kufanya maboresho mbalimbali
 
Back
Top Bottom