Kiswahili kumbe hakieleweki hata hapo kwa jirani Malawi, tunakikuza kuliko uhalisia, ni ajabu

Malawi ,zambia na msumbiji hawajui kabisa kishwahil except baadh yavijij vya mipakan mle
Zambia nakonde tu apo hawajui kishwahil
Malawo chitipa ndo hawajui kishwahil

Sio kweli ukiwa mfano ukiwa msumbiji unakuwa safe zaidi ukijua kiswahili even wao wenyewe wanapenda kiswahili kuna miji kama Nampula pemba na montepuez iko mbali na Tz na wanaongea kiswahil msidanganye watu
 
sasa mbona hueleweki Mkuu? Kiswahili kinazungumzwa nchi nyingi wakati hata majirani wa karibu tu hapo hawakijui?
Au kwa kuwa unaona wazungu wakizungumza Kiswahili unasema basi kimeenea Duniani? Wazungu wanazungumza hadi kinyarwanda, so utasema kinyarwanda kimeenea Duniani?
Mkuu labda sijaeleweka. Hoja yangu ni kwamba kuzungumza lugha yoyote, iwe Kiswahili au nyingine, ikatafsiriwa kwa lugha ya pili sio lazima iwe wasikilzaji hawailewi. Hii hufanywa iwapo lugha hiyo ama sio lugha ya taifa au sio lugha rasmi. Malawi Kiswahili sio lugha ya taifa wala sio lugha rasmi, ndo hotuba ya uncle ilifasiriwa kwa lugha ama ya taifa au lugha rasmi. Naelewa, ingawa sina hakika, lugha rasmi ya Malawi ni Kiingereza, lakini pia Chichewa ama ni lugha ya taifa au ni moja ya lugha rasmi za nchi hiyo. Hivyo sio ishara tosha kwamba watu/wasikilizaji walikuwa hawaielewi lugha ya Kiswahili. Vyovyote iwavyo, uncle katika hili anaikuza lugha ya Kiswahili, iwe anajua au hajui lugha ya Kiingereza KWA UFASAHA
 
Hawawezi wakawacheka, kisa rais kaongea kiingereza kibovu sababu wao sio wajinga kama nyinyi.

Maana hapa pia mnaponda rais kuongea lugha yake.
Mkuu nakuhakikishia michepuko watatuponda kwamba rais wetu kaongea broken,huwajui wamalawi wewe,watanzania tunaafadhari,right ungejua wanavyomponda Prof APM ?
 
Hawa jamaa wana lugha nyingi sana,kinyanja,kichewa,kitumbuka na Kiingilishi.....Kiswahili ni ngumu kutoboa,ila kwasasa waTz niwengi so kinasogea kiasi
 
Mkuu nakuhakikishia michepuko watatuponda kwamba rais wetu kaongea broken,huwajui wamalawi wewe,watanzania tunaafadhari,right ungejua wanavyomponda Prof APM ?
Basi watawazomea na kuwaacha mtakapowaambia rais wetu hajui kabisa kuongea kiingereza. Akaongea lugha ya kiswahili.
 
Mkuu labda sijaeleweka. Hoja yangu ni kwamba kuzungumza lugha yoyote, iwe Kiswahili au nyingine, ikatafsiriwa kwa lugha ya pili sio lazima iwe wasikilzaji hawailewi. Hii hufanywa iwapo lugha hiyo ama sio lugha ya taifa au sio lugha rasmi. Malawi Kiswahili sio lugha ya taifa wala sio lugha rasmi, ndo hotuba ya uncle ilifasiriwa kwa lugha ama ya taifa au lugha rasmi. Naelewa, ingawa sina hakika, lugha rasmi ya Malawi ni Kiingereza, lakini pia Chichewa ama ni lugha ya taifa au ni moja ya lugha rasmi za nchi hiyo. Hivyo sio ishara tosha kwamba watu/wasikilizaji walikuwa hawaielewi lugha ya Kiswahili. Vyovyote iwavyo, uncle katika hili anaikuza lugha ya Kiswahili, iwe anajua au hajui lugha ya Kiingereza KWA UFASAHA
Sasa kama lugha inaeleweka na wengi point ya Kuitafsiri ni nini?

Lengo kuu la kugha ni kuwasiliana, kama inaeleweka iwe official ama sio official kama inaeleweka mkalimani haitajiki

Na simaanishi kuwa Malawi hawaelewi Kiswahili wote, ila wanaoielewa ni wachache
 
Tofautisha lugha inayokuwa kwa kasi na kuongelewa sehemu nyingi kwa upande wa lugha za Africa kiswahili ndio lugha rasmi inayojulikana kimataifa kusema malawi hawaongei sio kipimo kuwa kiswahili hakiongelewi nimekaa msumbiji provincial ya cabo delgado yote wanazumza kiswahili na cha kushangaza kuna miji ambayo ipo mbali na mpaka wa Tanzania na msumbiji wanazungumza kiswahili...juzi Roma wakati wa kujiandaa na pasaka chuo cha st. Anselm waafrica wanaosoma hapo waliamua kusali misa kwa kiswahili kama lugha pekee rasmi kutoka Africa...sào paulo Brazil nimeshuhudia watoto wakiimba kwa lugha tofauti duniani na wakaimba pia kwa kiswahili unataka lugha hii ikue kwa kiwango kipi? jivunie cha kwako then fanya tafiti kwanza kabla kusema jambo fulani
Ujue tungekuja na utafiti wenye takwimu kidogo ndio huu mjadala ungekuwa na mashiko kuliko maneno matupu

Hapa nime search mtandaoni nikaona 0.1% ya Watu wa Msumbiji ndio wanaojua Kiswahili hii ilikuwa ni takwimu zilizokusanywa mwaka 1998, japo inawez kuwa idadi imepanda haiwezi kuzidi 10%
Waongeaji wengi ni wa mpakani, ukienda ndani haeakielewi, so mtu unaweza ishi kwenye sehemu ipo mpakani wakawa wanazungumza Kiswahili ukadhani ni nchi nzima
 
nilikuwa huko mwaka jana bro japo sina takwimu halisi ila kwa kweli sikupata shida sana
 
Back
Top Bottom