Phinna
Member
- May 31, 2017
- 12
- 6
Habari wana jf
Ni matumaini yangu sote tunaendelea vizuri na majukumu yetu mbalimbali yanayotukabili. Lakini pia hatukosi muda wa kukutana hapa jamvini na kupeana mambo kadha wa kadha.
Leo hii mimi napenda kuongelea mwenendo wa lugha yetu hii adhimu ambayo imetufanya kuwa na utambulisho wetu katika mataifa mengine kutokana na kuitumia sana kama lugha yetu ya taifa. Nayo si lugha nyingine bali ni lugha ya Kiswahili. Mwenendo wa watumiaji wa lugha hii hasa hapa kwetu Tanzania ambapo naweza kupaita ndiyo makao makuu ya lugha hii, ndipo Kiswahili kimeanza kuharibiwa tena kwa kasi ya ajabu.
Kila lugha ina nahau zake, misemo yake na hata methali zake, lakini jambo linaloshangaza sana tumeanza kuona vya kwetu havifahi na kuanza kurukia yaliyoko kwenye lugha ngeni. Hapa chini naorodhesha baadhi ya makosa ambayo nadiriki kuyaita ni ya makusudi kabisa ambayo yanaweza kusababisha kupotea kwa uhalisia wa Kiswahili kutokana na kuharibiwa sarufi yake.
1: Neno "pelekea"-Kisarufi neno hili linamaana nyingi. Neno hili ni mnyumbuliko wa neno peleka. Lakini sasa linatumika kwa maana ya "sababisha", jambo ambalo si sahihi. Wamegeuza maneno ya Kiingereza "lead to" ambayo tafsiri yake sahihi ni sababisha watu wakatafsiri neno lead kwa Kiswahi pasipo kujua kuwa "lead to" ni clause ambayo kwa Kiswahili ni sababisha.
Ni jambo la kawaida sasa kumkuta mtu hata kama ni msomi wa kiwango gani, mwana habari au mwandishi wa vitabu naye akitumia lugha hii "hiki ndicho kilichompelekea kukamatwa" badala ya "hiki ndicho kilichosababisha akamatwe".
2: All in all- Nimewasikia watu wengi wakihangaika kutafsiri maneno hayo kwa Kiswahili. Utamsikia mtu anasema "yote katika yote". Hivi kweli tangu shule ya msingi hadi ya upili, umewahi kukutana na maneno kama hayo katika Kiswahili? Au tukifika Chuo Kikuu ndiyo tunatengeneza Kiswahili kipya?
3: Kuna lugha nyingine sasa inazaliwa tena na kukuwa kwa kasi. Sijui lugha hii itaitwa je! Eti unamkuta mtu anaongea kwa madaha kweli kweli, "atleast angalau", "sorry samahani", "infact kwa kweli". Hii ni Lugha gani?
4: Kuna tatizo ambalo sasa ndiyo limeanza kuwa sugu kama malaria, nalo ni kuchanganya herufi. Panapotakiwa kuweka "r" mtu anaweka "l" na kinyume chake. Athirika mtu anaandika adhirika. Hivi hata kama wewe unatokea kaskazini, ndivyo ulivyofundishwa darasani?
Jamani nawaombeni Waswahili wenzangu, tuipende lugha yetu isije kupotea ikazaliwa lugha mpya isiyokuwa na maana. Nakumbuka hayati Baba wa Taifa aliwahi kusema wasomi ndiyo watu wa kwanza kukiharibu Kiswahili. Kuchanganya lugha si alama ya usomi. Ni hayo tu jamani.