Kiswahili kitamu kutoka congo

matubara

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
226
88
Wadau nimekuwa nawafuatilia sana watangazaji wanaoripoti kutoka Kinshasa na kwa hakika kiswahili chao ni cha kukufanya ucheke! Ebu angalia mifano hii kisha na wewe utupie ulichosikia:
1.Askari thelathini waliuwawa - Masoje makumi matatu walikufishwa
2. Wanasiasa - Wafanya siasa
3.Upande wa upinzani - Ng'ambo ya upinzani
4.Mara kwa mara - Maya kwa maya
 
Mie niliisikia "nina miaka makumi matano na kenda" nikenda ngoe :glasses-nerdy:
 
Machozi imejaa macho baridi mu mwili ~ macho yamejaa machozi na mwili unasikia baridi
 
Madawa yenye kulefisha - mihadarati
Charanga fiboko kumafi - viboko vya kwenye masaburi
 
leo ni tarehe makumi moja na mamoja tisa kwa mwezi tulionao, mwaka elfu mbili na makumi moja na mamoja mbili [19.08.2012].!!!!!
 
Uchunguzi mwingi uliofanyika wa lugha ya kiswahili ulishaonesha kuwa wa Kongo ndiyo wanazungumza kiswahili asilia, kwani huko kwao ndipo kilipoanzia. Tofauti iliyotokea ni kuwa kiswahili cha pwani baadaye kiliingiza maneno mengi ya kigeni- hususan Kiarabu, Kireno, na Kijerumani na ndiyo kikazaliwa hiki kiswahili ambacho wengi wetu wanahisi ndiyo fasaha.

Hata mimi naamini hivyo kwani Kiswahili cha Kongo kina maneno karibu yote ya Kibantu wakati hiki tunachotumia viraka ni vingi tu (maneno mengi ni ya kuazima). Kitu cha muhimu ni kuwa Kongo wanazungumza kiswahili chenye lafudhi ya bara na siso wengine tunazungumza kiswahili cha lafudhi ya mwambao, ambacho kiliendelezwa zaidi na wafanyabiashara miaka iliyopita.

Ahsanteni.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom