Kiswahili kinakosa nguvu za kiuchumi

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,449
2,113
Kiswahili hakijaenea leo wala jana kuingia Bara na sehemu nyingi za Afrika kwa ukubwa kiswahili kilienea karne ya 20 (Wakati wa wakoloni hasa waingereza na wengineo).

> Shughuli za kiuchumi hasa biashara ilisaidia pakubwa lugha ya Kiswahili kupiga hatua katika karne hiyo ya 20. Nami Nafikiri hata Leo Nguvu za kiuchumi zinaweza kukisukuma kiswahili zaidi ingawa nilipolisema hili siku moja katika mjadala wa DW, Profesa Clara Momanyi na Mwalimu Abdilatif walikuwa na mitazamo tofauti. Sidhani kama miktadha ya Akademia pekee itafaulu kukieneza kiswahili duniani.

> Vyombo vya habari kwa sasa sidhani kama vina nafasi kubwa ya kueneza Kiswahili. Vyombo vingi ni vya hapa hapa na hata idhaa za kimataifa zinazorusha matangazo yake kwa kiswahili zinalenga eneo hili la maziwa makuu. Je, hilo ndilo lengo letu Kiswahili kienee tu Afrika Mashariki?

Hata hivyo kungali kuna nafasi ya kutumia vyombo vya kimtandao vinavyofikiwa na watu wote duniani (Heko kwa jamii forum kuwa mtandao wenye maandishi mengi ya kiswahili kuliko chombo chochote duniani)

Hoja yangu ni kuwa kiswahili kinahitaji kuwekezwa na kuenezwa zaidi kiuchumi.

Napenda kutoa mfano , Kampuni kubwa ya matangazo ya Biashara Google AdSense haikitambui kiswahili katika program zake za matangazo ya kidigital na wakati huo huo wanapokea matangazo ya Kiswahili. (Hawaweki matangazo katika tovuti za kiswahili lakini huweka matangazo ya kiswahili katika tovuti za lugha nyingine hata zenye wazungumzaji wachache kuliko idadi ya wazungumzaji wa kiswahili)

Sababu ni nini? utafiti wangu haujakamilika Lakini sababu ya haraka inaweza kuwa kiswahili kinakosa nguvu ya kiuchumi. Kwasababu hakijawekezwa vyakutosha kiuchumi na kuenezwa kiuchumi kwa sasa. Tunapaswa kujua kuwa Kingereza watu hawajaamka wakakuta kimeenea walifanya kazi kubwa kuieneza lugha yao, waliunda mashirika yenye nguvu kama British Council, na ukuaji wa uchumi wao ulienda sambamba na ukuzaji wa lugha yao na ndiposa lugha yao inamashiko kibiashara miongoni mwa lugha nyingine.

> Pengine wageni wengi wanaojifunza Kiswahili kwa sasa ni watafiti na wanafunzi wa masomo ya lugha za kiafrika labda pengine na Usalama , mambo Haya pekee hayatoshi kueneza Kiswahili. Ninadhani kiswahili kinapaswa kuwa na mvuto zaidi kibiashara rejea kiswahili kilivyoenezwa nyuma na sasa kama hutaona kuwa wakoloni walifanya kazi kubwa kwa kipindi kifupi kuliko Sisi kwa kipindi kirefu.

Muda ungalipo, Nchi zenye hati miliki ya kiswahili ziamke. 1, kwanza Kiswahili kitambulike kikatiba kuwa ni lugha ya Taifa la Tanzania, kama ilivyo Kenya na Uganda.

2. Serikali hizi ziwekeze kweli kweli kiuchumi katika ukuzaji wa lugha hii. (Lugha ni uchumi hakuna lugha inayoenda hivi hivi yenyewe tu, lugha inabebwa kiuchumi na mwisho inakubeba wewe na uchumi wako , Prof Kai Mutembei).

3. Utekelezaji wa Sera mf 2014 kuhusu lugha ya kufundishia

4. Mashirika yanayohusika na ukuzaji wa Kiswahili yakumbushwe upya majukumu yake.

Mwisho.
"Ukuzaji wa Kiswahili ni lazima uende sambamba na ukuzaji na uwekezaji wa kiuchumi "

#mashelekiswahili
#mawazohuru
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom