Kiswahili Kimezidi Mno Kuelemea Kwenye Kiarabu Zaidi Ya Kibantu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili Kimezidi Mno Kuelemea Kwenye Kiarabu Zaidi Ya Kibantu

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Steve Dii, Feb 13, 2009.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwanza kabisa napenda nianze kwa kukili kuwa Kiswahili bado ni lugha inayonipiga chenga pahala pengi. Hivyo kuna pahala pengi katika hoja yangu nitachanganya na lugha ya Kiingereza, pamoja na kwamba ningelipenda sana kuepuka. Lakini hilo lingewezekana tu kama ningelikuwa na muda na uwezo wa kupangilia na kukumbuka maneno fasaha ya kutumia. Pia nakili kuwa hii hoja sijaifanyia utafiti madhubuti kuhakikisha kuwa ina vielelezo vya kutosha ili kuchanganua na kufafanua mifano mbalimbali ambayo inaweza kutumika kuikoleza na kuipa msingi zaidi hoja yenyewe. Ni imani yangu kuwa wale walio bobea kwenye maswala ya lugha wanaweza kuiendeleza zaidi. Shukrani.
  ------------------ ***** --------------

  Nitaanza;

  Nikisema 'ngoko' au 'nkoko' Wasukuma, Wahaya na ninaamini makabila mengine mengi ya Tanzania wataelewa kuwa ninalotaka kulitaja ni jina la ndege tumjuaye kama 'kuku' kwa Kiswahili. Si makabila ya Tanzania tu, bali Wabemba wa Zambia, Washona wa Zimbabwe, Baganda wa Uganda nao wangelielewa.

  Nikisema 'nzoka' au 'nyoka' vivyo hivyo makabila mengi yenye asili ya Kibantu yatanielewa.

  Sawa, lugha nyingi zinakua na kuendelea kwa kuazima maneno kutoka kwenye lugha nyingine. Na maneno mengine yanajitokeza na kukua na kukubalika kama moja ya maneno ya lugha fulani kutokana na mazingira yanayozungukuka jamii.

  Maneno kama 'swahiba', 'mstakabali', na mengine mengi yenye kusikika na kutamkwa kwa lafudhi ya pwani asili yake kubwa ni kutoka Kiarabu. Na ukweli wa mambo ni kwamba chimbuko la lugha ya Kiswahili ni lugha ya Kiarabu.

  Hoja yangu: Je, chimbuko la lugha yetu ambayo tumerithi, tumejifunza, tumeikuza na kuienzi ndiyo kipimo pekee cha uhalisia wa maneno tuyatumiayo katika Kiswahili chetu?

  Kimfano, nasema hivi kwani leo hii nikija na neno fulani hivi kutoka katika lugha ya Kihaya na neno hilo hilo kuwa tafsiri ya kitu ambacho kinapatikana Uhayani lakini hakipatikani katika Pwani, lakini hapo hapo kitu hicho kikabahatika kuwa na tafsiri yake katika lugha ya Kiarabu; uwezekano wa neno la Kiswahili kutumia (au hata kunyambulisha tu hilo neno la Kihaya ili iwe tafsiri yake katika Kiswahili) neno la Kihaya ni mdogo kuliko ambavyo urithi au ukubalianaji wa tafsri ya neno hilo ungelikuwa ule wa kutoka kwenye neno la Kiarabu.

  Sasa, hii (sijui niite dosari) favouritism ya Uarabu dhidi ya Ubantu inatokana na nini, is it the case for inferiority complex ya aina fulani hivi, elimu au nini haswa?! Kwanini tunaenzi sana maneno kutoka Kiarabu kuliko maneno ambayo yana maana ileile kutoka lugha zetu za Kibantu. Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day.

  "Akhsanteni", "Shukrani", natanguliza "Fadhila" zangu, au basi niseme... "ndaga fijo", "mwabeja"?!

  SteveD.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Steve,

  Hii mada inaturudisha katika historia nzima ya Kiswahili. Kama unavyoweza kuwa unafahamu, Kiswahili ni "lingua franca" lugha iliyokuzwa na biashara katika Pwani ya Afrika Mashariki. Kutokana na hili, kiarabu kilikuwa na mizizi mirefu mapema sana katika Kiswahili. Kiswahili, tofauti na Kifaransa, hakina chombo kinachokipangia msamiati na matumizi fasihi, hata Baraza la Kiswahili halina kazi hii kwa mujibu wa nielewavyo. Katika hili Kiswahili kiko sawa na Kiingereza, lugha nyingine iliyokuzwa kwa kuchanganywa sana na lugha nyingine za Kihindi-Kiulaya (Indo-European languages) hususan Kijerumani (the Saxon in "Anglo-Saxon") na Kilatini.

  Ukweli ni kwamba huwezi kuongelea Kiswahili kiujumla bila kuhusisha lahaja unayozungumzia. Kwa sababu za kihistoria na ki Jiografia, lahaja za pwani (Kiunguja, Kitumbatu,Kimrima, Kimakunduchi, Kimgao, Kipemba, Kimvita zimepatwa na mvuto wa kiarabu zaidi kutokana na kuwa pwani, lakini lahaja kama za Kingwana za huko DRC ziko kibantu zaidi. Na maneno mapya mengi ya Kiswahili yanakuwa na tashtiti za kibantu zaidi kama si Kiingereza.

  Uzuri au ubaya wa Kiswahili ni kwamba lugha hii inakua kiasili, bila kuingiliwa. Nyerere katika jitihada zake zote za kukuza Kiswahili hakuwahi kukibadilisha na kukilazimisha kwa watu kama alivyofanya Mustapha Kemal Ataturk kwa Waturuki baada ya kuudondosha utawala wa Ottoman.

  Kwa hiyo ukiangalia muelekeo, Kiswahili kilikuwa kinavutwa zaidi na kiarabu zamani kuliko hivi sasa, sasa hivi muelekeo unaenda kwenye Kiingereza (sijui kama kumbadilisha muarabu na muingereza ni kitu kizuri) na maneno yanayotamkika kibantu.

  Kitu tunachoweza kujifunza kutoka katika Kiingereza ni kwamba hata lugha hii ya watawala wa dunia ilibidi kukubali mabadiliko makubwa sana kutoka Kiingereza cha zamani mpaka hiki cha sasa.Katika Kiingereza cha sasa ni vigumu kuandika sentensi ya maneno kumi bila kutumia neno lenye msingi wa kilatini.

  Labda tabia moja isiyoepukika ya lugha zenye mafanikio ni kuweza kutohoa vizuri.
   
 3. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni ulimbukeni!

  Limbukeni, limbukeni!

  Eti unasema "Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day."

  Mtanzania na utashi wako unadiriki kusema kiswahili kinakupiga chenga na utakaposhindwa utatumia kiingereza? Hicho kitu hapo juu ndo huwezi kukisema kiswahili? Acha kupotosha kwamba umejaribu kuepuka. Hujajaribu!

  Tumenyanyaswa na mabeberu wa Magharibi, tukapelekwa Uarabuni wakatukata mapumbu tusizaliane, tukapelekwa Marekani kutumikishwa kwenye visiwa vilivyoibiwa kulimishwa miwa na tumbaku na kuchapwa mbakora kama punda, halafu leo unatamka hadharani kwamba lugha ya Mama yako huijui vizuri na ukishindwa utatumia ya watwana na mabwana wa magharibi!

  Wewe ni mfano wa kitabuni wa saratani ya ulimbukeni.

  Huna soni!
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sawa Kuhani. Mimi limbukeni nisiye soni. Naomba mchango wako kwenye hoja yangu. Shukrani.
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tutaendeleaje kujadili mada wakati tabia inayopingwa ni ya kilimbukeni na anaepinga anajua, anakubali, kwamba yeye ni mfano wa kitabuni wa saratani ya ulimbukeni?

  Tutakuwa wanafiki kenyekenye.

  Anza upya!
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Lugha kubwa (zenye maneno mengi zaidi au zitumiwazo na watu wengi zaidi duniani) karibu zote, zina maneno ya kutokana na lugha zingine. Sijakutana na lugha ya kimataifa ambayo haina maneno ya lugha zingine.

  Ki-swahili kina asili mia kubwa ya maneno yatokanayo na Kiarabu kwa sababu ya misafara mingi ya baharini kati ya nchi zinazo-ongea kiarabu na pwani ya Afrika Mashariki, toka enzi na enzi, hakuna ajuaye mwanzo wake.

  Ki-swahili pia kina maneno yatokanayo na ki-hindi, ki-reno, ki-china na kadhalika. Na pia lugha zingine zote za kimataifa utakuta zipo hivyo hivyo.

  Kiswahili kuwa na asilimia nyingi ya maneno ya kiarabu pia imechangiwa na kuwa, si zamani sana toka kiswahili kianze kuandikwa na herufi hizi za kilatini tuzitumiazo kwa sasa, kabla ya hapo kiswahili kilikuwa kikiandikwa kwa kutumia herufi za kiarabu. Na mpaka sasa wazee wengi wa pwani ya Afrika Mashariki hutuia herufi za kiarabu kuandika kiswahili.

  Sidhani kama itatokea kuweza kukiondowa kiswahili kabisa kutoka kwenye uarabu, kwani hata neno lenyewe ki-''swahili'' ni la kiarabu likimaanishi kando kando ya bahari au pwani kwa kifupi.

  Ki-swahili ni luugha yenye chipuko kutoka mwambao wa bahari ya hindi kuanzia Somalia mpaka Mozambique, kwa hiyo kiswahili ni lugha ya mwambao, na ni raha zaidi utaposikia watu wa mwambao wakiiongea kuliko wakiiongea watu wa bara.

  Natamani nimsikie Msukuma (ambae hajaishi mwambao) akisoma mashairi ya ki-Swahili.
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sitoanza kwa matakwa yako. Naamini kuna WanaJF watakayoichukulia hoja yangu kimsingi na kuijibu kama hoja iliyokamilika.

  SteveD.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280

  Labda ingekuwa vigumu zaidi kujadili mada kama mtoa mada asingekubali kwamba yeye ni limbukeni kuliko hivi sasa ambapo mtoa mada amekubali.

  Katika kukubali kwake ulimbukeni, tumeona mizizi ya ulimbukeni ilivyokuwa mirefu, kiasi cha kwamba hata mtoa mada inayopinga ulimbukeni ametumbukia katika ulimbukeni ulio katika nusu-ufahamu wake.

  Kanuni tunayojifunza hapa ni kuwa ulimbukeni unaenda mbali sana, na kama hata anayeleta mada ya kupinga ulimbukeni anaweza kutegeka na mtego wa ulimbukeni, mkosoaji mleta mada inayopinga ulimbukeni kwa msingi wa kwamba mleta mada inayopinga ulimbukeni ameileta mada iliyochanganya na ulimbukeni naye pia hayuko juu ya kuanguka katika mtego wa ulimbukeni.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unajuwaje kama kugha ya mama yake ni ki-Swahili? wacha lawama zisizo na msingi, kuna watanzania wengi hii leo hawajui ki-swahili na kuna wengine wanajuwa kidogo sana, tembea Tanzania hii ukaone.
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  .... :) :) acha uchokozi DSM, watajitokeza hapa utakimbia mwenyewe!!! lol
   
 11. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sawa, Kiranga, ni kwa vipi aliyemkosoa limbukeni mleta mada pia hayuko juu ya mtego wa ulimbukeni?
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Hakuna mwana-adamu aliye juu ya mtego wa ulimbukeni, maadam unaishi siku yoyote unaweza kuuonyesha ulimbukeni wako, kizuri ni kujifunza.

  Ulimbukeni unakuja kwa sura nyingi, naamini sana katika kukosoana, lakini kuwa na asili ya ubishi uso kipimo, kutokuwa na tabia ya kuchukuliana, kushailoki, kuona maovu tu kunamuweka mkosoaji mtoa maada katika mtego mkubwa wa ulimbukeni kuliko ule wa mtoa maada.

  Nuita huu ulimbukeni wa ujuaji, ambao kwao tunachofikiri tunakijua kinatupa ujivuni wakati kwa kweli kujua ni kitendawili cha kifalsafa.

  Hakuna kujua :) Tunajifunza tu.

  Heck, hakuna kujua hata kwamba hakuna kujua!
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuto kujuwa ki-Swahili nawe um-Tanzania si ulimbukeni, Kiswahili toka kiwe lugha ya Taifa la Tanzania si miaka mingi sana, nadhani hata hamsini haijafika. Nadhani ni baada ya mwaka 1961 ndio ki-Swahili kikaanza kuwa lugha ya Taifa. Kabla ya hapo, ki-Swahili kilikuwa kikiongewa sana kwenye ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na katika miji mikubwa ya biashara kuingia bara.

  Kwa miaka chini ya 50 kuwa kugha ya Taifa ni michache sana kwa nchi yenye lugha zaidi ya mia moja kukifanya kiwe lugha mama ya kila m-Tanzania.

  Lugha mama ni ile unayoisikia toka unazaliwa, kuna makabila mengi Tanzania yanajivunia lugha zao za asili kiasi cha kwamba, kuna wa-Tanzania wengi mpaka leo hii, huanza kujifunza ki-swahili wanapoanza shule, hao huwezi kusema kuwa ki-swahili ni lugha yao mama. Kwa wao kutokujuwa ki-swahili fasaha si ulimbukeni, ulimbukeni ni kuanza kushambulia mtu bila kuwa na mantiki.
   
 14. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  STEVE D unaelewa nini hasa kuhusu lugha ya kiswahili na chimbuko lake pili unaelewa kuwa kiswahili hapa TANZANIA hakikuwa kinazungumzwa na watu hote tatu nenda katafute kumbukubu za mwali julis utakuka ni siku gani mwalimu alitangaza rasmi kutumika kiswahili kama ndio lugha ya taifa ?naimani itasaidia kuelewa chimbuko lake
   
 15. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  "Unajuwaje" ndio nini?

  Na wewe hukukulia wanapoongea kiswahili, au?

  Kama wewe na mtoa mada mmekulia sehemu ambazo lugha ya Mama haikuwa Kiswahili halafu mnajua na mnatumia kiingereza maana "kiswahili ni lugha inayonipiga chenga" ina maana mmeruka, mkakimbilia kujifunza lugha za mbali za kigeni kabla ya ile ya karibu, ya Taifa.

  Na huo ndio utako wa ninachosema: Malimbukeni!

  Wapo ndio, mko wengi, ndio maana tatizo la ulimbukeni wenu nimelipa mfano wa saratani, limeenea.
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kiranga, nashukuru kwa hili. Kuhusiana na ndugu Kuhani kuna mengi yameandikwa jamvini hapa kuhusiana na misimamo yake.Pia kuna mengi ameandika ambayo yanaelezea misimamo yake. Nathubutu kusema kuwa, misimamo yake mingi ni yenye ku-challenge fikra na ukiipima ni yenye manufaa overall.

  Hata hivyo pahala pengi provocative language anayotumia inafanyika makusudi, kwa malengo ya kukatisha tamaa au kukomoa kwa maneno ya kejeli na yaliyojaa dhihaka dhidi ya wale anaowalenga. Na mara nyingi anachagua target, again kwa makusudi kabisa. Tatizo ni pale unapojitokeza kuonesha mapungufu yake, ni vitisho na visa vinafuatia kwa almost kila utakachokiandika baada ya hapo. Nadhani ni sahihi kusema kuwa ni mtu ambaye anaamini kwenye 'infallibality' and may be thinks he's one.

  Mkuu, mimi nachukulia kila post kama vile ni mtu mpya amejiunga na kutuma maoni yake. Hivyo, hata kama kwamba ni mmoja wa wanaJF ambao wamekumbana na visa vyake, kwangu mimi kila atakachoandika nitakisoma na kukichukulia kama post ya mwanachama mpya na inayohitaji kuwa judged by its own merit, jambo ambalo wengine laweza kuwaghafrisha.

  Ahsante.

  SteveD.
   
 17. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sonara, challenge kubwa hii na nina ahidi kuijitahidi kuitekeleza. Ahsante.

  SteveD.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Limbukeni utamjuwa kwa ulimbukeni wake. Hata namna ya kujieleza imekaa kilimbukeni-limbukeni.

  Kwetu hunena ''Mwenda tezi na omo marejeo ngamani''
   
 19. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  SteveD,

  Mada ya mjadala wako ni Kiswahili na kutukuzwa kwa asili za kigeni au mada yako ni kumjadili mchangiaji aliyepinga ulimbukeni wa kukemea ulimbukeni wakati mwenyewe u mfano wa kitabuni wa tatizo?
   
 20. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mada hiii HAPA , unaweza kuisoma tena na kung'amua mwenyewe. Shukrani.
   
Loading...