Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,783
- 1,822
Kama kuna wakati kiswahili kimejishushia hadhi kimataifa, ni kipindi hiki kwa kuwa na salaam ya utata. Nilimuonea huruma Palamagamba Kabudi akihutubia wageni waalikwa wa nchini na wa-kimataifa wakiuga mwili wa marehemu Mh JPM, huku akianza kwa kuwasalimia " Asalaam aleykum na baadae Bwana yesu asifiwe". Nilimuona Uhuru Kenyata akishangaa! Katika kuwakaribisha viongozi wa dini kuoma dua, akamkaribisha mkuu wa Hindu Mandal sijui mkuu huyo alijisikiaje maana alitengwa katika salamu ya Kabudi hapo awali.
Kiswahili ni lugha kitaifa isitekwe na akina Gwajima na kundi lake. Hata kama kusalimiana Asalaam aleykum (amani iwe juu yenu) kulikuwa na makosa, ni vyema kutafuta salamu mbadala na sio kuongeza kosa zaidi kwa kuwapendeza kikundi fulani. Hili lilikuwa kosa kubwa sana, amalo BAKITA lazima ilirekebishe hasa katika salamu za kiserikali, kitaifa n.k.
Hii haiwakatazi watu huko mitaani kusalimiana - Bwana yesu asifiwe au Asalaam aleykum, lakini kitaifa ni muhimu kuwa na salamu maalum ambayo haitaitenga kundi fulani. Kwa mfano tukisema JAMBO, HABARI HATA SALAMU ZA KABILA MOJA ILIYONYOOKA , lakini isiwe na ishara ya kulenga imani fulani.
Ni wakati muafaka sasa hivi kutafakari na kupeleka mswaada Bungeni ili suala hili litafutiwe muafaka wa kisheria. Nawasihi watanzania wenzangu kulitazama hili kwa jicho la Tatu na kuitazama Tanzania kama nchi yenye dini zaidi ya mbili.