Kiswahili enzi za ukoloni

misha

Member
Nov 19, 2010
59
0
Hayati Bibi Titi Mohamed alipojiunga na TANU alimshauri Hayati Nyerere alifunze Kiswahili, binafsi nimekuwa nikijiuliza na kuduwaa kwa hili, maana Wakoloni kuanzia Wajeremani walijifunza na kufundisha Kiswahili .
JF ni jamvi la kuuliza na kupata habari, kwa hiyo naomba kuuliza, kiwango cha ufahamu wa lugha ya Kiswahili kwa mtu aliyekuwa na kiwango cha kisomo cha Hayati Mwalimu Nyerere au Kiswahili alichokitaja Hayati Bibi Titi ni kitu kingine tofauti kabisa? Naamini kuna watu wengi sana Tanzania waliomfahamu Mwalimu kama mwalimu wakati akiwa TBR na Pugu, hivi, Kiswahili chake kilikuwa hoi kiasi hicho.Nitashukuru kusikia zile hotuba za awali za Mwalimu wakati wa TAA na TANU kabla ya tamko la Bibi Titi.
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,610
1,500
Kama Nyerere alichelewa kujifunza Kiswahili amefaulu vema, sivyo?
Kwa upande mwingine: Je unan uhakika Bibi Titi Muhammad alimshauri ajifunze Kiswahili gani?

Maana Nyerere alikuwa mtu wa bara labda alimshauri kuzoea Kiswahili cha pwani? Maana najua Kenya hadi leo watu wa pwani na wale wa bara unasikia tofauti wakiongea Kiswahili.
 
misha

Member
Nov 19, 2010
59
0
Asante sana ndugu Kipala, hata mimi nimejuliza kwa maana Bibi Titi alipomshauri, Mwalimu Nyerere alikuwa Pwani karibu miaka minne na sitegemei kuwa alikuwa anaongea lugha nyingine katika maswala ya TAA na TANU, zaidi ya Kiswahili. Hayati Bibi Titi aliliongelea hili(kumshauri Mwl. kujifunza Kiswahili ) kwenye makala kadhaa kuwa Mwl. hawezi kuendelea kuongea na wananchi kwa namna ile aliyokuwa akiitumia, mwanzoni nilidhani labda Mwl. alikuwa anajinoa kama 'orator' na Titi aliyekuwa msanii mahiri alitaka amnoe ktk hilo, lakini nikakuta ripoti za umahiri wake katika hilo na alikuwa mchangiaji kwenye gazeti za Zuhura-la Kiswahili.
Kiswahili cha Mwl. kilikuwa cha kibara zaidi kuliko kipwani-kimatamshi kwa kipindi alichokuwa Rais hadi kustaafu,hili sidhani kuna mtu atakataa.
Kwangu mimi kauli ya Bibi Titi imebaki kuwa ni swali na kitendawili
 
Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,610
1,500
Labda nyingine. Mwalimu alijifunza Kiswahili kama sijui lugha ya pili au ya tatu. Sasa akianza kujadili habari za itikadi au siasa mara nyingi kuna matata ya maelewano kati ya mhubiri na wasikilizaji katika chaguo ya maneno au msamiati pia muundo wa sentensi
Labda kwa watu wenye Kiswahili kama lugha asilia aliongea mwanzoni kwa namna ya kigeni kidogo . . kama ilikuwa hivyo haikuwa rahisi kufikia mioyo ya wasikilizaji.
Labda ni hii alichomaanisha Bibi Titi.
 
Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,459
2,000
Inawezekana kabisa Kiswahili cha Mwalimu kilikuwa kigumu/cha kitabuni zaidi, wakati wananchi walizoea Kiswahili cha mtaani/nyumbani....
 
misha

Member
Nov 19, 2010
59
0
Asanteni wakuu kwa kuchangia, kama sikosei Hayati Bibi Titi hakujitambulisha kuwa ni 'Mswahili' bali alitumia kabila la baba yake, kwa uhakika DSM ya miaka ya 50 'Waswahili' walikuwa ni wachache sana, hata wataalam wetu wengi wa lugha ya Kiswahili ni wachache sana waliokuwa wanajitambulisha kuwa ni 'Waswahili', Hayati Shaaban bin Robert ni miongoni mwa watu wachache sana waliojua kabila za wazazi wao na kujitambulisha kuwa ni 'Waswahili'. Sikatai kuwa kuna uwezekano(mdogo) Kiswahili cha Mwalimu kilikuwa cha kitabuni/kigumu zaidi ndiyo maana niikawa na hamu ya kusikia hotuba zake za wakati wa TAA, Mwalimu alikuwa mtu wa walalahoi tokea akiwa mwanachuo/mdogo, nadhani alipofika DSM alijitahidi kuwafahamu na kufahamu lugha yao--hii ni-speculation yangu. Tatizo kubwa la Kiswahili kuna maneno mengi ya kigeni hasa ya Kiarabu na kwa maoni yangu mtu anayefahamu kiswahili pekee yake kama kilivyo, sidhani kama anaweza kuifanyia lugha 'justice', na hapa mimi naona kuna haja yetu wakereketwa wa kujua lugha na historia yetu kujikita zaidi na kujiuliza zaidi.
 
Monstgala

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
1,081
2,000
Wataalamu wetu wanatwambia lugha kubwa Tanzania so far ni kisukuma ikifuatiwa na kiswahili.... mpo?
 
Monstgala

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
1,081
2,000
Hata ukikopa kumi moja haiwezekani.

Lakini hebu fikiria kidogo, Tanzania kuna zaidi ya makabila 120 na zaidi ya 80% ya watanzania wote wanaishi vijijini hivyo kiswahili ni lugha ya pili ya watanzania wengi, population ya wasukuma ndio kubwa tanzania hivyo kwa uwingi wao na kisukuma kama lugha yao ya kwanza huoni kama hiyo inaifanya kuwa ndio lugha kubwa inayoongewa tz? maana hata watanzania walio mijini(20%) wengi hawakijui kiswahili kwa ufasaha zaidi ya lugha za kabila zao.... au unaonaje mkuu?
 
misha

Member
Nov 19, 2010
59
0
Hata ukikopa kumi moja haiwezekani.

Ndugu Pmwasyoke nimesoma kwenye moja ya 'post' yako kuwa wewe ni Msafa, binafsi siifahamu lugha ya Kisafa, sote tunajua kuwa neno 'lugha' asili yake ni Kiarabu na siyo la Kibantu, hivi katika Kisafa neno 'lugha' mnaliitaje
 
misha

Member
Nov 19, 2010
59
0
Wataalamu wetu wanatwambia lugha kubwa Tanzania so far ni kisukuma ikifuatiwa na kiswahili.... mpo?

Mkuu, hivi neno kabila bado ni neno linalotumiwa na wataalam, kwa sababu kuna maneno ya Kiswahili yamebadilika, Ila kama neno 'kabila' bado linatumika, kabila la Wasukuma ni kubwa kuliko kabila la Waswahili. Kuhusu lugha - hapo sina uhakika, tunarudi kwenye utata wa kauri ya Hayati Bibi Titi . Washairi hujumlisha 'nyimbo' za asili kuwa ni mashairi ya Kiswahili wakati mitaani tunatofautisha kati ya tungo za nyimbo na shairi, kwa kuwa Kiswahili ni lugha inayokua, wataalam wetu wanaweza kuwa bado hawajarekebisha kamusi na kulifafanua neno lugha kisawasawa. Nifahamvyo lugha ya Kiswahili ni lugha ya Taifa -Tanzania na ni kubwa kama lugha , sijui mwenzangu unaonaje?
 
pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
4,122
2,000
Ndugu Pmwasyoke nimesoma kwenye moja ya 'post' yako kuwa wewe ni Msafa, binafsi siifahamu lugha ya Kisafa, sote tunajua kuwa neno 'lugha' asili yake ni Kiarabu na siyo la Kibantu, hivi katika Kisafa neno 'lugha' mnaliitaje

Mimi na Msafwa sio Msafa. Lugha ni Injango.
 
pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
4,122
2,000
Lakini hebu fikiria kidogo, Tanzania kuna zaidi ya makabila 120 na zaidi ya 80% ya watanzania wote wanaishi vijijini hivyo kiswahili ni lugha ya pili ya watanzania wengi, population ya wasukuma ndio kubwa tanzania hivyo kwa uwingi wao na kisukuma kama lugha yao ya kwanza huoni kama hiyo inaifanya kuwa ndio lugha kubwa inayoongewa tz? maana hata watanzania walio mijini(20%) wengi hawakijui kiswahili kwa ufasaha zaidi ya lugha za kabila zao.... au unaonaje mkuu?

Kiswahili ndiyo lugha iliyosambaa na kueleweka zaidi Tanzania. Hata ikisemekana kuwa lugha ya pili - bado inabaki kuwa inaeleweka zaidi. Mimi ni msafwa lakini lazima nikiri nawasiliana vizuri zaidi kwa kiswahili - na hii ni kweli kwa wengi wetu.
 
misha

Member
Nov 19, 2010
59
0
Asante kwa kunifahamisha, nakushukuru pia kwa kunipatia fasri ya neno 'lugha' , ingawaje umesema kuwa unawasiliana vizuri zaidi kwa kwa Kiswahili kuliko Kisafwa, naomba kuuliza kama neno 'Injango' lina maana nyingine zaidi na kunisaidia katika kutatua swali langu( kuhusu kauri ya Bibi Titi). Nimefurahi sana kusikia 'injango' maana (nifahamuvyo mimi) kwetu sisi(neno lugha) halina fasri moja , mimi siwezi kusema kuwa ni fundi wa lugha ya kabila langu!
 
Kwa nini huwezi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom