Kiswahili cha "SOFT COPY" na "Hard Copy"

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
Mtanisamehe kama ilishwahi kuulizwa lakini naomba mnisaidie kwani nami nimeulizwa na kukwama
 
nami nilimsaidia hivi lakini nikamtahadaharisha kwamba ni direct tranlsation, kama tutapata wajuvi wenye kuelewa kiundani

Kaka,

Nachukua fursa hii kukutahadharisha kuwa neno wajuvi halina maana sawa na neno wajuzi

Wajuvi kwa Kiswahili sanifu lina maana mbaya kama ifuatavyo:

1. Watu wanaojifanya kujua kila kitu [neno muhimu ni "wanaojifanya. Kwa lugha nyengine "much know"]

2. Watu wajeuri, wajuba,
 
huenda bado ina muktadha hapo
 
Tusaidie na jibu ka swali la hapo juu
Kaka,

Nachukua fursa hii kukutahadharisha kuwa neno wajuvi halina maana sawa na neno wajuzi

Wajuvi kwa Kiswahili sanifu lina maana mbaya kama ifuatavyo:

1. Watu wanaojifanya kujua kila kitu [neno muhimu ni "wanaojifanya. Kwa lugha nyengine "much know"]

2. Watu wajeuri, wajuba,
 
nami nilimsaidia hivi lakini nikamtahadaharisha kwamba ni direct tranlsation, kama tutapata wajuvi wenye kuelewa kiundani

Mkuu tatizo la lugha yetu bado haina misamiati mingi ya kiteknolojia, wakati mwingine ni kazi sana kupata tafsri ya maneno kwa kiswahili
 
ni nakala tepe na nakala ngumu , ni uhakika hapo hiyo istilah ya nakala laini iljkuwa inatumika zamani sana haikuwa imethibitishwa na bakita
 
Mkuu tatizo la lugha yetu bado haina misamiati mingi ya kiteknolojia, wakati mwingine ni kazi sana kupata tafsri ya maneno kwa kiswahili
Astaghfillulah! Sikuwa na dhamira ya dhati kuchangia lolote lakini BHULULU ametibua akili yangu. Anasema eti 'tatizo la lugha yetu bado haina misamiati ya kiteknolojia'!!!! Ukweli ni kwamba ni yeye ambaye hana ukwasi wa haja katika msamiati wa Kiswahili. Badala ya kujibidiisha kujielimisha ili apate misamiati ya kutosha, yeye anaishia kulalama ili hatimaye ahalalishe utumwa wa kiutamaduni uliolitafuna taifa hili miaka yote 51 ya uhuru wa bendera. Namshauri asome nyuzi za wachangiaji na atamaizi kwamba 'hard copy' hufasiriwa kama nakala ngumu na 'soft copy' hufasiriwa kama nakala tepe. hataki aache!
 
Mkuu kiswahili bado sana katika misamiati ya kiteknolojia. kwa kifupi bado changamoto ni kubwa sana
 
BHULULU wewe ndiyo bado sana wala siyo lugha ya Kiswahili. Hivi umeangalia vizuri maneno ya Kiingereza kwenye uzi uliouleta ukiponda Kiswahili? Kwa hiyo Kiswahili huwezi, Kiingereza hujui na hata lugha yako mama pia nahisi ni tatizo kubwa!
 
Nakala ya ki-elektroniki na nakala ya kawaida. (sina hakika sana lakini nilishawahi sikia mahali)
 
uwazi na mipasho na weledi

Back
Top Bottom