KISUTU: Yaliyojiri kesi ya Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio. Shahidi wa Jamhuri aweweseka

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Kesi namba 208 ya 2016 imekwama kuendelea leo katika Mahakama ya Kisutu baada ya Wakili kuhoji shahidi asihojiwe mambo ya Zanzibar.

Shahidi wa kwanza upande wa serikali alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Salumu Hamduni.

Wakili wa serikali Paul Kadushi aliiomba mahakama izuie lakini Lissu akijitetea alisema suala hilo lazima lijadiliwe sababu serikali yenyewe ndio imeliweka kwenye hati ya mashtaka.

MAHOJIANO NA SHAHIDI WA KWANZA WA SERIKALI, KESI YA GAZETI LA MAWIO.

Wakili wa Serikali: Paul Kadushi

Shahidi: Salum Rashid Hamduni

WAKILI: Iambie mahakama ulibaini nini kwenye kazi yako, Januari 14, 2016 asb

SHAHIDI: Nilibaini Mikusanyiko isiyo rasmi sehemu za kuuzia magazeti, wananchi wakijadili habari iliyochapishwa na Mawio.

WAKILI: Baada ya Hapo ulichukua hatua gani

SHAHIDI: Nilimjulisha Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalumu ya Dar (ZCO), na makao makuu ya polisi, ambapo nilitaafiriwa kuwa hali ilikuwa vile vile upande wa Zanzibar

WAKILI; Baada ya hapo ulichukua hatua gani?

SHAHIDI: Niliamua kwenda kununua gazeti la Mawio, nisome kuona kama kuna taarifa zozote zilizochapishwa, nikagundua kuna taarifa za uchochezi na kutia hofu, nikaamua kufungua jalada la uchunguzi.

WAKILI: Kwanini ulifikia Uamuzi huo?

SHAHIDI: Nilifikia uamuzi huo baada ya kusoma headline ya ”machafuko yaja Zanznibar”, nilijiridhisha kuwa baadhi ya maneno katika habari hyo yanaweza kuleta hofu na chuki dhidi ya serikali ya Zanzibar

WAKILI: Taarifa kuhusu tukio hilo uliletewa na nani?

SHAHIDI: Nililetewa na wakuu wa upepelezi wa mikoa ya Ilala, Temeke na Kinondoni, yaani SSP Mchomvu-Temeke, SP Ndalama wa Kinondoni na Jumanne Mliro wa Ilala. Walisema kuna mikusanyiko maeneo yao kwenye vijiwe vya magazeti kulingana na habari iliyochapwa na Mawio.

*** WAKILI WA SERIKALI ALIFUNGA MASWALI*****

Kwa upande wa Wakili Peter Kibatala alimuuliza huyo shahidi anafahamu hilo gazeti la mawio linasambazwa Zanzibar na Tanzania Bara kwa kiwango gani katika shughuli zake za kiuchunguzi?

Shahidi huyo wa upande wa mashtaka alimueleza kuwa hana takwimu sahihi.

KIBATALA; Gazeti la Mawio unajua linachapishwa na nani

Shahidi; sifahamu isipokuwa nakumbuka muandishi alikuwa ni Jabir Idrissa

KIBATALA; Ni sehemu gani ambayo ulisoma na kuona kuna taarifa za uchochezi

Shahidi; Ni heading yenyewe ndio ilikuwa inazungumzia uchochezi kwamba Machafuko yaja Zanzibar

KIBATALA; Je, habari hiyo ina uhusiano gani na washtakiwa wa nne

Shahidi; Habari hiyo kwa sehemu kubwa inaonyesha mwandishi alivyomuhoji kwa kina Lissu

KIBATALA: Unafahamu aliyekuwa DCI , Diwani Athumani alitenguliwa na mheshimiwa rais baada ya kumuhusisha na Meno ya Tembo.

Shahidi sifahamu

LISSU AJITETEA MWENYEWE

Kisha mshitakiwa namba 4, Tundu Lissu alijitetea Mwenyewe na mahojiano yalikuwa hivi;

LISSU: Shahidi ieleze mahakama elimu yako

SHAHIDI: Nilisoma Uchama Sekondari, nikasoma A Level Kigurunyembe, na IDM Mzumbe

LISSU: Ulijiunga lini na Jeshi la Polisi

SHAHIDI tangu mwaka 1999.

LISSU ulisema wewe ndio ulifungua jalada la uchunguzi, baada ya wakuu wa upepelezi wa mikoa tajwa kukuletea taarifa, je uliwaandika maelezo yao kama mashahidi wa kesi hii?

SHAHIDI; Hapana

LISSU; Mikusanyiko isiyo rasmi, ni halali au sio halali

SHAHIDI: Ni halali

LISSU: Mihemuko na Hofu inazuiliwa kisheria?

SHAHIDI: Hapana

LISSU: Hofu kama ya Mungu, au ya shetani au ya Dikteta, inazuiliwa kisheria?

SHAHIDI: Ndio inazuiliwa,

LISSU: Sheria gani?

SHAHIDI: SIJUI.

LISSU; Mweleze hakimu, sisi tulikaa wapi kula njama ya kuchapisha gazeti hili

SHAHIDI: sijui

LISSU; Mweleze hakimu tuliwasiliana kwa njia gani ili kukaa pamoja kula njama kama tunavyoshtakiwa

SHAHIDI: Sijui

LISSU, unafahamu ni saa ngapi tulikula njama?

SHAHIDI: Sijui

LISSU; kabla ya kushtakiwa hapa je mimi nilifahamiana na washtakiwa hawa wengine?

SHAHIDI; Sijui

LISSU; Kama hujui muda gani, mahali gani, hujui kama tulifahamiana ulijuaje kama tulikula njama?

SHAHIDI; sijui

LISSU; kwa ufahamu wako, mimi ni mwandishi , au mhariri wa Mawio?

SHAHIDI; Hapana, wewe sio Mwandishi au Mhariri

LISSU; Je unafahamu labda najishughulisha na kazi zozote za uchapishaji wa magazeti?

SHAHIDI; SIJUI.

LISSU: Mweleze hakimu, mimi nawezaje kushtakiwa wakati mimi sio mwandishi, sio mhariri, wala sio mchapishaji au mmiliki wa gazeti?

SHAHIDI; siwezi

LISSU; Mamlaka halali ya serikali ya Mapinduzi ya wananchi wa Zanznibar inachaguliwa kwenye uchaguzi kwa mujibu wa katiba na sharia za uchaguzi wa Zanzibar kweli au si kweli?

SHAHIDI; kweli

LISSU;25 Oktoba 2015 kulikuwa na uchaguzi halali wa Zanzibar kweli au si kweli

SHAHIDI ; Kweli

LISSU, Kwa ufahamu wako uchaguzi huo wa Oktoba 25, 2015 ulifanyika kisheria na ulifutwa kinyume cha sharia na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha ni kweli au si kweli?

SHAHIDI; Kweli

LISSU; Mweleze hakimu kama unaijua katiba ya Zanzibar na sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar

PAUL KADUSHI WAKILI WA SERIKALI AWEKA PINGAMIZI

Kadushi: Napinga swali , tafsiri ya Katiba na serikali halali ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria, wanataka shahidi atafsiri katiba ya Zanzibar huyu sio mtaalamu wa masuala ya katiba, shahidi sio mwanasheria wala mahakama inayotafsiri sheria.

LISSU; Pingamizi halina mashiko, suala la kwamba serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni halali au si halali , na masuala ya Jecha kufuata uchaguzi wameyaleta wenyewe mahakamani ndio maana inabidi yajadiliwe, shitaka lenyewe linasema tulikula njama ya kuleta chuki dhidi ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kifungu cga 157, kinaweka wazi kuwa shahidi anaweza kuulizwa shwali lolote na kwa kuwa wameyaleta wenyewe, wakubali suala la Zanzibar lijadiliwe, naomba mahakama iruhusu.

KIBATALA ANASIMAMA KUONGEZA;

Kwanini wakili wa serikali anamkinga shahidi asijibu Maswali? Imekuja hoja ya wakili huyu kuwa suala la Zanzibar ni suala la Kikatiba, na uchaguzi wake, ikumbukwe kuwa tulipoweka PO, (pingamizi la awali) kuhusu mahakama ya Kisutu kuwa na uwezo wa kusikiliza kesi zinazohusu serikali ya mapinduzi ya Zanzibar iliaamuliwa kuwa inaweza, ndio maana hoja za kesi zimekuja zikitaja masuala ya Zanziba

Hakimu Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho saa 3 na nusu.
 
Kesi namba 208 ya 2016 imekwama kuendelea leo katika Mahakama ya Kisutu baada ya Wakili kuhoji shahidi asihojiwe mambo ya Zanzibar.

Shahidi wa kwanza upande wa serikali alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Salumu Hamduni.

Wakili wa serikali Paul Kadushi aliiomba mahakama izuie lakini Lissu akijitetea alisema suala hilo lazima lijadiliwe sababu serikali yenyewe ndio imeliweka kwenye hati ya mashtaka.

Hakimu Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho saa 3 na nusu.
hahahahha, unajua kuna wakati hata kama hutaki utajikuta unaicheka serikali yako, kesi wamefungua wao, mashaidi wamelata wao, alafu wanazuia asihojiwe???
 
Nilisema hata hii kesi ya mwisho serikali itapata shida kwani nayo ni kuhusu matamshi ya Tundu Lisu ya jinsi Zanzibar inavyopata viongozi wake. Sasa kama huo ni uchochezi tusubiri nondo zitakavyo anguka mahakamani. Jiulize Maalim alitoswa wapi, Bilai yalimkuta yapi, Shein alitoka wapi, Mzee Jumbe aliangukia wapi? Uchaguzi wa Oktober 2015 bila JK na JPM jeuri ya Cheja ingetoka wapi? Mimi nasubiri somo toka kwenye kesi hii.

Hivi by the way wale wa Uamsho wameishia wapi-kuna kesi au ndio bado wako mahabusu toka walipo shikwa au nimepitwa na wakati?
 
Namshauri mh rais aachane n Lissu watu kama akina lisu wana akili sana na wanapatikana dunia nzima, watu kama hawa wakinihusisha na uhalifu huwa ni hatari sana kwani wana upeo mkubwa wa mambo, kwa lissu amejikita kwenye mammbo ya maana na yenye tija ya kutetea haki.

Serikali ispoangalia itaishia kupambana na watu ishindwe kutekeleza mipango yake
 
Kesi namba 208 ya 2016 imekwama kuendelea leo katika Mahakama ya Kisutu baada ya Wakili kuhoji shahidi asihojiwe mambo ya Zanzibar.

Shahidi wa kwanza upande wa serikali alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Salumu Hamduni.

Wakili wa serikali Paul Kadushi aliiomba mahakama izuie lakini Lissu akijitetea alisema suala hilo lazima lijadiliwe sababu serikali yenyewe ndio imeliweka kwenye hati ya mashtaka.

MAHOJIANO NA SHIHIDI WA KWANZA WA SERIKALI, KESI YA GAZETI LA MAWIO.

Wakili wa Serikali: Paul Kadushi

Shahidi: Salum Rashid Hamduni

WAKILI: Iambie mahakama ulibaini nini kwenye kazi yako, Januari 14, 2016 asb

SHAHIDI: Nilibaini Mikusanyiko isiyo rasmi sehemu za kuuzia magazeti, wananchi wakijadili habari iliyochapishwa na Mawio.

WAKILI: Baada ya Hapo ulichukua hatua gani

SHAHIDI: Nilimjulisha Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalumu ya Dar (ZCO), na makao makuu ya polisi, ambapo nilitaafiriwa kuwa hali ilikuwa vile vile upande wa Zanzibar

WAKILI; Baada ya hapo ulichukua hatua gani?

SHAHIDI: Niliamua kwenda kununua gazeti la Mawio, nisome kuona kama kuna taarifa zozote zilizochapishwa, nikagundua kuna taarifa za uchochezi na kutia hofu, nikaamua kufungua jalada la uchunguzi.

WAKILI: Kwanini ulifikia Uamuzi huo?

SHAHIDI: Nilifikia uamuzi huo baada ya kusoma headline ya ”machafuko yaja Zanznibar”, nilijiridhisha kuwa baadhi ya maneno katika habari hyo yanaweza kuleta hofu na chuki dhidi ya serikali ya Zanzibar

WAKILI: Taarifa kuhusu tukio hilo uliletewa na nani?

SHAHIDI: Nililetewa na wakuu wa upepelezi wa mikoa ya Ilala, Temeke na Kinondoni, yaani SSP Mchomvu-Temeke, SP Ndalama wa Kinondoni na Jumanne Mliro wa Ilala. Walisema kuna mikusanyiko maeneo yao kwenye vijiwe vya magazeti kulingana na habari iliyochapwa na Mawio.

*** WAKILI WA SERIKALI ALIFUNGA MASWALI*****

Kwa upande wa Wakili Peter Kibatala alimuuliza huyo shahidi anafahamu hilo gazeti la mawio linasambazwa Zanzibar na Tanzania Bara kwa kiwango gani katika shughuli zake za kiuchunguzi?

Shahidi huyo wa upande wa mashtaka alimueleza kuwa hana takwimu sahihi.

KIBATALA; Gazeti la Mawio unajua linachapishwa na nani

Shahidi; sifahamu isipokuwa nakumbuka muandishi alikuwa ni Jabir Idrissa

KIBATALA; Ni sehemu gani ambayo ulisoma na kuona kuna taarifa za uchochezi

Shahidi; Ni heading yenyewe ndio ilikuwa inazungumzia uchochezi kwamba Machafuko yaja Zanzibar

KIBATALA; Je habari hiyo ina uhusiano gani na washtakiwa wa nne

Shahidi; Habari hiyo kwa sehemu kubwa inaonyesha mwandishi alivyomuhoji kwa kina Lissu

KIBATALA: unafahamu aliyekuwa DCI , Diwani Athumani alitenguliwa na mheshimiwa rais baada ya kumuhusisha na Meno ya Tembo.

Shahidi sifahamu

LISSU AJITETEA MWENYEWE

Kisha mshitakiwa namba 4, Tundu Lissu alijitetea Mwenyewe na mahojiano yalikuwa hivi;

LISSU: Shahidi ieleze mahakama elimu yako

SHAHIDI: Nilisoma Uchama Sekondari, nikasoma A Level Kigurunyembe, na IDM Mzumbe

LISSU: Ulijiunga lini na Jeshi la Polisi

SHAHIDI tangu mwaka 1999.

LISSU ulisema wewe ndio ulifungua jalada la uchunguzi, baada ya wakuu wa upepelezi wa mikoa tajwa kukuletea taarifa, je uliwaandika maelezo yao kama mashahidi wa kesi hii?

SHAHIDI; Hapana

LISSU; Mikusanyiko isiyo rasmi, ni halali au sio halali

SHAHIDI: Ni halali

LISSU: Mihemuko na Hofu inazuiliwa kisheria?

SHAHIDI: Hapana

LISSU: Hofu kama ya Mungu, au ya shetani au ya Dikteta, inazuiliwa kisheria?

SHAHIDI: Ndio inazuiliwa,

LISSU: Sheria gani?

SHAHIDI: SIJUI.

LISSU; Mweleze hakimu, sisi tulikaa wapi kula njama ya kuchapisha gazeti hili

SHAHIDI: sijui

LISSU; Mweleze hakimu tuliwasiliana kwa njia gani ili kukaa pamoja kula njama kama tunavyoshtakiwa

SHAHIDI: Sijui

LISSU, unafahamu ni saa ngapi tulikula njama?

SHAHIDI: Sijui

LISSU; kabla ya kushtakiwa hapa je mimi nilifahamiana na washtakiwa hawa wengine?

SHAHIDI; Sijui

LISSU; Kama hujui muda gani, mahali gani, hujui kama tulifahamiana ulijuaje kama tulikula njama?

SHAHIDI; sijui

LISSU; kwa ufahamu wako, mimi ni mwandishi , au mhariri wa Mawio?

SHAHIDI; Hapana, wewe sio Mwandishi au Mhariri

LISSU; Je unafahamu labda najishughulisha na kazi zozote za uchapishaji wa magazeti?

SHAHIDI; SIJUI.

LISSU:Mweleze hakimu, mimi nawezaje kushtakiwa wakati mimi sio mwandishi, sio mhariri, wala sio mchapishaji au mmiliki wa gazeti?

SHAHIDI; siwezi

LISSU; Mamlaka halali ya serikali ya Mapinduzi ya wananchi wa Zanznibar inachaguliwa kwenye uchaguzi kwa mujibu wa katiba na sharia za uchaguzi wa Zanzibar kweli au si kweli?

SHAHIDI; kweli

LISSU;25 Oktoba 2015 kulikuwa na uchaguzi halali wa Zanzibar kweli au si kweli

SHAHIDI ; Kweli

LISSU, Kwa ufahamu wako uchaguzi huo wa Oktoba 25, 2015 ulifanyika kisheria na ulifutwa kinyume cha sharia na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha ni kweli au si kweli?

SHAHIDI; Kweli

LISSU; Mweleze hakimu kama unaijua katiba ya Zanzibar na sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar

PAUL KADUSHI WAKILI WA SERIKALI AWEKA PINGAMIZI

Kadushi: Napinga swali , tafsiri ya Katiba na serikali halali ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria, wanataka shahidi atafsiri katiba ya Zanzibar huyu sio mtaalamu wa masuala ya katiba, shahidi sio mwanasheria wala mahakama inayotafsiri sheria.

LISSU; Pingamizi halina mashiko, suala la kwamba serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni halali au si halali , na masuala ya Jecha kufuata uchaguzi wameyaleta wenyewe mahakamani ndio maana inabidi yajadiliwe, shitaka lenyewe linasema tulikula njama ya kuleta chuki dhidi ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kifungu cga 157, kinaweka wazi kuwa shahidi anaweza kuulizwa shwali lolote na kwa kuwa wameyaleta wenyewe, wakubali suala la Zanzibar lijadiliwe, naomba mahakama iruhusu.

KIBATALA ANASIMAMA KUONGEZA;

Kwanini wakili wa serikali anamkinga shahidi asijibu Maswali? Imekuja hoja ya wakili huyu kuwa suala la Zanzibar ni suala la Kikatiba, na uchaguzi wake, ikumbukwe kuwa tulipoweka PO, (pingamizi la awali) kuhusu mahakama ya Kisutu kuwa na uwezo wa kusikiliza kesi zinazohusu serikali ya mapinduzi ya Zanzibar iliaamuliwa kuwa inaweza, ndio maana hoja za kesi zimekuja zikitaja masuala ya Zanziba

Hakimu Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho saa 3 na nusu.
Huyo polisi hana kazi kama kila kitu ni sijui na hapana
 
Asante sana afande kwa kukiri mbele ya mahakama. Huu ni mwanzo

LISSU;25 Oktoba 2015 kulikuwa na uchaguzi halali wa Zanzibar kweli au si kweli

SHAHIDI ; Kweli

LISSU, Kwa ufahamu wako uchaguzi huo wa Oktoba 25, 2015 ulifanyika kisheria na ulifutwa kinyume cha sharia na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha ni kweli au si kweli?

SHAHIDI; Kweli
 
Nimecheka sana nusu nijambe mbele ya wajukuu!!Nyie vijana mtatuuwa mbavu wazee wenu.Huyu Lissu ni hatari sana!!Kwani hivi kuzaa watoto aina ya Lissu vijana wa siku hizi hamuwezi kufaytua?Huyo Kibatala naye ni hatari sana!!

Huyo jamaa shahidi kaulizwa juu ya hofu ya Mungu,Shetani na dikteta akashindwa kutoa majibu!Kesho nitafika Kisutu,ili nisikilize muendelezo!!
 
Vyombo vya dola jamani kuweni makini na utendaji wenu wa kazi maana siku hizi sio kama zamani kwamba watu ni mbumbumbu,
ona sasa mnavyoahibishwa adharani!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom