Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,797
- 11,959
WATANZANIA 100 wamepewa adhabu ya kutofanya kosa ndani ya miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kutenda kosa la kutoka ndani ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwenda Afrika Kusini bila kufata utaratibu wa uhamiaji.
Raia hao ni Laurence Omary, Sultani Ditutu, Nassoro Lingumbulu, Abdul Masoud, Waziri Waziri, Dotto Abdallah na wenzao 94 ambao walipewa adhabu hiyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.
Katika kesi hiyo, wakili wa serikali Godfrey Ngwijo, akisaidiana na Sitta Shija, wamedai kuwa, washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Julai 3 mwaka 2020 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Ilidaliwa kwamba, wakiwa raia wa Tanzania walibainika kutoka nje ya Tanzania katika tarehe zisizofahamika bila kufata utaratibu wa kiuhamiaji na kuelekea Afrika Kusini.