Kisutu: Tundu Lissu ashindwa kutokea Mahakamani, kesi zake zaahirishwa hadi 26/08/2020

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Salaam Wakuu,

0911HRS: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu hajatokea Mahakamani kama ilivyotarajiwa kwenye kesi inayomkabili namba 123 ya 2017 mbele ya Hakimu Mheshimiwa Enock Matembele.

Wakili wa Utetezi Peter Kibatala, ameiambia Mahakama kwamba Tundu Lissu alikuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu, amerudi majuzi (Jumatatu). Kutokana na hali yake, ilishauriwa apate mapumziko (isolation/karantini) aweze kuangalia afya yake, hivyo tunaomba tarehe nyingine, tunaamini siku hiyo atakuwepo.

Mawakili Upande wa Jamhuri, Wakili Mkuu Renatus Mkude na mwenzake Wakili Wankyo Simon (Wakili Mwandamizi) hawakuwa na pingamizi, hivyo kesi imeahirishwa hadi tarehe 26 August 2020.

Hii kesi ina Makosa matano

KOSA LA KWANZA

Kwenye kesi namba 123 ya Mwaka 2017, inadaiwa tarehe 11January 2017 Tundu Lissu akiwa huko Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar katika Kampeni za Uchaguzi huku akiwa ni raia wa Tanzania Bara, aliongea maneno ya kuwaudhi Waislam, alisema;

... "Kwahiyo hicho kunachoitwa Uchaguzi wa marudio uharamia mtupu, haramu, haramu, haramu.. Kinachoitwa Uchaguzi wa marudio ni haramu tupu... Nyie ni Waislam sana naomba niseme uharamu wa Uchaguzi wa Marudio wa Mwaka jana hautofautiani na kula nguruwe, kwa wala nguruwe hawa, wala nguruwe hawa, nlikuwa nazungumzia yaliyokuja baada ya wala nguruwe hawa kufanya uharamia wao.. Laana tullah'

KOSA LA PILI

Tarehe 11 January 2017 Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa Kampeni za Uchaguzi alisema;

"Tangu 1964 Tanganyika ndiyo inaamua nani atawale Zanzibar".

KOSA LA TATU

Tarehe 11 January 2017 Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa Kampeni za Uchaguzi alisema;

"Tangu mwaka 1964 Zanzibar inakaliwa kijeshi na Tanganyika, nani anayebisha... Tangu mwaka 1995 ikifika Uchaguzi askari wa Tanganyika wanahamia Zanzibar ili kuja kihakikisha Vibaraka wao wa Zanzibar hawaondolewi Madarakani na Wananchi wa Zanzibar mnapigwa, mnateswa, mnauawa kwa sababu ya Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar...., Marehemu Karume alipoanza kushitukia mwaka 71, 72 akauawa...., itakapofika tarehe 15 mwezi wa kwanza muadhimishe mika 53 ya kukaliwa Kijeshi na Tanganyika"

KOSA LA NNE

Tarehe 11 January 2017 Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa Kampeni za Uchaguzi alisema;

"Jumbe aliondolewa Dodoma, Ally Hassan Mwinyi alipewa Urais Dodoma, na aliyempa ni Nyerere sio Wazanzibar.., Marais wa Zanzibar wote ni made in Tanganyika..
.., wametengenezwa Tanganyika, wanakaa madarakani kwa sababu ya Tanganyika...,

KOSA LA TANO

Tarehe 11 January 2017 Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa Kampeni za Uchaguzi alisema;

"Zanzibar inatawaliwa na Tanganyika kwa kivuli cha Tanzania, Tanzania ni Tanganyika..., Tanzania ni kivuli cha kuikalia Zanzibar, cha kuigeuza Zanzibar Koloni na Makoloni huwa yananyonywa, Makoloni yanatawaliwa, Kisiasa yananyonywa Kiuchumi na yanakandamizwa Kijeshi..., metawaliwa kisiasa na Tanganyika miaka yote hii.. Ali Mohammad Shein hatufai tena ataondolewa kama Aboid Jumbe alivyoondolewa.... ".

NOTE: Leo hapa Kisutu watu hawaruhusiwi kuingia isipokuwa wenye kesi na Mashahidi tu. Ulinzi ni Mkali wa Polisi kila sehemu hapa Kisutu. Hawataki mtu asogee.

=====

0925HRS: Sasa tunaingia Kesi ya Pili ya Lissu Open Court #2.

Hii Kesi ya Pili tupo kwa Hakimu Mbando.

Kesi inayo mkabili Tundu Lissu namba 236 ya mwaka 2017 ya Uchochezi imeahirishwa hadi 26 August 2020. Sababu za kutokufika zinafanana na kesi ya Kwanza.

Kwa leo kesi zake zote zimeahirishwa.

Katika kesi namba 236, inadaiwa Tarehe 17 July 2017 Maeneo ya Mtaa Ufipa Kinondoni, Tundu Lissu aliongea Maneno ya kuudhi kwamba "Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni ya Kibaguzi wa Kifamilia, Kikabila, Kikanda na Kidini. Vibali vya kazi Work permit vinatolewa kwa wamishenari wa Kikatoliki tu huku Madhehebu mengine yakielezwa kupanga foleni Uhamiaji. Viongozi Wakuu wa Serikali wanachaguliwa kutoka kwenye Familia, Kabila na Ukanda... Acheni woga pazeni sauti.. Kila mmoja wetu.. Tukawaambie kama tulivyo waambia Serikali ya Makaburu, hii Serikali Isusiwe na Jumuiya ya Kimataifa, isusiwe Kisiasa, Kiuchumi na Kidiplomasia kwa sababu ya Utawala huu wa Kibaguzi.. yeye ni Dikteta Uchwara".

Mwisho.
 
Zile mbwenbwe za kutishia kutoa hati za kumkamata leo hawakutoa tena jamaniiii khaaaaaa!! Wameanza kunywea baada ya simba kufika mbona walikuwa wanatishia kumkamata sasa mbona hakamatiki tena,hizo tarehe walizotaja tutakuwa kwenye kampeni natumai hatoenda huko tena!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom