KISUTU: Singh Sethi na Rugemalira wanyimwa dhamana, wapelekwa Keko

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Watuhumiwa wa Kesi ya Uhujumu Uchumi, Ndg. Harbinder Sethi na James Rugemalira wamenyimwa dhaman na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu na kupelekwa katika Gereza la Mahabusu Keko.

Walifikishwa Mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya muda mrefu sana kuhusu kesi za Escrow zimeishia wapi, na Kesi ya IPTL imeishia wapi.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU inasema huu ni muendelezo wa majuku yao na walichunguza shauri hili kwa muda mrefu, Sasa imefika muda muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa wakuu hawa wa mashauri hayo ya uhujumu uchumi wa nchi yetu Mahakamani.

Habari zaidi soma=>News Alert: - TAKUKURU yawafikisha mahakamani Harbinder Sethi na James Rugemalira kwa kosa la Uhujumu uchumi
 
Kupitia kwenu atawashuri na atahakikisha anapata siri zote(taarifa zote muhimu na nyeti) zitakazoweza kuwa--implicate vigogo wote waliohusika maana huyo ni mpinzani na atahakiisha hamfi peke yenu na pia atahakikisha hii kesi inawavua nguo watu wakiwemo wanasiasa untouchable kama walihusika.

Najua teyari mna mawakili lakini na huyo niliemtaja muongezeni.

Lissu kama mwanasiasa wa upinzani hii kesi haimfai.
 
Back
Top Bottom