Kisutu: Shamim Mwasha na Mume wake, Abdul Nsebo(Abdukandida) wapandishwa Kizimbani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Mmiliki wa Blog ya 8020 Fashion, Shamim Mwasha na Mume wake, Abdul Nsebo maarufu Abdukandida wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin.
IMG_20190513_161852_821.jpg
IMG_20190513_161847_150.jpg

Picha kapiga Mohammed Ibrahim wa Michuzi TV

======


TUHUMA ZA KUKUTWA NA GRAMU 232.70 ZA HEROINE ZAWAFIKISHA KORTNI SHAMIM NA MUMEWE

Na Karama Kenyunko

MMILIKI wa Blog ya 8020 Fashion, Shamim Omary Mwasha (41) na mume wake, Abdul Nsembo(45) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa wakikabiliwa na tuhuma za kusafrisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 232.70.

Akisoma hati ya mashtaka leo Mei 13, 2019 Wakili wa Serikali, Costastine Kakula amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi, Steven Mhina kuwa washtakiwa wametenda kosa hilo Mei 1,2019 wakiwa huko Mbezi beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa siku ya tukio washtakiwa hao walikutwa na gramu 232.70. za Dawa za kulevya kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi mpaka Mahakama Kuu ama kwa kupata Kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula ameuomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka ili hatua nyingine iweze kuendelea licha ya kwamba Leo ndiyo siku ya kwanza kwa kesi hiyo kusomwa Mahakama hapo.

Kesi imeahirishwa hadi Mei 27, 2019 kwa kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.

Zaidi, soma:

 
Society yetu ina tabia ya kusifu kila mtu mwenye utajiri mkubwa bila kujari chanzo cha utajiri huo ni nini.
At least we have something to learn from Reginald Mengi...wengine wengi ni utata mtupu. Ndio maana dawa za kulevya haziishi. Ndio maana mauaji ya kishirikina nayo hayaishi.
Tuache kupamba watu wenye hela chafu kama ndio role models wetu
 
Kwanini wasiwe wanamaliza upelelezi wao kwanza ndo wawapeleke watu huko mahakamani
 
Back
Top Bottom