Kisutu: Mzigo wa Madini wenye thamani ya Bil 61 Wataifishwa, ni ule Uliokamatwa Uwanja Ndege wa Dar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,931
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetaifisha mzigo wa madini ya almasi ambao ulikutwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, ukiwa unasafirishwa kwenda nchini Ubelgiji, wenye thamani ya sh. bilioni 61, 970,625,864.

Almasi hizo zina uzito wa carats wa 71,654.45 ambazo zilikuwa zinasafirishwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania(TANSORT), Archard Kakugendo na Mthamini almas wa Serikali Edward Rweyemamu.

Pia mahakama hiyo, imewahukumu wathaminishaji hao ambao ni Kalugendo na Rweyemamu , kulipa faini ya sh. milioni moja kila mmoja au kwenda jela miaka mitatu, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuisababishia Serikali hasara sh. bilioni 61.9.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya, baada ya washitakiwa kuandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini( DPP), Desemba 17, mwaka huu ya kuonyesha nia ya kuingia makubaliano ya kukiri kosa lao.

Awali kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, jopo la mawakili watatu wa Serikali Wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Monica Mbogo, walidai shauri lilipelekwa kwa kutajwa na upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kwa Mamlaka ya sheria ya Uhujumu uchumi, DPP ameridhika kuwashitaki washitakiwa katika mahakama hii.

Pia Wakili wa Serikali Jacqueline Nyantore, alidai kesi hii ni Uhujumu Uchumi, hivyo DPP ameipa kibali mahakama hii kesi kusikilizwa.

Akiwasomea shitaka alidai washitakiwa wote wanakabiliwa na shitaka la kuisababishia Serikali hasara ambapo alidai Agosti 25 na 31, mwaka 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa wa Dar es Salaam na Shinyanga, washitakiwa hao kwa pamoja wakiwa wathamini wa Wizara ya Nisahati na madini walisababisha hasara ya dola za 29,509, 821.84, sawa na sh. bilioni 61.9
 
.
swahilitimes-___CI-IxBxFe-a___-.jpg


Serikali ya #Tanzania imetaifisha Madini ya Almasi ya Tsh. Bilioni 61.97 yaliyokuwa yanatoroshwa na waliokuwa watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwenda nchini Ubelgiji kupitia Uwanja wa JNIA


Waliotorosha Almasi hizo zenye uzito wa Kg 14.33 ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito (Tansort), Archard Kalugendo na aliyekuwa Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu Madini hayo yametaifishwa baada ya Mahakama ya Kisutu kutoa hukumu dhidi ya washtakiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Dola 29,509,821.84


Mbali na kutaifisha Madini hayo, Mahakama pia imewapiga faini ya Tsh. Milioni 1 kila mmoja na kama watashindwa kulipa faini watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
 
Kwahiyo jamaa walikuwa wanafanya kazi zao za kuthaminisha huku mengine wanajisogezea.
 
Kilo 15, je wamekaa rumande miaka mingapi kwa anayefahamu? Tanzania ni tajiri bali ni sisi Watanzania ndio wajinga.
 
Ila wazungu wanaiba sana. Hapa inamaaana serikali ya Ubelgiji inajua hii michezo yote. Haijaanza leo. Ni miaka na miaka.

Wamejenga hiyo Antwerp kwa uhuni wa hivi. Kesho wanawaletea msaada wa 10bn mnashangilia sana.
Naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa mambo iliyofanya kwenye sekta ya madini.
 
Watumishi 22 TRA wamesimamishwa kazi lakini hawa hasara ya 61bil wanatozwa faini 1m.

QNET hawawezi kuwarudishia watu hela zao

250gm za heroine jela miaka 20.

DPP jamani kweli hii mizani inabalance?
 
Yaani sahivi utoki mule bila kuweka mpunga mezani kwa Dipipii, tena huyu dipipiii tangu kompyuta zake zipotee kusiko julikana amekua mkali sana.

Wachina wawai kuleta hizo pesa tunusurike aisee
 
Back
Top Bottom