KISUTU: Mbunge John Heche aongezwa katika kesi dhidi ya Vigogo 7 wa CHADEMA, Adai maagizo hayamtishi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche(CHADEMA) afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kistu na kwasasa amewekwa mahabusu ndogo huku akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili

> Kuna tetesi kuwa anaweza kuunganishwa kwenye kesi inayowakabili viongozi wengine 7 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe(Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa)

Mbunge Heche alikamatwa tarehe tatu na kunyimwa dhamana.

Habari zaidi, soma=>Mbunge John Heche aendelea kushikiliwa kituo cha Polisi cha Kati Dar baada ya kwenda kuripoti

UPDATES:

Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, ameingizwa mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

> Heche anakabiliwa na mashtaka matatu la kwanza kufanya mkusanyiko usio halali, kufanya mkusanyiko wenye vurugu na kuchochea chuki kinyume cha sheria.

> Wakili wa Serikali Faraja Nchimbi ameomba kumuongeza katika kesi inayowakabili akina Mbowe hivyo washtakiwa watakuwa wanane

> Masharti ya dhamana ya Heche ni sawa na wenzake.

1. Awe na wadhamini wawili watakao saini bondi ya Tsh. 20 milioni

2. Wadhamini wawe na barua toka kwa wenyekiti wa mtaa au kijiji na kopi za vitambulisho vyao

Washitakiwa wote wanatakiwa wawewanaenda kuripoti Kituo kikuu cha Polisi mara moja kila wiki(Ijumaa)

Mbunge John Heche, ameachiwa kwa dhamana muda huu katika mahakama ya Kisutu.
 
Last edited:
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche(CHADEMA) afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kistu na kwasasa amewekwa mahabusu ndogo huku akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili

> Kuna tetesi kuwa anaweza kuunganishwa kwenye kesi inayowakabili viongozi wengine 7 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe(Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa)

Kwa sasa sintoshangaa kuona viongozi wote wa upinzani wakiwekwa ndani kwa sababu udikteta umefikia kiwango cha north Korea
 
"Tujenge utamaduni wa kudhibiti viongozi wetu wanapo vunja kaitba"
hizi gharama wala tusiogope!
huyu joka kwanza kaanza kuchoka mawe anayopigwa ni mengi japo anajifanya bado kichwa ngumu
 
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche(CHADEMA) afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kistu na kwasasa amewekwa mahabusu ndogo huku akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili

> Kuna tetesi kuwa anaweza kuunganishwa kwenye kesi inayowakabili viongozi wengine 7 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe(Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa)
Siyo tetesi Heche yumo kwenye kesi ya Mbowe ila aliruka dhamana!
 
Wakuu,

Habari kutoka hapa Kisutu ni kuwa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche(CHADEMA) ameunganishwa kwenye kesi ya akina Mbowe na hivyo kufanya watuhumiwa kwenye kesi ile kufika 8. Na kwa pamoja wanafikisha makosa 10.

Heche amesomewa makosa matatu:
1. Kufanya mkusanyiko au maandano yasiyo halali
2. Kufanya mkusanyiko au maandamano yenye vurugu
3. Kosa hili ndilo linaongezeka kule kwa wenzake na kufanya yawe 10 kwa ujumla: 'Kuchochea chuki kinyume na sheria'

Masharti ya dhamana kwa Heche ni sawa na wenzake:

1. Awe na wadhamini wawili watakao saini bondi ya Tsh. 20 milioni
2. Wadhamini wawe na barua toka kwa wenyekiti wa mtaa au kijiji na kopi za vitambulisho vyao

Wakili wa Utetezi ni Jeremiah Mtobesya
Wakili wa Jamhuri ni Faraja Nchimbi
Hakimu muendesha Mashtaka ni Wilbard Mashauri
 
Kabila la wasukuma ni miongoni mwa kabila yenye msimamo saaaana hapa Nchini
Huwa hawabadiliki badiliki hovyo wala hawayumbishwi

Sasa kwa hawa wenzetu wangesoma nyakati kwanza kwa utawala huu wa awamu ya 5.
Baba Jeska hataki mchezo,
Ndio maana hawa jamaa kila wakitikisa kiberiti Baba Jeska anazidi kufanya kweli,
Msimamo upo palepale
 
Chini ya utawala huu tutajua vizuri maana ya mshamba na limbukeni, hata mimi nilikuwa sijui maana ya maneno haya
 
Wakili wa Serikali ana kazi ngumu sana maana lazima atekeleze maelekezo kutoka mbinguni ya Tanzania
 
Kabila la wasukuma ni miongoni mwa kabila yenye msimamo saaaana hapa Nchini
Huwa hawabadiliki badiliki hovyo wala hawayumbishwi

Sasa kwa hawa wenzetu wangesoma nyakati kwanza kwa utawala huu wa awamu ya 5.
Baba Jeska hataki mchezo,
Ndio maana hawa jamaa kila wakitikisa kiberiti Baba Jeska anazidi kufanya kweli,
Msimamo upo palepale
Unasifu vitu gani wewe?!
Elimu tuliyoipata waTz ni mzigo
 
Naahidi - Baada ya ccm kung'olewa na wananchi kitambo kifupi sana kijacho jeshi la polisi litafutwa , wala haitokuwa mara ya kwanza , Mwl Nyerere alipowang'oa wakoloni hakuendelea na polisi wa kikoloni lakini nchi ikasonga
 
Back
Top Bottom