Kisutu: Mahakama yawafutia Mashtaka Harry Kitilya na wenzake, Polisi yawakamata tena

Ila giza likiwa zito sana jua kunakaribia kucha. Pole sana Kitilya na Sioi, Mungu yu nanyi
Unamuomba Mungu afanye nini? Yaani umeshajua usafi wa watu hawa au basi tu unaamini wanaonewa. Mi naomba Mungu awape wanachostahili. Kama walifanya uhuni huo, ngoja makubwa yawapate! Na wakome!
 
Duuh aisee, labda wanataka waanze upya kutafuta ushaihidi,ila nikwanini huwa wanafungua kesi na kutesa watu wakati ushahidi haupo?
Africa hio lengo ni kukukomoa,ili hata kama una biashara zako nje zife ili ukitoka uwe masikini. Wenzetu hawana mambo haya wanaangalia mchango wako ktk kodi ngapi watakosa ukiwa ndani thus wakikuhukumu ni kweli umetenda kosa.Africa waweza singiziwa na ukafia jela. Yote ni mambo yaifanyayo Africa kulaanika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamuomba Mungu afanye nini? Yaani umeshajua usafi wa watu hawa au basi tu unaamini wanaonewa. Mi naomba Mungu awape wanachostahili. Kama walifanya uhuni huo, ngoja makubwa yawapate! Na wakome!


Hakuna hata siku moja mtu anaweza kumwombea mabaya binadamu yoyote all in all God is watching
 
Maagizo toka mamlaka za kichaa jiwe AKA Dukuzi.

Mahakama ya Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya na maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, hata hivyo wamekamatwa tena na kurudishwa mahabusu.

-----------
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya na mwenzake wawili ambao ni maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon.

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo ya kutakatisha fedha.

Wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Uamuzi huo imefikiwa leo Januari 11 na Hakimu Mkazi, Salum Ally baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kueleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole akisaidia na wenzake Pendo Mangole na Patrick Mwida, amedai mahakamani hapo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

"Taarifa hii ya kutokuendelea na shauri hili mbele ya mahakama yako, imeletwa chini kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002," amesema Ngole.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Ally alisema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kuwekwa mahabusu.

Chanzo Mwananchi


Habari zaidi, soma=>Harry Kitilya, Sioi Sumari na Shose Sinare wafikishwa mahakamani - JamiiForums
 
Hapo watapewa lesser charges na watakiri kisha wataambiwa walipe faini na kuachiwa huru.

Hilo ni deal la kuwasaidia watoke. Inakua kama ya ndugu yake Rostam.

dili after two years in cells, brother unaijua jela unaisikia?

refer wimbo wa LWP-Majitu (Wanaokwenda Jela sio wote wenye hatia na wala si wote ni watuhumiwa)

jela balaa
jela jelasi

psychologically jamaa hawapo sawa tena, yani wakitaka kuishi bongo hapa siku zao zitahesabika km Liumba..mark my words
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom