Ukishaona kesi zinafutwa jua Furaha ya mfalme imetimia,pia hakuna kesi nia ilikuwa kuwakomoa team lowasa,kadri uchaguzi unavokaribia wataachiwa wengi.
Wapiga dili hawana aibu kila mahali wao ni fursa,Watalipa faini hao jiwe linataka hela tu hapo
Lazima watu wametemeshwa sana mpung@Ukishaona kesi zinafutwa jua Furaha ya mfalme imetimia,pia hakuna kesi nia ilikuwa kuwakomoa team lowasa,kadri uchaguzi unavokaribia wataachiwa wengi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ya Manji na vita feki vya madawa,ukiwa safi shetani hana nafasi Mungu u upande wakoZuga tu badae utaambiwa kesi waliyofunguliwa upya inadhamana wanakuwa nje kisha game ova mambo yakuoneana tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Unamuomba Mungu afanye nini? Yaani umeshajua usafi wa watu hawa au basi tu unaamini wanaonewa. Mi naomba Mungu awape wanachostahili. Kama walifanya uhuni huo, ngoja makubwa yawapate! Na wakome!Ila giza likiwa zito sana jua kunakaribia kucha. Pole sana Kitilya na Sioi, Mungu yu nanyi
Africa hio lengo ni kukukomoa,ili hata kama una biashara zako nje zife ili ukitoka uwe masikini. Wenzetu hawana mambo haya wanaangalia mchango wako ktk kodi ngapi watakosa ukiwa ndani thus wakikuhukumu ni kweli umetenda kosa.Africa waweza singiziwa na ukafia jela. Yote ni mambo yaifanyayo Africa kulaanikaDuuh aisee, labda wanataka waanze upya kutafuta ushaihidi,ila nikwanini huwa wanafungua kesi na kutesa watu wakati ushahidi haupo?
Kama u MTU wa Mungu MTU wa imani Kwa nchi za kiafrica utampeleka jehanamu,wengi wao huwa ni sawa na loudspeaker ufuata maagizo.Ni nadra kusimamia haki.Aisee, Nitamwambia mwanangu ausomee u-DPP, ni mtu mkubwa mno.
Unamuomba Mungu afanye nini? Yaani umeshajua usafi wa watu hawa au basi tu unaamini wanaonewa. Mi naomba Mungu awape wanachostahili. Kama walifanya uhuni huo, ngoja makubwa yawapate! Na wakome!
Hata mitume walikasirika! Binafsi nilishaachana na maombi kwa watu waovu. Let them get what they deserve!Hakuna hata siku moja mtu anaweza kumwombea mabaya binadamu yoyote all in all God is watching
Mahakama ya Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya na maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, hata hivyo wamekamatwa tena na kurudishwa mahabusu.
-----------
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya na mwenzake wawili ambao ni maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon.
Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo ya kutakatisha fedha.
Wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Uamuzi huo imefikiwa leo Januari 11 na Hakimu Mkazi, Salum Ally baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kueleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.
Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole akisaidia na wenzake Pendo Mangole na Patrick Mwida, amedai mahakamani hapo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.
"Taarifa hii ya kutokuendelea na shauri hili mbele ya mahakama yako, imeletwa chini kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002," amesema Ngole.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Ally alisema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.
Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kuwekwa mahabusu.
Chanzo Mwananchi
Habari zaidi, soma=>Harry Kitilya, Sioi Sumari na Shose Sinare wafikishwa mahakamani - JamiiForums
Hapo watapewa lesser charges na watakiri kisha wataambiwa walipe faini na kuachiwa huru.
Hilo ni deal la kuwasaidia watoke. Inakua kama ya ndugu yake Rostam.
😁😁😁😁 iko nini sasa