Kisutu: Mahakama yatupilia mbali hoja za Meya wa Dar es Salaam kutaka asalie madarakani, yasema hoja za mwombaji hazina miguu ya kusimamia

CCM ni sawa na mtu wanatenga ugali ili mle yeye anakunywa mchuzi wote anachukua finyango anasokomeza mifukoni kisha anaanza kuondoka eneo la tukio kwa mbwembwe.

Na kwa sisi watanzania ni janga kubwa kuruhusu siasa kuingia hadi kwenye mifumo ya Haki..tutapata shida sana mbeleni zaidi ya hizi.
 
Kwa hili ingawa siungi mkono meya kuondolewa kihuni kwa sababu ya kutoolewana na Makonda..Lkn nadhani mahakama imemtendea haki,kwa sababu aliwahi mno kwenda kufungua kesi ya hisia ya kufukuzwa.

Meya hakuwa na sababu ya kufungua kesi ya mahakama kuzuia kikao cha kumuondoa,bora hata angeweka zuio la kikao chenyewe kwamba ni kikao batili ukizingatia yy ndo mwenyekiti wa vikao vyote.

Lakini pia mahakama ipo sahihi sana kusema,haiwezi kuzuia kikao cha kumuondoa kwa sababu hata akiondolewa hapati hasara yoyote!! Hapo ndo nimepapenda kweli..!! Kwani mwita anapata hasara gani akiondolewa kuwa MEYA!.?0

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuambie kulikua na hasara gani kutokumchagua kua meya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haiwezi kuzuia Meya wa DSM,Isaya Mwita kuondolewa kwenye nafasi yake kwa sababu hakuna uthibitisho wa uwepo wa kikao cha kumuondoa madarakani wala hasara atakayoipata endapo akiondolewa.

Yasema mwombaji hajatoa sababu za msingi za kukidhi vigezo vitatu vya kwanini abaki kwenye nafasi hiyo.

Hakimu asema maombi yamekosa ushahidi kuwa kulikuwa na kikao kinachokusudia kumwondoa madarakani.

“Mahakama hii inatupilia mbali hoja za kutaka muombaji (Mwita) kubaki madarakani kwa sababu hoja za Wakili wa muombaji hazina miguu ya kusimamia kwa kushindwa kufata vigezo ikiwemo uwepo wa kikao cha kutaka kumtoa madarakani”- Hakimu Janeth Mtega.

Uamuzi wa Mahakama kusema haiwezi kuzuia Mwita kuondolewa kwenye Umeya unatokana na maombi yake ambayo aliyawasilisha Jan 6, 2020 ya kutaka kuzuia Kikao cha Baraza la Madiwani wasijadili ajenda ya kumng’oa, kesi ya msingi ya mchakato wa kumuondoa kukiuka Utaratibu imepangwa Jan 13.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kikao Cha Jana hakikua na uhalali wa kumuondoa madarakani hivyo jumatatu nitaripoti kazini kama kawaida.

"Nakusudia kuwashtaki wote waliohusika kufoji saini ya Diwani ambaye yupo nje ya nchi na mmoja wa washtakiwa Hawa atakuwa Kigogo mkubwa tu katika Jiji la Dar es Salaam" Isaya Mwita Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Leo asubuhi nimeripoti ofisini japo mkurugenzi ananipa gari sijui shida nini hivyo nimemuandikia Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam aniletee gari kwa haraka mno" Mstahiki Meya wa Jiji Isaya Mwita.

Pia soma
- Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Meya anyang’anywa gari, ofisi yafungwa. Adai kuwa yeye bado ni Meya halali
Hili lilikuwa Wazi Mkuu! Labda kama Ingekuwa kama Kenya na si Tanzania. Hakuna Tofauti kati ya CCM, Police, Majeshi yote kiujumla, Mahakama na Vyombo vyote vya Dola kiujumla.
 
Vipi kuhusu wale wanaohujumu nchi kwa makusudi kwa kushirikiana na adui zetu. Haki yao ni nini??
Nyie mkiambiwa ukweli mnasema hujuma lisu mlitaka kumuua kisa aliwaoutsmart wajinga nyie na Kama kweli aliwahujumu je Sheria inasema wauwawe?
 
Huyo hakimu si ni yule aliesimamia kesi ya kabendera magoti?
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es salaam, Janeth Mtega amesema Mahakama hiyo imeyatupilia mbali maombi ya Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita kwa kuwa Wakili wake hakufuata baadhi ya vigezo katika kufungua madai yake.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kikao Cha Jana akikua na uhalali wa kumuondoa madarakani hivyo jumatatu nitaripoti kazini kama kawaida.

"nakusudia kuwashtaki wote waliohusika kufoji saini ya Diwani ambaye yupo nje ya nchi na mmoja wa washtakiwa Hawa atakuwa Kigogo mkubwa tu katika Jiji la Dar es Salaam" Isaya Mwita Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Leo asubuhi nimeripoti ofisini japo mkurugenzi ananipa gari sijui shida nini hivyo nimemuandikia Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam aniletee gari kwa haraka mno" Mstahiki Meya wa Jiji Isaya Mwita.

Yasema mwombaji hajatoa sababu za msingi za kukidhi vigezo vitatu vya kwanini abaki kwenye nafasi hiyo.

Hakimu asema maombi yamekosa ushahidi kuwa kulikuwa na kikao kinachokusudia kumwondoa madarakani.
=======
Rejea
 
Kila mara Rais wa JMT amekuwa akisisitiza kuwa maendeleo hayana vyama.

Yaani ni ya kwetu wote watanzania uwe Cuf au Chadema. Sasa hili la kutaka mayor wa chama flan tu ndio awe kiongozi linatoka wapi! Na kama alipata ajari na gari alikuwa anaendesha yeye? Dereva kwa nini asichunguzwe kama ni mzembe. Alafu kama hakutumia hizo bil 5.1 kwani yeye alizuia zisitumike .Madiwani na baraza zima kwa nini hawakuhoji?

Mwisho kwani akiwa mayor wa chama kingine ndio ataleta maendeleo? Na kwa nini kumchomoa mtu kw figisu figisu. Hata umeya wenyewe aliupata kwa mbinde mpaka Rais wa JMT alipotoa neno.
Hakimu Janet Mtenga anatafuta Ujaji!
 
Wale wote wanaofanya hujuma kwa upinzani kwa makusudi tuweke rekodi zao siku hi nchi ikikombolewa watajibu unless wawe wametangulia mbele ya haki.

Nchi hii kwa sasa inatawaliwa na vichaa,wendawazimu,malimbukeni na madikteta wa awamu hii…!
Sielewi Rais Magufuli anafurahia nini kuona Viongozi walioko Upinzani na walochaguliwa kwa ridhaa ya Wananchi wanaondolewa kwene Uongozi kwa hila za Serikali ya CCM ikishirikiana na Mahakama ya Kisutu!
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haiwezi kuzuia Meya wa DSM,Isaya Mwita kuondolewa kwenye nafasi yake kwa sababu hakuna uthibitisho wa uwepo wa kikao cha kumuondoa madarakani wala hasara atakayoipata endapo akiondolewa.

Yasema mwombaji hajatoa sababu za msingi za kukidhi vigezo vitatu vya kwanini abaki kwenye nafasi hiyo.

Hakimu asema maombi yamekosa ushahidi kuwa kulikuwa na kikao kinachokusudia kumwondoa madarakani.

“Mahakama hii inatupilia mbali hoja za kutaka muombaji (Mwita) kubaki madarakani kwa sababu hoja za Wakili wa muombaji hazina miguu ya kusimamia kwa kushindwa kufata vigezo ikiwemo uwepo wa kikao cha kutaka kumtoa madarakani”- Hakimu Janeth Mtega.

Uamuzi wa Mahakama kusema haiwezi kuzuia Mwita kuondolewa kwenye Umeya unatokana na maombi yake ambayo aliyawasilisha Jan 6, 2020 ya kutaka kuzuia Kikao cha Baraza la Madiwani wasijadili ajenda ya kumng’oa, kesi ya msingi ya mchakato wa kumuondoa kukiuka Utaratibu imepangwa Jan 13.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kikao Cha Jana hakikua na uhalali wa kumuondoa madarakani hivyo jumatatu nitaripoti kazini kama kawaida.

"Nakusudia kuwashtaki wote waliohusika kufoji saini ya Diwani ambaye yupo nje ya nchi na mmoja wa washtakiwa Hawa atakuwa Kigogo mkubwa tu katika Jiji la Dar es Salaam" Isaya Mwita Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Leo asubuhi nimeripoti ofisini japo mkurugenzi ananipa gari sijui shida nini hivyo nimemuandikia Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam aniletee gari kwa haraka mno" Mstahiki Meya wa Jiji Isaya Mwita.

Pia soma
- Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Meya anyang’anywa gari, ofisi yafungwa. Adai kuwa yeye bado ni Meya halali
Huyo akatafute kazi nyingine asilete ujuaji mwisho akalala mlupango na Mahakama imeshaitupilia mbali kesi yake!
 
Nchi hii kwa sasa inatawaliwa na vichaa,wendawazimu,malimbukeni na madikteta wa awamu hii…!
Sielewi Rais Magufuli anafurahia nini kuona Viongozi walioko Upinzani na walochaguliwa kwa ridhaa ya Wananchi wanaondolewa kwene Uongozi kwa hila za Serikali ya CCM ikishirikiana na Mahakama ya Kisutu!
Kunywa maji upunguze stress
 
Nyie mkiambiwa ukweli mnasema hujuma lisu mlitaka kumuua kisa aliwaoutsmart wajinga nyie na Kama kweli aliwahujumu je Sheria inasema wauwawe?
Msaliti adhabu yake ni moja tu kufugwa jiwe kubwa na kutupwa katika ya bahari kwenye kina kirefu. Kasome Biblia mkuu!
 
Wale wote wanaofanya hujuma kwa upinzani kwa makusudi tuweke rekodi zao siku hi nchi ikikombolewa watajibu unless wawe wametangulia mbele ya haki.
Wewe utakuwa umeshaliwa na funza tayari
 
Tuambie kulikua na hasara gani kutokumchagua kua meya?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakukuwa na hasara yoyote..kuchaguliwa kuwa MEYA haina maana kwamba ww una akili zaidi kuliko madiwani wengine. Kuchaguliwa kuwa MEYA ni utaratibu wa kawaida tu kwamba madiwani wakishachaguliwa wanachagua miongoni mwao mmoja awe meya na mwingine awe naibu...!!

Nashangaa huyu MEYA anavyotokwa na povu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom