KISUTU: Mahakama yamuachia huru Yusuf Manji katika kesi ya dawa za kulevya iliyokuwa ikimkabili

kimpango

JF-Expert Member
Apr 24, 2011
600
716
Niko Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi Mh.Cyprian Mkeha. Leo hukumu ya kesi ya matumizi ya Dawa za kulevya dhidi ya Mfanyabiashara Yusuf Manji itasomwa.

Nitawajuza baada ya hakimu kumaliza...

UPDATES:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 6 mwezi wa 10, 2017 imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa.

Sababu kuu ni kuwa mtuhumiwa alikuwa na bado anatumia dawa mbalimbali kwa matibabu yake kulingana na maagizo ya daktari na dawa hizo zina elements za morphine ambayo pia inaweza kukutwa kwenye heroin kwahiyo maabara ya Mkemia Mkuu ingeenda mbele zaidi kujua morphine iliyokutwa kwa mtuhumiwa imetokana na nini. Hilo ndio limesababisha Manji kuachiwa HURU.

Wakili wa Manji akiongea baada ya kesi

Manji mahakamani

OQ
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru mfanyabiashara, Yusuf Manji katika kesi ya dawa za kulevya iliyokuwa inamkabili.

Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema upande wa mashitaka ameshindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi yake.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alias Daudi Albert Bashite ndiye aliyemtangaza Yusuph Manji kuwa ni mhusika wa madawa ya kulevya. Ndiye hasa alisababisha Manji kushikiliwa na Polisi, kupimwa na hata kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi ya madawa ya kulevya.

Leo, Manji ameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusafishwa kuwa hatumii madawa ya kulevya. Kinachofuata, na napenda iwe hivyo, ni kwa Manji kumshtaki Makonda kwa kumdhalilisha na kumtweza utu na heshima yake kwenye jamii. Kwa kumsisha na madawa ya kulevya.

Makonda lazima ashughulikiwe kisheria. Lazima aoneshwe kuwa kuropoka na kutaja kwa kuwahusisha watu na madawa ya kulevya si jambo dogo wala jepesi. Kumshtaki mtu kwa hila au kutaka sifa tu si jambo la kuliacha lipite hivi hivi. Makonda alipe alichokitaka. Makonda avune alichokipanda.

Bunduki za nini tena jamani katika kujenga hoja!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kibiti, Pwani)
 
Niko Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi incharge Mh. Mkeha. Leo hukumu ya kesi ya matumizi ya Dawa za kulevya dhidi ya Mfanyabiashara Yusuf Manji itasomwa.

Nitawajuza baada ya hakimu kumaliza...

UPDATES:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 7 mwezi wa 10, 2017 imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa.

Sababu kuu ni kuwa mtuhumiwa alikuwa na bado anatumia dawa mbalimbali kwa matibabu yake kulingana na maagizo ya daktari na dawa hizo zina elements za morphine ambayo pia inaweza kukutwa kwenye heroin kwahiyo maabara ya Mkemia Mkuu ingeenda mbele zaidi kujua morphine iliyokutwa kwa mtuhumiwa imetokana na nini. Hilo ndio limesababisha Manji kuachiwa HURU.
safi...sasa ale sahani moja na Bashite kwa defamation!!
 
Back
Top Bottom