KISUTU: Kigogo aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya Sh 323 milioni toka akaunti ya Escrow aachiwa huru

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya Sh 323 milioni toka kwa James Rugemalira fedha ambazo ni sehemu ya zilizotoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa amemuachia huru Rugonzibwa leo Alhamisi baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kuomba kesi hiyo iondolewe mahakamani hapo chini ya kifungu cha 98 (a) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) na Mahakama kuridhia.

Rugonzibwa alifikishwa na Takukuru mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 14, 2015 akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya Sh 323 milioni toka kwa Rugemalira fedha ambazo ni sehemu ya zile Akaunti ya Tegeta Esrow.

Hata hivyo baadaye alibadilishiwa hati ya Mashtaka na kusomewa upya ambayo hayakuonyesha tena kuwa fedha zilizopokelewa na Mujunangoma toka kwa Rugemalira ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.

Kupitia hati hiyo mpya, Rugonzibwa alikuwa akidaiwa kuwa Februari 5, 2014 akiwa mtumishi wa Serikali kama Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipokea rushwa ya Sh Sh323 milioni kupitia akaunti yake namba 00120102602001 iliyopo kwenye Benki ya Mkombozi .

Alidaiwa kuwa alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Rugemalira, ambaye ni mshauri huru wa kitaalamu, mkurugenzi wa VIP na mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa kampuni hiyo.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa umekwisha kamilika.

CHANZO: Mwananchi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nasikia kuna mahakama ya mafisadi.

Labda akiamia upinzani ushaidi unaweza kukamilika na kuchukuliwa hatua.
Ukiwa na uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo, tanzania sio sehemu salama kwako.
Hii nchi sasa hivi ni salama kwa mambulula
 
Hahaaaaaaa lazima wawaachie kuna watu ndio wapishi wakuu wa yote mbaya zaidi hawagusiki wanalindwa.
 
Hayo ni mazingaombwe ya Taasisi ya Kutetea na Kukuza Rushwa nchini. Ukiwauliza wengine mbona hamjawagusa na huyu ana kesi ya kujibu mbona mmemuachia huru? watakujibu ni maagizo toka mamlaka za juu AKA Ikulu au watang'aa macho. Serikali ya majizi, mafisadi na pia yanayopenda rushwa ndivyo ilivyo Mkuu.

Mbona orodha ya waliopokea fedha za Rugamalila ni ndefu lakini waliopelekwa mahakamani ni wa kuokoteza?
 
Back
Top Bottom