KISUTU: Kigogo aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya Sh 323 milioni toka akaunti ya Escrow aachiwa huru

Hayo ni mazingaombwe ya Taasisi ya Kutetea na Kukuza Rushwa nchini. Ukiwauliza wengine mbona hamjawagusa na huyu ana kesi ya kujibu mbona mmemuachia huru? watakujibu ni maagizo toka mamlaka za juu AKA Ikulu au watang'aa macho. Serikali ya majizi, mafisadi na pia yanayopenda rushwa ndivyo ilivyo Mkuu.
Hiyo ndiyo tafsiri sahihi
 
Soon ruge na seth watakuwa huru,tutajumuika nao uraiani

Ova
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Awamu hii hawatashinda kesi hata moja tu ya Ufisadi ............................!!
Ruge na seth watamuita yule mkulu mstaafu Kama shahidi wao maana yeye alishasema fedha hizo syo za umma....hapo Mapema sana kesi kwishaaa....
Kama ile kesi ya mahalu?

Ova
 
Ruge na seth watamuita yule mkulu mstaafu Kama shahidi wao maana yeye alishasema fedha hizo syo za umma....hapo Mapema sana kesi kwishaaa....
Kama ile kesi ya mahalu?

Ova
Kesi za chuki au visasi huwezi shinda ............... Kinachoendela ni kuwakomoa tu kwa kuwalaza Ukonga.

Yaani hapa pesa ya walipa kodi inapotea bure!!
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya Sh 323 milioni toka kwa James Rugemalira fedha ambazo ni sehemu ya zilizotoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa amemuachia huru Rugonzibwa leo Alhamisi baada ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kuomba kesi hiyo iondolewe mahakamani hapo chini ya kifungu cha 98 (a) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) na Mahakama kuridhia.

Rugonzibwa alifikishwa na Takukuru mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 14, 2015 akikabiliwa na shtaka la kupokea rushwa ya Sh 323 milioni toka kwa Rugemalira fedha ambazo ni sehemu ya zile Akaunti ya Tegeta Esrow.

Hata hivyo baadaye alibadilishiwa hati ya Mashtaka na kusomewa upya ambayo hayakuonyesha tena kuwa fedha zilizopokelewa na Mujunangoma toka kwa Rugemalira ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.

Kupitia hati hiyo mpya, Rugonzibwa alikuwa akidaiwa kuwa Februari 5, 2014 akiwa mtumishi wa Serikali kama Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipokea rushwa ya Sh Sh323 milioni kupitia akaunti yake namba 00120102602001 iliyopo kwenye Benki ya Mkombozi .

Alidaiwa kuwa alipokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Rugemalira, ambaye ni mshauri huru wa kitaalamu, mkurugenzi wa VIP na mkurugenzi wa zamani wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL kama tuzo kwa kushughulikia mambo ya ufilisi wa muda wa kampuni hiyo.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa umekwisha kamilika.

CHANZO: Mwananchi
Tatizo ni wanasheria wa serikali, prosecutors, hawawezi wasilisha na kutetea hoja zao!
 
Makufuli maana yake ni kuyafunga mafisadi.Alisema uncle mwenyewe ila ndo hivo tena
 
Jamani sie tupo busy tunaandaa maandamano ya kumpongeza mkulu kwa kupambana na Rushwa
 
Ningeshangaa sana,, maana hii ingekuwa mara ya kwanza kwa taahira kufanikisha mapambano ya rushwa hapa duniani!!
 
Yule Mbunge alierudsha hela bor angebak nazo tu mambo yenyewe ndio haya kumbe?
 
Back
Top Bottom