Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Tunatawaliwa na serikali ya kibabe na katili sana. Ukitaka uthibitisho, liangalie suala la Kabendera, ombi la mama yake kwa Rais, na sasa msimamo wa serikali kupitia mawakili wake baada ya kifo cha mama. Ni ukatili wa kutisha, Yaani ni kama tuko kwa akina Pinotchet wa Amerika ya Kusini!!!
Sasa kila aliyeko mahabusu mama yake aombe msamaha kwa Rais ndivyo sheria zilivyo hata Rais hasamehi walioko mahabusu bali wafungwa na sio mama zao wanaomuomba Rais awasamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Kama we ni mwanaume jua ipo siku unaweza panusa yakakukuta na ukatamani sana kufanya jambo muhimu ukashindwa ndugu ya duniani ni mengi mno huijui kesho yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa kumpa mifano halisi mwambie dunia ina mengi kuna kesho ambayo yeye haijui bado hata baadae tu haijui
Mkuu tetea uovu maana uko mezani kwa mfalme na sahani yako imejaa mlo wa kutosha, na namna nzuri ya huo mlo ili uweze kushuka utakavyo ni pamoja na kujenga hoja ya kuutetea huo uovu. Hata akina Mwigulu, Nape, Januari nk walikuwa wanatetea uovu enzi za JK wakiwa mezani kwenye mlo kama ww. Ila hiyo warmup inayowakuta hivi sasa akili imewarudia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuombeani mabaya ila itatafsirika vipi mchana huu kila mwendesha mashtaka aliyepo hapo kabla ya kusimamia hiyo "Jamhuri" kila mmoja akapata ujumbe kwenye simu yake "mama yako na mkeo wameaga dunia kwa kugongwa na gari la mkaa"?
Wataendelea kusubiri SAA za kesi kutajwa tena?
Mnaweza kuona ni hadithi, lakini Mungu akitaka kutoa fundisho anatoa tuu. Kitabu cha Kutoka Mungu alimwadhibu Farao kwa watoto wazaliwa wa kwanza kufa nchi nzima usiku mmoja kwa sababu ya moyo mgumu wa mtu mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti hii nayo hoja
Wacha mifano ya Kishamba
Sheria haina hisani
 
Nimewaza hivi, niko upande wa Erick na sipendi jinsi watu wanavyobambikiwa kesi ili kuwakomoa lakini anajua hasa nini alikuwa anakifanya, labda nia yake ilikuwa nzuri lakini alivyofanya haikuwa yenye kupendeza. Yeye mwenyewe anajua hatari iliyokuwa inaweza kumkabili na hata mtakumbuka siku aliyochukuliwa kwake, ukweli alikuwa anapotea ila alikuwa 'amejiandaa' ndio mpaka leo yupo.
Mkuu hapa jukwaani ukieleza ukweli kama huu uliosema hapa hautaeleweka na utaonekana katili sana unashabikia hayo yaliyomkuta Erick.
Ukweli ni kama ulivyosema kwamba Erick alikuwa anajua alichokuwa anafanya na kinaweza kumfikisha wapi.
The obvious truth is, Erick Kabendera new what he was getting himself into. He was putting his freedom and may be his life too in the line.
 
Duniani hakuna haki,,, ndiyo maana kunawatu wanaamua maamuz magumu dhidi ya mamlaka
 
kinachonisikitisha mimi ni kwamba hii kesi ni ya kubambikiwa,Kabendera angekuwa amefanya uhalifu kweli hata mimi ningeunga mkono kunyimwa hiyo ruhusa.
Kubambikiziwa kivipi? Shauri linasema alipokea pesa million zaidi ya 170 na akaanza kuzitumia. Mapato yoyote lazima kwanza ulipe kodi, kitu ambacho hakufanya (kosa la kwanza ni la kutolipa kodi). Kosa la pili (itategemeana na utetezi) ni kwamba vyanzo vya hiyo hela havijulikani na kupokea pesa ambayo utashindwa kuidhibitishia mahakama imetoka wapi basi hiyo ni hela chafu na kibaya zaidi ukianza kuitumia kwa kuiingiza kwenye mzunguko utakuwa unatakatisha pesa (kosa la pili). Makosa yote mawili yanazaa kosa la tatu la uhujumu uchumi. Sasa kwavile Erick ana wakili watajitetea na mwisho wa siku atakuwa huru. Cha msingi hapa tuiachie mahakama ifanyekazi yake.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom