KISUTU: Kesi namba 458 ya Jamhuri dhidhi ya JamiiForums ya kutotumia Kikoa cha .TZ, yaahirishwa kwa mara ya mwisho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
KISUTU: Kesi namba 458 ya Jamhuri dhidhi ya JamiiForums ya kutotumia Kikoa cha .TZ imeendelea tena Mahakamani.

Kesi hii imeahirishwa hadi tarehe 13 mwezi Machi. Sababu ya kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kukosekana kwa shahidi kwa upande wa Jamhuri.

Aidha, Hakimu anayeendesha kesi hiyo Nongwa amewaambia Upande wa Jamhuri kuwa inawezekana wanataka Washtakiwa waendelee kuwa na kesi mahakamani kwa kuwa kila mara wanaaihirisha kesi kwa kisingizio cha kukosa mashahidi na hata wakiwa na mashahidi wanaairishwa kwa kisingizio cha kuwa busy na kesi nyingi zinazoingiliana. Hakimu ameongeza kuwa anatambua kuwa akifuta kesi hii washtakiwa watakamatwa tena.

Hakimu Nongwa amesema hili ni ahirisho la mwisho kabisa katika kesi hii.

Tulipoishia=>Kesi namba 458 (Jamhuri vs JamiiForums) yasikilizwa na kuahirishwa hadi Novemba 20, 2017
 
Ha haa. Hizi kesi za Jamuhuri vs JF huwa zinanifurahisha sana. Yani ni kama bembea. Mbele hawataki kwenda na nyuma hawataki kurudi.
 
Kesi za kutengeneza mara nyingi huwa zinaitia aibu Serikali ya awamu hii ya 5 maana inapenda sana kesi za kijinga
 
Back
Top Bottom