KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums), Hakimu aomba muda zaidi kutatua tatizo la kisheria kwenye jalada la kesi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Kesi namba 456 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) ambapo kampuni ya OilCom iliandikwa katika mtandao wa JamiiForums ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandarini Dar (iliyopo chini ya Hakimu Thomas Simba) imetajwa tena leo Mei 03, 2018

Shauri hili limeahirishwa mpaka Juni 01, 2018 baada ya Hakimu Simba kusema anahitaji muda zaidi ili kutatua tatizo dogo la kisheria alilokumbana nalo wakati anasoma jalada ya shauri hilo.

Ikumbukwe Hakimu Simba mara ya mwisho kusikiliza shauri hili Aprili 09, 2018 aliomba pia muda wa kutatua tatizo hilohilo.

Hakimu Simba anasubiriwa kutoa uamuzi mdogo juu ya ushahidi uliochapishwa(printed copy) na kutolewa na upande wa Jamhuri.

Kwa kujua kesi hii ilipotokea rejea hapa - KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums), Hakimu ashindwa kutoa uamuzi mdogo kutokana na tatizo la kisheria
 
Uelekeo unaonekana kabisa, kuna juhudi flani zinafanyika..ok tuone mwisho wake
Inawezekana kabisa ikawa hivyo au anahofia kufanya uamuzi ambao ni wa haki lakini yule dhalimu hatoupenda. Mahakama haziko huru tena.
 
Binafsi Hata wakifunga Jf Sawa kwasasa Jf ni genge la wahuni tu

Aisee watu wengine sijui kichwani mmejaza nini tu.....

Unaita JF ni "genge la wahuni", huku wewe meenyewe ume - subscribe. Maana yake hata wewe ni muhuni tena usiye hata na chembe chembe za maarifa!!
 
Back
Top Bottom