Kisutu: Hakimu amesema atakaposhikwa na mashetani ataifuta kesi ya vigogo wa NIDA

nkanga chief

JF-Expert Member
May 31, 2016
2,084
1,620
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Respicious Mwijage ameuambia upande wa mashtaka kuwa siku akipandwa na mashetani ataifuta kesi ya vigogo wa Mamlaka ya Vitambulisho vyaTaifa (NIDA) endapo kama upelelezi hautakamilika.

Hakimu Mwijage alitoa angalizo hilo baada ya Wakili wa Serikali, Peter Vitalis kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na baada ya kusema hayo, Hakimu Mwijage alisema kesi hiyo ina takribani siku 365 na upelelezi haujakamilika jambo ambalo linatoa taswira mbaya.

“Kamilisheni upelelezi ili kama hawa wamekula fedha za umma wafungwe au kama hawajala waachiwe huru, siku mashetani yangu yakipanda nitafuta hii kesi.”

Hakimu Mwijage aliahirisha kesi hiyo hadi December 6,2017 huku akiutaka upande wa mashtaka kufika na taarifa kuhusu upelelezi.

Kesi hiyo inamkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa (NIDA), Dickson Maimu na wenzake saba, ambao wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 1.16.

Mbali na Maimu, washtakiwa wengine ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Xavery Kayombo, Meneja Biashara wa mamlaka hiyo, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Joseph Makani.

Washtakiwa pamoja na mashtaka mengine yakiwemo kuisababishia Serikali hasara wanadaiwa tarehe tofauti kati ya January 15 hadi 19, mwaka 2010 katika Makao Makuu ya NIDA wilayani Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kwa nafasi walizokuwa nazo walitumia madaraka vibaya kwa kuidhinisha malipo bila kufuata viwango vya kubadilishia fedha.

MillardAyo
 
Mara nyingi kesi za kubaka na kuiba kuku ndio Zina ushahid
 
Chanzo: Mwananchi
 
Huyu hakimu hajui bwana yule alivyokuwa anatoa maelezo kwa nguvu na povu kuhusu hela za NIDA zilivyoliwa? asijikute anafutwa yeye tu
 
Faza1980 RAIS HANA MAMLAKA YA KUMFUTA KAZI HAKIMU/JAJI. HATA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA ILI KUMFUTA KAZI HAKIMU LAZIMA IWE NA SABABU ZINAZOELEWEKA NA USHAHIDI, VINGINEVYO NI HASARA KWA KODI ZETU.
 
Muachie ajitie uwendawazimu tu, hayo mashetani yake yote yatamtoka.
 
Mbali na Maimu, washtakiwa wengine ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa NIDA, Benjamin Mwakatumbula, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege, Xavery Kayombo, Meneja Biashara wa mamlaka hiyo, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Joseph Makani.

Washtakiwa pamoja na mashtaka mengine yakiwemo kuisababishia Serikali hasara wanadaiwa tarehe tofauti kati ya January 15 hadi 19, mwaka 2010 katika Makao Makuu ya NIDA wilayani Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kwa nafasi walizokuwa nazo walitumia madaraka vibaya kwa kuidhinisha malipo bila kufuata viwango vya kubadilishia fedha.
Sioni kama kuna uwezekano wa team nzima hiyo kukaa na kupanga malipo yasiyo halali .......... Hii kesi nayo itaishia kufutwa tu.

Kama wameshindwa kupata ushahidi baada ya mwaka mzima kwa mambo yaliyofanyika 2010, sioni kama kunauwezekano wa kupata more info with time. Yaani kadri siku zinavyopita ndivyo ugumu wa kupata more data unavyopungua!!

Imewashinda ya Masamaki, wataiweza hii ya 2010!!?
 
Yampande halafu tusikie na Magogoni upande wa pili.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom