Kisutu: DPP Biswalo, awaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso

Mmh. Hii imefutwa under duress....ujue kuna watu ambao walikuwa implicated walishinda kwa wachungaji balaa - wakitafuta 'breakthrough'. But time will tell...
Duress?? Lete evidence. Haki imetendeka
 
Awalipe fidia sasa.Ni aibu kumweka mtu ndani kisha unakosa ushahidi unamuachia.Civilized country ushahidi kwanza kisha ndo unashikiliwa
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo Alhamisi imewaachia huru, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso Tabura. Hatua hiyo imefikiwa Baada ya aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga kutokuonesha nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.

Upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi ya DPP mahakamani kwamba hana nia ya kuendelea kuwashtaki vigogo hao dhidi ya kesi ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa inawakabili.

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele, ilipokea maombi hayo mapema leo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliomba kuwasilisha hati hiyo iliyotiwa saini Mei 10, 2021 na aliyekuwa DPP (kwa sasa Jaji mteule), Biswalo Mganga.

Tarehe 05/06/2020 aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na mwenzake, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Sh bilioni 1.6. Sambamba na Bwanakunu, mwingine ni aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Logistiki MSD, Byekwaso Tabura.

Wote walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate. Wakili wa Serikali, Faraji Nguka akiwasomea mashtaka washtakiwa hao, alidai kuwa kati ya Juai 1, 2016 na Juni 30, 2019 maeneo mbalimbali ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma, kwa pamoja walitengeneza genge la uhalifu kwa ajili ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 20, 2019, washtakiwa wote kwa pamoja waliisababishia MSD hasara ya Sh 3,816,727,112.75.

Shitaka la tatu ambalo linamkabili Bwanakunu ni matumizi mabaya ya madaraka, ambapo ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2916 na June 30, 2019 katika maeneo ya Keko wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam, kwa makusudi alitumia nafasi yake kulipa kiasi cha Sh 3,816,727,112.75 kwa wafanyakazi wa MSD kama nyongeza ya mishahara na posho, bila ruhusa ya Katibu Mkuu Utumishi, na hivyo kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Katika shtaka la nne, washtakiwa wote wanadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo ya tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa pamoja waliruhusu uhifadhi mbaya wa vifaa tiba, uliosababisha vifaa hivyo kuharibika, hivyo kuisababishia MSD hasara ya Sh 85,199,879.65

Shitaka la tano linalowakabili washtakiwa hao ni utakatishaji fedha, ambapo inadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo ya Keko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam, wote kwa pamoja walijipatia Sh 1,603,991,095.37 wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu, ambao ni kuongoza genge la uhalifu.
Bado yule Mhasibu Mkuu wa TAKUKURU na wenzie pia waachiwe huru maana hawana hatia
 
Ofisi ya DPP inazidi kuonesha kuwa kuna kesi nyingi hazikutakiwa kufika mahakamani wala watu kuozea mahabusu na magerezani.

Mfumo wa "Haki za Jinai " Criminal Justice System ya Tanzania unabidi ufumuliwe ili usitumike kukomoa, kunyima watu dhamana au kuswekwa mahabusu wakati upelelezi hauna ushahidi wa kutosha wakati kesi hiyo haitishii usalama wa taifa au watu.
Upo sahihi mkuu. Watu wanateseka sana ndani ya nchi yao.
 
Ofisi ya DPP inazidi kuonesha kuwa kuna kesi nyingi hazikutakiwa kufika mahakamani wala watu kuozea mahabusu na magerezani.

Mfumo wa "Haki za Jinai " Criminal Justice System ya Tanzania unabidi ufumuliwe ili usitumike kukomoa, kunyima watu dhamana au kuswekwa mahabusu wakati upelelezi hauna ushahidi wa kutosha wakati kesi hiyo haitishii usalama wa taifa au watu.
Huyu Mganga alaaniwe kabisa
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo Alhamisi imewaachia huru, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso Tabura. Hatua hiyo imefikiwa Baada ya aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga kutokuonesha nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.

Upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi ya DPP mahakamani kwamba hana nia ya kuendelea kuwashtaki vigogo hao dhidi ya kesi ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa inawakabili.

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele, ilipokea maombi hayo mapema leo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliomba kuwasilisha hati hiyo iliyotiwa saini Mei 10, 2021 na aliyekuwa DPP (kwa sasa Jaji mteule), Biswalo Mganga.

Tarehe 05/06/2020 aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na mwenzake, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Sh bilioni 1.6. Sambamba na Bwanakunu, mwingine ni aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Logistiki MSD, Byekwaso Tabura.

Wote walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate. Wakili wa Serikali, Faraji Nguka akiwasomea mashtaka washtakiwa hao, alidai kuwa kati ya Juai 1, 2016 na Juni 30, 2019 maeneo mbalimbali ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma, kwa pamoja walitengeneza genge la uhalifu kwa ajili ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 20, 2019, washtakiwa wote kwa pamoja waliisababishia MSD hasara ya Sh 3,816,727,112.75.

Shitaka la tatu ambalo linamkabili Bwanakunu ni matumizi mabaya ya madaraka, ambapo ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2916 na June 30, 2019 katika maeneo ya Keko wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam, kwa makusudi alitumia nafasi yake kulipa kiasi cha Sh 3,816,727,112.75 kwa wafanyakazi wa MSD kama nyongeza ya mishahara na posho, bila ruhusa ya Katibu Mkuu Utumishi, na hivyo kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Katika shtaka la nne, washtakiwa wote wanadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo ya tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa pamoja waliruhusu uhifadhi mbaya wa vifaa tiba, uliosababisha vifaa hivyo kuharibika, hivyo kuisababishia MSD hasara ya Sh 85,199,879.65

Shitaka la tano linalowakabili washtakiwa hao ni utakatishaji fedha, ambapo inadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo ya Keko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam, wote kwa pamoja walijipatia Sh 1,603,991,095.37 wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu, ambao ni kuongoza genge la uhalifu.

Tanzania ni ngumu sana kufanya uongozi kwenye mashirika ya umma kwasababu kuu mbili

1. Hakuna malengo ya mwaka. Kampuni yeyote inatakiwa kuwa na malengo ya mwaka na watendaji wanatakiwa kupimwa kazi kutokana na malengo hayo. Sio kila siku matukio ambayo ni ngumu kufanya utendaji wa kazi
2. Hujui nani ni boss wako. Kila mtu anajaribu kuwa boss wako ingawa umechaguliwa na wengine. Katibu mkuu ni boss, mawaziri wote ni ma boss....... , bodi ya wakurugenzi ni ma boss sasa ni ngumu kuripoti kwa kila mtu .

Hii ndiyo sababu wengine tulikataa kufanya kazi kwenye mashirika ya umma ya serikali. Nilipata mahojiano ya kazi MSD mwaka 2012 lakini nika kataa baaada ya kujua kwamba hata mkurugenzi sio boss wako. Yaani anaweza kuja mwanasiasa akaamua ubadilishiwe mshahara!! ni ngumu sana kuwa mkurugenzi pale kama wewe una ujuzi wa kupata kazi sehemu nyingine.
 
Shetani mganga na ibilisi wenzake, wana mashtaka makubwa mbele ya wanadamu na Mungu, kwa ushetani waliowafanyia Watanzania kwa karibia miaka mitano.
 
Ndio maana nasema zile pesa alizokuwa anakusanya DPP ulikuwa ni uporaji, watu waliogopa kwenda jela bila kosa ndio maana wakawa wanatoa pesa, warudishiwe pesa zao, kama wana ushahidi wa makosa yao wapeleke kesi mahakamani.
 
Back
Top Bottom