Kisutu: DPP Biswalo, awaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo Alhamisi imewaachia huru, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso Tabura. Hatua hiyo imefikiwa Baada ya aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga kutokuonesha nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.

Upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi ya DPP mahakamani kwamba hana nia ya kuendelea kuwashtaki vigogo hao dhidi ya kesi ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa inawakabili.

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele, ilipokea maombi hayo mapema leo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliomba kuwasilisha hati hiyo iliyotiwa saini Mei 10, 2021 na aliyekuwa DPP (kwa sasa Jaji mteule), Biswalo Mganga.

Hati hiyo ilisainiwa chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2019.

Tarehe 05/06/2020 aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na mwenzake, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Sh bilioni 1.6. Sambamba na Bwanakunu, mwingine ni aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Logistiki MSD, Byekwaso Tabura.

Wote walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate. Wakili wa Serikali, Faraji Nguka akiwasomea mashtaka washtakiwa hao, alidai kuwa kati ya Juai 1, 2016 na Juni 30, 2019 maeneo mbalimbali ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma, kwa pamoja walitengeneza genge la uhalifu kwa ajili ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 20, 2019, washtakiwa wote kwa pamoja waliisababishia MSD hasara ya Sh 3,816,727,112.75.

Shitaka la tatu ambalo linamkabili Bwanakunu ni matumizi mabaya ya madaraka, ambapo ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2916 na June 30, 2019 katika maeneo ya Keko wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam, kwa makusudi alitumia nafasi yake kulipa kiasi cha Sh 3,816,727,112.75 kwa wafanyakazi wa MSD kama nyongeza ya mishahara na posho, bila ruhusa ya Katibu Mkuu Utumishi, na hivyo kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Katika shtaka la nne, washtakiwa wote wanadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo ya tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa pamoja waliruhusu uhifadhi mbaya wa vifaa tiba, uliosababisha vifaa hivyo kuharibika, hivyo kuisababishia MSD hasara ya Sh 85,199,879.65

Shitaka la tano linalowakabili washtakiwa hao ni utakatishaji fedha, ambapo inadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo ya Keko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam, wote kwa pamoja walijipatia Sh 1,603,991,095.37 wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu, ambao ni kuongoza genge la uhalifu.

Zaidi;

 
Leo tarehe 13/05/2021 mahakama ya Kisutu imefuta kesi iliyokuwa inawakabili viongozi wa MSD hii ni baada ya Jamhuri kudai haiana nia yakuendelea Nayo.

Tutazidi kupeana updates kuweza kuweka kumbukumbu zetu sawa kuhusu namna Takukuru,Mahakama, Polisi na DPP walivyoshirikiana kwa miaka mitano kujaza mahabusu
 
Leo tarehe 13/05/2021 mahakama ya Kisutu imefuta kesi iliyokuwa inawakabili viongozi wa MSD hii ni baada ya Jamhuri kudai haiana nia yakuendelea Nayo.

Tutazidi kupeana updates kuweza kuweka kumbukumbu zetu sawa kuhusu namna Takukuru,Mahakama, Polisi na DPP walivyoshirikiana kwa miaka mitano kujaza mahabusu
" za kuondokea"
 
Hivi hii ya kuachiwa huru bila ya upelelezi kukamilika na umeshapotezewa muda wako imekaaje?
Serekali inabidi ilipe fidia kwa kweli manake huku ni kukomoana...
serekali ikilipishwa fidia naamini hawatorudia kuleta kesi zisizo na ushahidi
 
Ofisi ya DPP inazidi kuonesha kuwa kuna kesi nyingi hazikutakiwa kufika mahakamani wala watu kuozea mahabusu na magerezani.

Mfumo wa "Haki za Jinai " Criminal Justice System ya Tanzania unabidi ufumuliwe ili usitumike kukomoa, kunyima watu dhamana au kuswekwa mahabusu wakati upelelezi hauna ushahidi wa kutosha wakati kesi hiyo haitishii usalama wa taifa au watu.
 
Serekali inabidi ilipe fidia kwa kweli manake huku ni kukomoana...
serekali ikilipishwa fidia naamini hawatorudia kuleta kesi zisizo na ushahidi
Mmh. Hii imefutwa under duress....ujue kuna watu ambao walikuwa implicated walishinda kwa wachungaji balaa - wakitafuta 'breakthrough'. But time will tell...
 
Back
Top Bottom