Kisutu, Dar: Soudy Brown, Shaffih Dauda, MC Luvanda na wengineo wafikishwa mahakamani, wapata dhamana

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,745
4,277
Soudy Brown, Shaffih Dauda, MC Luvanda na wengine 4 waliokuwa wanashikiliwa na polisi kwa zaidi ya siku 7 wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo

Walishikiliwa kwa kumiliki na kurusha maudhui kupitia chaneli za YouTube ambazo hazijasajiliwa na TCRA.

UPDATE:
Soudy amepata dhamana Mahakama ya Kisutu baada ya kudhaminiwa na mdhamini mmoja na bondi ya Sh. Milioni 2... Kosa: Kuendesha akaunti ya YouTube na kuweka maudhui bila leseni

Habari zaidi...

Shafii Dauda na Felix Kadege wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa kosa moja la kutumia ONLINE TV bila ya kuwa na kibali.

Washtakiwa hao wameachiwa baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 wenye vitambulisho, barua zinatambulika.

Pia kila mdhamini kusaini bondi ya Sh.Milioni 15 na hawaruhusiwi kusafirisha nje ya Tanzania bila kupata kibali cha mahakama.

Pia wametakiwa kuwasilisha hati zao za kusafirisha mahakamani.

Washtakiwa hao, wamesomewa kosa lao na Wakili wa serikali Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakimu Mfawidhi Kelvin Mhina.

Awali akisoma shtaka lao, Wakili Kombakono amedai kuwa washtakiwa wametenda kosa hilo, kati ya June 14 na September, 2018 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa kutumia ONLINE TV inayojulikana kwa jina la Shafii Dauda kinyume cha sheria.

Inadaiwa walitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa hao walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo wakili Jebra Kambole anayewatetea washtakiwa hao aliomba wateja wake hao wapewe dhamana kwa sababu shtaka linadhaminika.

Washtakiwa walifanikiwa kupata dhamana na kesi yao imeahirishwa hadi October 8, 2018.

=======

UPDATES: 17 march 2020

========


Mahakama ya Kisutu imemhukumu mwandishi wa habari Shafii Dauda na Benedict Kadeghe ambaye ni mtaalamu wa Tehama kulipa faini ya Shilingi milioni tano kila mmoja ama kufungwa miezi 12 gerezani baada ya kukiri kosa lao la kuchapisha maudhui mtandaoni bila leseni.

Kisutu: Shafii Dauda na Benedict Kadeghe Wahukumiwa kulipa Mil 5 kila mmoja au Jela miezi 12, kwa kosa la kuweka Maudhui YouTube
 
Wasanii wa bongo waoga kinoma; wanaishia kutweet tu nyuma ya keyboards zao, tena kwa kuuma na kupuliza.

Basi nikajua leo hata at least watakusanyika na mabango nje ya mahakama kuwasapoti wenzao, ila hamna kitu.

Ndio maana wana awamu hii inawaburuzwa na kwaudharau.
 
Back
Top Bottom