Kisutu, Dar: Ndama ‘mtoto wa ng’ombe’ ahukumiwa, alipa faini na kuwa huru

Moja ya watu waliofurahia kifo cha Hayati Magufuli ni huyu tapeli sugu Ndama Mutoto ya Ng'ombe. Chuma kingelikua hai huyu alikua anaozea Jela.
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu mfanyabiashara Ndama Hussein na Mkemia Yusuph Yusuph, kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5 au kwenda jela miaka mitano baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kujipatia Dola za Marekani 75,000 kwa njia ya udanganyifu.

Kiasi hicho walijipatia kutoka kwa raia ya Botswan Emmanuel Motilhathedi baada ya kumdanganya kwamba wana kampuni ya dhahabu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya, baada ya washitakiwa hao kuandika barua ya kukiri kosa na kisha kuingia makubaliano na Mkurugenzi ya Mashtaka nchini( DPP).

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya, alisoma maelezo ya makubaliano hayo kwamba fidia inakwenda katika akaunti ya mlalamikaji ambaye alitapelewa.

Alidai katika makubaliano tayari mlalamikaji ameshalipwa kiasi cha Dola za Marekani 50,000 katika akaunti yake na kiasi kilichobakia kinalipwa ndani ya miezi minne kuanzia sasa.

Alifafanua kuwa kuanzia Septemba 31, mwaka huu washitakiwa wanatakiwa kulipa Dola 12,500 na kumalizika kiasi kilichobakia Novemba 31 mwaka huu katika akaunti yake.

Hata hivyo washitakiwa walifanikiwa kulipa faini hiyo na kukwepa adhabu ya jela.

Wakili Komanya, kutokana na ushahidi ulioko washitakiwa walitekeleza kwa pamoja genge la uharifu kujihusisha na biashara ya kuuza madini feki kwa raia wa Botswana ambapo waliweza kumlaghai kuwa Kampuni yao inajihusisha na madini.

Baada ya mawasiliano kwa njia ya simu na barua pepe na raia huyo kabla ya kufika nchini Januari 2021 akishirikiana nao kwa hatua mbalimbali waliwapatia Dola za Marekani 150,000 ili wampatie shehena ya dhahabu kilogramu 500.

Waliendelea kumshawishi mlalamikaji huyo kwamba anatakiwa kutoa fedha kwa ajili ya tozo la vibali ndipo alipowashtukia na kufanya ufuatiliaji kwa wahusika wa madini na kujiridhisha kwamba madini hayo ni feki.
Mkuu mbona hatuna September 31 na November 31. Wewe unatumia kalenda ya sayari ipi?
 
Only in Tanzania wanamshikilia Gaidi Mbowe wanaachia hawa wauza ngada, very interesting counrty, tuendelee kujifukiza ndugu zangu
 
Anatuongopea hadi sie kina "sina kitu"?

hapana huyu madili yake hasa watu wazito.au akiwa anawaongepea watz wenzake ni mambo ya udalali wa nyumba na nyumba zenyewe ni maeneo ya kwa wakubwa.ukae tahadhari tu Ndama ni G.O.A.T kwa dar.tena kasi watakayorudi nayo nina wasiwasi itakuwa ya 5G
 
hapana huyu madili yake hasa watu wazito.au akiwa anawaongepea watz wenzake ni mambo ya udalali wa nyumba na nyumba zenyewe ni maeneo ya kwa wakubwa.ukae tahadhari tu Ndama ni G.O.A.T kwa dar.tena kasi watakayorudi nayo nina wasiwasi itakuwa ya 5G
Hahahah Eti GOAT
 
Anatuongopea hadi sie kina "sina kitu"?

Mwenyewe amefurahi anarudi sasa wengine wote wakasome tu.
IMG_3901.jpg
 
Back
Top Bottom