KISUTU, DAR: Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA), Zodo Miraji wamefikishwa mahakamani

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,507
KISUTU, DAR: Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA), Zodo Miraji wamefikishwa katika Mahakama hiyo kwa tuhuma za kuhujumu uchumi na kuisababishia taasisi hiyo hasara ya Takribani Tsh Milioni 147 Kwa mujibu wa Wakili wa TAKUKURU, Bwana.

Max Ally akiwa mbele ya Hakimu anayeendesha kesi hiyo Thomas Simba alidai Mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo kati Mei 01, 2014 na Mei 01, 2016. Wakili huyo anadai kuwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake vizuri Bwana.

Zodo aliisababishia taasisi hiyo hasara ya Tsh. 147,256,661.53 Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alipewa nafasi ya kuongea na alikana kosa hilo. Mahakama ilisikiliza kesi hiyo kutokana na kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP). Wakili wa upande wa utetezi Jamuhuri Johnson, aliomba Mahakama itoe dhamana kwa mstakiwa.

Upande wa Mashtaka uliridhia ombi hilo na ulieleza kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo waliomba Mahakama ipange siku ya kutaja tena kesi hiyo Hakimu Simba aliridhia kutoa dhamana na kusema kuwa masharti ya dhamana ni kwamba mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja atasaini bondi ya Tsh 73,000, 700 Aidha, alimtaka Mshtakiwa awasilishe hati yake ya kusafiria mahakamani hapo na asitoke nje ya bila ya kibali cha Mahakama Mshtakiwa alikamilisha masharti ya dhamana na kesi kuhairishwa mpaka Aprili 16, 2018.
 
tatizo mwisho wa siku adhabu atakayo pewa hailingani na hasara aliyo isababisha!!!!!!!
 
Tungekua na mahakama nzuri haya makosa ya uhujumu uchumi tungekuaga tunayasikia kwenye redio tu.

Wanakuja wapuuzi wametumwa na bwana wao wanafikia kufungulia mtu kesi ya uhujumu uchumi, ivi uhujum uchumi wanajua maana yake???

Ni kwel kwamba kila mtu yupo kwenye nafasi kuhujumu uchumi???
 
Back
Top Bottom