Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

Dereva wa Mbowe alivyokamatwa ndio kaongea yote haya
Mbowe alikaa kimya muda wote dereva wake yupo ndani kwa nini hakuwaeleza nyumbu hii habari?
Watu wanadhani hii kesi ni simple, na kuna yule bodyguard wa Mbowe aliekamatwa na kupewa tuhuma za ugaidi enzi za JPM,mpaka leo yupo rumande na Mbowe hajawahi kuzingumza chochote.
 
Nchi inaangaika sana hii.Imetoka kubambikia watu kesi za uhujumu uchumi sasa hivi wameamia kwenye ugaidi.Hao viongozi wangekua wanaangaika hivi kuleta maendeleo kwa hakika tungekua mbali sana.ila nasikitika kusema akili zetu ni kiasi kidogo sana.Ujinga kama huu utakuja kua na mwisho mchungu siku moja.
 
Sio msemaji lakini aliyatamka yale maneno kwenye kongamano halali la CHADEMA, na kwakua hakuna kiongozi yeyote wa chama aliyejitokeza kuipinga kauli ile ni wazi kuwa ilikuwa na baraka zote...
CHADEMA wanazipenda confrotational politics ila mwisho wa siku wao ndio huumia, ila nimejifunza kitu, hizi kesi huwafanya kupiga hela za michango tu hamna lolote.
 
Nchi inaangaika sana hii.Imetoka kubambikia watu kesi za uhujumu uchumi sasa hivi wameamia kwenye ugaidi.Hao viongozi wangekua wanaangaika hivi kuleta maendeleo kwa hakika tungekua mbali sana.ila nasikitika kusema akili zetu ni kiasi kidogo sana.Ujinga kama huu utakuja kua na mwisho mchungu siku moja.
ujinga wa mbowe ni kutokuwa na subira yaani mtu muungwana kama mama anawaambia tuwe na subira katiba inakuja anatokea mbowe hatutaki lazima sasa hivi anatokea mdude nitamnyoa huyo mama yenu kwakweli hata angekuwa huyo mbowe ndiyo yuko madarakani asingekubali ujinga wake anaoufanya sasahivi
 
Tanzania 🇹🇿 hii ya mapito!! Gaidi wiki mbili zilizopita alipata Salaam za rambirambi toka kwa Rais wa nchi.
 
Kukusanya watu wakati wa janga(epidemic) kama korona ni ugaidi, acha ashughulikiwe!

Na zile hela wanazopokeaga Nairobi baada ya Lissu kuzisomba toka ulaya wanadhani vipepeo hawazionagi? Vipepeo wako katika inner circle ya Chadema,mnakaa mnapanga, zinavujishwa!

Angalia kiwango kikubwa cha usaliti wa viongozi wakuu wa CDM, Mashinji, aliyekuwa katibu mkuu Bavicha sasa waziri, angalia wabunge wa COVID, chama kimeingiliwa siafu,wametoka baadhi tu,wengi wamo bado
Endelelea kurembua utapata bwana
 
Tatizo na nyinyi Chadema mlianza shobo mapema sana kwa Samia mlikuwa nyinyi ndo mmepewa kazi ya kusifu na kuabudu ghafla mwenyekiti wenu kajitokeza alipojificha na kutaka kukutana na Rais lile tu nikajua bhasi siku zote mwanamke ukimshobokea sana anakudharau hata kama alikuwa na interest na ww

Jpm pamoja na mabaya yake wanayosema Chadema hakuwahi kumpa kesi ya Ugaidi mwenyekiti wa wachaga na Chadema Mr Mbowe . Sasa Serikali ya Muhula wa 6 mliyokuwa mnaipamba na kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu kwa roho mbaya zenu juu ya JPM, inamweka ndani Mwenyekiti wenu na Kesi ya Ugaidi


Mbowe yupo kundi Moja na Osama na Chadema ni Chama cha kigaidi kikiungana na Abu Sayyaf Group (ASG),Afghan Taliban,Al-Nusrah Front, Al-Shabaab,Ansar al-Sharia, Ansar Bayt al-Maqdis (ABM), Al-Qa'ida Core (AQ)
Endelea kurembua mzutii upakuliwe vizuri,bladifaken
 
Yule mama anaongoza nchi kwa kufuata sheria

Kama Freeman anahusika na hizo tuhuma atashughulikiwa, kama hahusiki ataachiwa

Tuache vyombo husika vifanye kazi yake
Kweli ccm akili huwa hamna,mmebaki kutegemea policeccm
Screenshot_20210725-085611_Twitter.jpeg
 
Kweli ccm akili huwa hamna,mmebaki kutegemea policeccmView attachment 1869854

Huyo alikamatwa na kushughulikiwa kadri ya makosa yake, na wengine watakamatwa na kushughulikiwa pia

Uhalifu sio kukutwa na silaha pekee, silaha ni matokeo ya mipango iliyokuwepo. Sasa wacha serikali ishughulike na ile mipango ya Wembe wa wanachadema waliomnyolea mtangulizi na sasa wanatishia kumnyoa na mama
 
Yaani Ugaidi aliutenda may-Aug 2020 wakati wa Utawala wa Mwendazake akaachwa mpaka alipoanza kudai Katibu Mpya ndiyo akakamatwa?
Kwa staili hiyo kama Mungu hataingilia kati tutarajie kumsahau uraiani!
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kusomewa mashtaka mawili likiwemo la Ugaidi.

Mbowe amefikishwa katika Mahakama hiyo leo July 26, 2021 na kusomewa mashataka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Tulimanjwa Majigo amesema kuwa Mbowe anaunganishwa na Washtakiwa wengine watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka mengine yote ya ugaidi wanayodaiwa kuyatenda mwaka 2020.

Katika kosa la kwanza, Mbowe anadaiwa kula njama ya kutenda kosa hilo kati ya Mei na Agosti 2020 akiwa katika Hoteli ya Aishi Mkoani Kilimanjaro, kosa la pili la Mbowe ni kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi kinyume cha sheria ya ugaidi kati ya tarehe hizo tajwa.

Baada ya kusomewa maelezo Mbowe hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 5, 2021 na upelelezi umekamilika ambapo zinasubiriwa nyaraka ili ihamishiwe Mahakama Kuu


haya
 
Sasa hapo ndo watapoteana kabisa, watapigwa mpaka wachake.Labda watafute nchi yoyote itakayowapa hifadhi wakati wanaandaa hao vijana wa kigaidi ila sio Tz.
Mshauri wao Kigogo kawambia watafute nchi wakaanzishe mapambano.
 
Unatetea upuuzi huu seriously?
"They" ni hao wanaomfungulia mashtaka. Hao ambao Mkuu wa Nchi alituambia wana tabia ya kuwabambikizia watu kesi.

Amandla...

Too early to say anything. Kwa vile issue yake iko mahakamani sasa, mbichi na mbivu tutazijua, sooner or later!
 
juu









Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na kusomewa mashtaka mawili ikiwemo la ugaidi.

Mbowe amefikishwa katika Mahakama hiyo jana July 26, 2021 na kusomewa mashataka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Tulimanjwa Majigo amesema kuwa Mbowe anaunganishwa na Washtakiwa wengine watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka mengine yote ya ugaidi wanayodaiwa kuyatenda mwaka 2020.

Katika kosa la kwanza Mbowe anadaiwa kula njama ya kutenda kosa ambapo anadaiwa kula njama hiyo kati ya Mei na Agosti 2020 akiwa katika Hoteli ya Aishi Mkoani Kilimanjaro, kosa la pili la Mbowe ni kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi kinyume cha sheria ya ugaidi kati ya tarehe hizo tajwa.

Baada ya kusomewa maelezo Mbowe hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka, kesi imeahirishwa hadi Agosti 5, 2021 na upelelezi umekamilika ambapo zinasubiriwa nyaraka ili ihamishiwe Mahakama kuu.
 
Back
Top Bottom