Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,635
40,790
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kusomewa mashtaka mawili likiwemo la Ugaidi.

Mbowe amefikishwa katika Mahakama hiyo leo July 26, 2021 na kusomewa mashataka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Tulimanjwa Majigo amesema kuwa Mbowe anaunganishwa na Washtakiwa wengine watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka mengine yote ya ugaidi wanayodaiwa kuyatenda mwaka 2020.

Katika kosa la kwanza, Mbowe anadaiwa kula njama ya kutenda kosa hilo kati ya Mei na Agosti 2020 akiwa katika Hoteli ya Aishi Mkoani Kilimanjaro, kosa la pili la Mbowe ni kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi kinyume cha sheria ya ugaidi kati ya tarehe hizo tajwa.

Baada ya kusomewa maelezo Mbowe hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 5, 2021 na upelelezi umekamilika ambapo zinasubiriwa nyaraka ili ihamishiwe Mahakama Kuu
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom