ISIS
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 96,073
- 858,529
Awamu ya tano si mchesoKwa hiyo pasaka itawakuta rumande?
Awamu ya tano si mchesoKwa hiyo pasaka itawakuta rumande?
Angalia wanaoondoka CHADEMA wanatoa picha gani? wanaobaki ndo hao ninaosema..... Data zako ni mgando, watu wanatoka na wanaendelea kutoka, wao wanaona ujinga uliopo huko. Umeweka data mgando, dunia ina move mbele, inaenda mbele hao wa 2015 si wote wamebaki huko, wengi wameondoka ...tumia akili kufikiri.
Umembiwa gari mbovu. Tulia
Washauri ccm wenzako waache wizi wa Mali za umma na UFISADI kwa ujumla. Wananchi mmewafanya sehemu ya kuchumia vipatoMimi sijazaliwa uingereza wala sina uhusiano na familia ya malkia hicho kingereza nilichoandika nimejitahidi kinatosha kama hujaelewa shauri yako kwani wewe umeolewa na familia ya malkia wa uingereza?
Ni shangwe tupu, dah kikundi hiki cha waharifu wanaspend pasaka wakiwa kolokoloni, hahahaha, Mungu ni kubwa. Tena wakithibitika na hatia wafungwe kabisa.Leo Mwenyekiti wa Chadema Mhe Freeman Mbowe pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema wanatarajia kufikishwa Mahakama ya Kisutu Kwa ajili kusikiliza shauri la dhamana leo
======
UPDATES:
======
04:00pm > Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza hoja zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri na utetezi amesema Aprili 3, 2018 washtakiwa waletwe mahakamani wasaini bondi wakishakuwa huru ndiyo zoezi zima la taarifa ya kukata rufaa kama Jamhuri ilivyoonyesha nia litafanyika.
03:20pm > Upande wa Jamhuri (mashtaka) wamesema hawajaridhishwa na uamuzi wa kutoa dhamana na watakata rufaa. Hii ni kwa mujibu wa wakili wa Jamhuri, Faraja Nchimbi. Wanasema kuwa usalama wa umma unaweza kuwa shakani kwa washtakiwa kuwa huru mtaani.
Hakimu amekubaliana na Wakili Kibatala kuwa mawakili wa Jamhuri hawakuwa na hoja za msingi wa kisheria kupinga dhamana kwa washtakiwa.
03:00pm > Hatimaye Hakimu ametoa dhamana kwa washtakiwa! Kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya Sh. Milioni 20 na wawe na barua toka kwa viongozi wao wa vijiji ama S/Mtaa na wawe na nakala za vitambulisho vyao.
Watatakiwa kuripoti Polisi kila Alhamisi (Central Police)
02:25pm > Wakili wa Jamhuri anamuomba mkuu wa Logistics za kuleta wafungwa Kisutu, aliyemtaja kwa jina moja la Shaban aeleze sababu za watuhumiwa kutofika mahakamani. Shaban anasema asubuhi aliwasiliana na mkuu wa gereza la Segerea ambaye alisema gari limeharibika.
2:08pm > Hakimu na Mawakili wa pande zote wanaelekea kwenye Ukumbi wa Mahakama. Ukumbi umeshajaa watu tayari. Ni wazi kuna uamuzi flani utatolewa hapa...
2:00pm > Hakimu amewaita mawakili. Waendesha mashitaka hawapo, aijulikani wameenda kula au vipi...
1:50pm > Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amerejea mahakamani akiwa na Ndg. Mgeja. Amefika na kunong’onezana kitu na Wakili Kibatala
View attachment 728573
View attachment 728574
1:20pm > Vurugu nje ya mahakama ya Kisutu now, mtu mmoja amezongwa na kulazimishwa kuondoka kwenye makusanyiko wa wanachama wa CHADEMA.
"Huyooooo huyoooo, ondoka hapa, wewe kibaraka, hatukutaki, ondoka," kelele zimesikika wakimtimua mtu huyo.
Inadaiwa na wanachama hao wa CHADEMA kuwa mtu huyo ni "kibaraka" wa CCM na wengine wakimtuhumu kuwa mwanausalama.
Mtu huyo kaondoka kwa kukimbia akielekea katikati ya jiji.
12:26pm > Wakili Kihwelo ameiambia JamiiForums kuwa Hakimu Mashauri ameamua kusoma uamuzi mdogo, wawepo watuhumiwa ama wasiwepo, kuhusu dhamana ya Mbowe na wenzake. Hatua hii inakuja baada ya Mawakili wa Mbowe na wenzake kwenda kwa Hakimu Mkuu Mkazi, Wilbard Mashauri.
12:01pm > Hadi muda ni kuwa watuhumiwa wote wakiongozwa na Mh. Freeman Mbowe ambao wapo gerezani Segerea waliokuwa waletwe Kisutu, hawajatokea. Inadaiwa gari hakuna na lililopo ni bovu!
11:50am > Askari wenye silaha za kivita wameanza kuitana, wanajikusanya. Hatujui walikuwa wanapanga nini. Baadae wamesambaa; baadhi wameelekea getini huku wengine wakijipanga tena kuzunguka viunga vya mahakama.
11:45am > Mawakili wa Jamhuri - Patrick Mwita, Mutalemwa Kishenyi na Mawakili wa washitakiwa Peter Kibatala na Hekima Mwasipu wameingia ofisini kwa Hakimu Mkuu Mkazi, Wilbard Mashauri.
11:34am > Baadhi ya Viongozi wa juu wa CHADEMA waliokuwa wamefika mahakamani wameondoka mahakamani Kisutu. Wanaenda kushiriki msiba wa marehemu Kimesela ambaye anazikwa makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
11:30am > Wananchi na makada wa CHADEMA wameanza kukosa uvumilivu baada ya kuzuiliwa nje ya lango kuu la mahakama na Polisi. Wameanza kuimba nyimbo za kudai haki, Wakili Kibatala amewasihi waondoke lakini dalili hazionyeshi kama wataondoka eneo hili.
11:20am > Mpaka muda huu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watano, hawajafikishwa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar. Tetesi zinadai kuna mikakati ya kuhakikisha wanakula Pasaka wakiwa gerezani. Kisingizio kinachodaiwa kutumika ni kuwa “Magereza hawana gari la kuwaleta mahakamani”
======
Katika Picha:
> Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa afika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi inayowakabili viongozi wakuu wa chama hicho, akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
View attachment 728388
==========
> Waandishi wa habari na wananchi wengi wamefika mahakamani ambapo ulinzi leo umeimarishwa sana. Kulikuwa na kesi ya Ugaidi hivyo inapelekea watu kuzuiliwa.
> Jeshi la Polisi limeimarisha zaidi ulinzi katika Mahakama ya Kisutu, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA na wananchi wamezuiwa kuingia, wamekusanyika nje ya mahakama.
View attachment 728403
> Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye pia amewasili mahakamani hapa kushuhudia kitakachotokea.
View attachment 728417
> Baadhi ya wanachama wa CHADEMA, viongozi na wananchi wakiwa ndani ya chumba cha mahakama kusubiri shauri la Mbowe na wenzake
View attachment 728420
Hahahah, wewe zombe zombe tu. Dkt Magufuli ni mtu safi anapendwa sana na watanzania, tunampenda sana tena sana, tupo tayari kufa kwa ajili yake, Mungu amlinde kabisa ili ainyoshe nchi, vibaraka wote lazima Mwenyezi Mungu awaue kama alivyopata kunena Shehe wa Mkoa Dar.Magufuli ukimaliza uraisi wako tegemea kupata shida ata kama utamrithisha mwanao, makosa yako hayatakuacha salama
Ausha lema aliwekwa ndani miezim sita hakukgeuka libya.Arusha kumemshinda ndo aweze nchi? Sema ana mikelele kama Lisu na Sugu tu .Hao watatu ndio wanaongoza kwa mikelele sasa hivi mwingine aliyeanza kujitutumia mikelele ni Heche.Hata mm ningewish iwe ivyo alaf chama kiachiwe kina LEMA kama hapajageuka libya hapa siyo mimi
Inaruhusiwa nje ya muda wa kazi wa mahakama na magereza ?Nina swali la kuuliza. Hivi kama ukipata dhamana bila kuletwa Mahakamani, Je utaratibu wa REMOVAL ORDER hauwezi kutumika?.
Jibu hoja.Umejitahidi kujitoa ufahamu, haya chukua buku saba ila mgawane na musiba!
hoja gani za kipuuzi! Et umeona wapi kiongozi mkubwa wa upinzani ananyimwa dhamana, hivi unamjua beseje? Si ni wa afrika!? Kwanza ulitaka wafuasi wa chama wafanyeje? Wavunje sheria kama unavyotaka wewe? Yaani wewe raha yako ulitaka uone wafuasi wa chadema waingie na geti pale kisutu? Kama ni hivyo basi jifikirie upya wallah huna ishu!Jibu hoja.