Kisutu, Dar: Kesi za JamiiForums vs Jamhuri zaendelea. Kesi namba 456 Hukumu kutolewa Desemba 06, 2019

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,930
2197985_1572414453980.png
Kesi namba 456 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums, imeendelea leo Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Thomas Simba.

Unaweza kusoma tulipoishia baada ya ushahidi kufungwa na watuhumiwa kujitetea: Maxence Melo aanza kujitetea Kesi Namba 456 Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji Mafuta Bandarini

Baada ya watuhumiwa kujitetea (defense) ilikuwa ni pande zote mbili kupeleka kwa Maandishi (Final submission) kabla ya Novemba 20 na leo ilikuwa iwe siku ya hukumu.

Upande wa Jamhuri haukuweza kupeleka Final submission katika muda uliopangwa, hivyo leo hakimu Thomas Simba kaomba muda wa ziada wa kupitia nyaraka zote zilizowasilishwa na upande wa Utetezi.

Tarehe rasmi ya kusomwa hukumu imetajwa kwamba itakuwa Disemba 06, 2019.

Upande wa utetezi uliwakilishwa na Mawakili Peter Kibatala, Benedict Ishabakaki na Jeremiah Mtobesya huku Upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon.
******

UPDATES: DESEMBA 06, 2019
Kesi namba 456 imeendelea leo Kisutu

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Silvia Mitanto huku Upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Peter Kibatala na Jebra Kambole

Hakimu Simba amesema anaendelea kuiandaa hukumu, kashamaliza kuandika bado kuandika nini alichoamua tu. Hivyo kaomba muda zaidi

Kesi imeahirishwa hadi tarehe 22 Januari 2020.

KESI NYINGINE YAENDELEA KUPIGWA KALENDA ZAIDI YA MWAKA

Kesi namba 458 ya Jamhuri vs Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Ndugu Maxence Melo na mwenzake Mickie William inayohusu kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kutumia Kikoa cha do.TZ na kutokutoa taarifa ya Mteja aliyeandika taarifa kuhusu Benki ya CRDB, imeendelea tarehe 26 Novemba 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Huruma Shaidi.

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Adolf huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Mawakili Benedict Ishabakaki na Peter Kibatala.

Wakili wa Serikali amesema Shahidi wa mwisho wanayemtegemea ameshindwa kufika hata leo. Hivyo wameomba muda zaidi ili waweze kuwasiliana na DPP kuhusu mwenendo wa huyu shahidi. Shahidi huyu anayesubiriwa (Tuly Mwambapa), sasa ni mwaka hajafika Mahakamani na kila kesi ikitajwa inaahirishwa akisubiriwa aweze kutoa ushahidi wake.

Hakimu kaiahirisha kesi hadi itakapotajwa tena tarehe 12 Desemba 2019.

Zaidi, soma:

Mungu wetu anasimama na wenye haki.

Sala zetu zi pamoja na Maxence na wote wanaopitia hili tanuri.

Amen
 
Mh Hakimu Thomas Simba hakika atatenda haki, Mungu amsimamie.
 
Kesi namba 456 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums, imeendelea leo Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Thomas Simba.

Unaweza kusoma tulipoishia baada ya ushahidi kufungwa na watuhumiwa kujitetea: Maxence Melo aanza kujitetea Kesi Namba 456 Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji Mafuta Bandarini

Baada ya watuhumiwa kujitetea (defense) ilikuwa ni pande zote mbili kupeleka kwa Maandishi (Final submission) kabla ya Novemba 20 na leo ilikuwa iwe siku ya hukumu.

Upande wa Jamhuri haukuweza kupeleka Final submission katika muda uliopangwa, hivyo leo hakimu Thomas Simba kaomba muda wa ziada wa kupitia nyaraka zote zilizowasilishwa na upande wa Utetezi.

Tarehe rasmi ya kusomwa hukumu imetajwa kwamba itakuwa Disemba 06, 2019.

Upande wa utetezi uliwakilishwa na Mawakili Peter Kibatala, Benedict Ishabakaki na Jeremiah Mtobesya huku Upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon.

KESI NYINGINE YAENDELEA KUPIGWA KALENDA ZAIDI YA MWAKA

Kesi namba 458 ya Jamhuri vs Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media Ndugu Maxence Melo na mwenzake Mickie William inayohusu kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kutumia Kikoa cha do.TZ na kutokutoa taarifa ya Mteja aliyeandika taarifa kuhusu Benki ya CRDB, imeendelea tarehe 26 Novemba 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Huruma Shaidi.

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Adolf huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Mawakili Benedict Ishabakaki na Peter Kibatala.

Wakili wa Serikali amesema Shahidi wa mwisho wanayemtegemea ameshindwa kufika hata leo. Hivyo wameomba muda zaidi ili waweze kuwasiliana na DPP kuhusu mwenendo wa huyu shahidi. Shahidi huyu anayesubiriwa (Tuly Mwambapa), sasa ni mwaka hajafika Mahakamani na kila kesi ikitajwa inaahirishwa akisubiriwa aweze kutoa ushahidi wake.

Hakimu kaiahirisha kesi hadi itakapotajwa tena tarehe 12 Desemba 2019.

Zaidi, soma:

Jamaaani hivi kweli ndo serikali etii duh serikali kitu kingine bana MUNGU amshindie mkurugenzi mickie Williams
 
Back
Top Bottom