Kisutu, Dar: Kesi namba 458 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums yaahirishwa hadi Jan 28, 2020, Shahidi bado Kitendawili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Kesi namba 458 ya Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo na mwenzake Mickie William inayohusu kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kutumia Kikoa cha do.TZ imeendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika Kesi hiyo ambapo Watuhumiwa hao wanashtakiwa pia kwa kuzuia upelelezi wa Polisi kwa kutokutoa taarifa za Mteja aliyeandika taarifa kuhusu Benki ya CRDB imeendelea mbele ya Hakimu Huruma Shaidi.

Kwa siku ya leo, upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Gloria huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Benedict Alex.

Wakili wa Jamhuri amesema, shahidi wa mwisho wanayemtegemea hawajampata bado na hivyo kuomba muda mfupi zaidi ili waweze kuwasiliana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kujua shauri hili litaendeleaje.

Shahidi huyo, Tully Mwambapa anayetokea CRDB amekuwa akisubiriwa tangu Agosti 01, 2019 ambapo upande wa Jamhuri ulisema ungemleta kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.

Tangu hapo shauri hili limekuwa likiahirishwa mara kwa mara kwa kukosekana kwa shahidi huyo huku sababu kadha wa kadha zikitolewa.

Katika shauri hili mara ya mwisho shahidi kusikilizwa ilikuwa ni Novemba 12, 2018 ambapo Mpelelezi Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Mtandaoni kutoka Makao Makuu ya Polisi (HQ), Inspekta Beatrice Majule alikuwa ndiye shahidi

Baada ya Wakili wa Jamhuri kuomba muda zaidi Wakili wa Utetezi alikubali na Hakimu Shaidi kuahirisha shauri hilo hadi mwakani mnamo Januari 28

Zaidi, soma;


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Washitaki na mashahidi wao wote wanaitegemea kwa kiasi kikubwa sana JF, siyo kwamba hizi kalenda zinasubiri wanayoyataja, ila wanajiuliza athari watakazozipata hata wao wenyewe iwapo hawataitendea haki JF
 
Huyo shahidi kutoka CRDB BANK hawezi kwenda mahakamani hata Kwa viboko hii kesi itaishia kimya kimya kwasabb wanajua jinsi gani Shahid ni Kati ya wapigaji madili na vigogo
 
Back
Top Bottom