KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri dhidi ya JamiiForums) yaendelea - Shahidi wa Tatu atoa ushahidi wake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
783
1,000
Leo kesi namba 457 (inahusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi bandarini, kuchonga nyaraka kutorosha makontena na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania) imeendelea katika Mahakama ya Mkazi, Kisutu ambapo Shahidi wa 3 amesikilizwa.

Shahidi wa kwanza na ushahidi wake: ‪Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai Polisi hawana utaalamu wa kulazimisha kuingilia mawasiliano kimtandao‬

Shahidi wa pili na ushahidi wake: KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri dhidi ya JamiiForums) yaendelea - Shahidi wa Pili atoa ushahidi wake

Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa shahidi wa tatu leo:

Hakimu Mwambapa: Kwa kumbukumbu, Shahidi wa leo ni shahidi wa tatu

Shahidi: Naitwa Rehema Kitambi, dini yangu ni Mkristo. Cheo changu ni Msajili Msaidizi Mkuu wa Makampuni kwa muda wa kama miezi sita iliyopita sasa.

Wakili wa Jamhuri: Waajiri wako ni nani?

Shahidi: Ni BRELA

Wakili wa Jamhuri: Kituo chako cha kazi ni wapi?

Shahidi: Dar es Salaam, Jengo la Ushirika ghorofa ya tatu

Wakili wa Jamhuri: Majukumu yako kama Msajili Msaidizi Mkuu wa makampuni ni yapi?

Shahidi: Majukumu ni kuhakiki nyaraka mbalimbali kwa ajili ya kufanya usajili kwa ajili ya makampuni mapya na na nyaraka baada ya usajili kwa ajili ya mabadiliko mbalimbali kwenye makampuni. Na kufanya usajili husika na majina ya biashara husika

Wakili wa Jamhuri: Nini pia unafanya tofauti na hilo?

Shahidi: Kuhakiki taarifa mbalimbali ikiwa ni kufanya mabadiliko mbalimbali katika kampuni na majina ya biashara. Pia kutoa ushauri wa kisheria, kujibu barua mbalimbali kutoka kwa mtu yeyote anayetaka kupata taarifa ikiwa ni Kampuni binafsi au taasisi za Serikali

Wakili wa Jamhuri: Umekuwepo BRELA tangu lini?

Shahidi: Tangu tarehe 03/09/2001

Wakili wa Jamhuri: Nini kilitokea mnamo tarehe 13/12/2016?

Shahidi: Nilipatiwa barua nijibu taarifa ikitaka taarifa juu ya Maxmelo na kampuni ya Jamii Forum, na nilipewa barua nieleze.

Wakili wa Jamhuri: Barua ilitoka wapi?

Shahidi: Ilikuwa inatoka kwa Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai

Wakili wa Jamhuri: Barua ilikuwa inataka nini?

Shahidi: Ilikuwa inataka taarifa za usajili za kampuni ya Jamii Forum na kujua jina Maxmelo kama ni mmoja wa Wakurugenzi wa hiyo kampuni.

Wakili wa Jamhuri: Halafu ukafanya nini?

Shahidi: Kwa mujibu wa taratibu unaitisha jalada, kwa uchunguzi niliitisha jalada toka Masjala kulikuwa hakuna kampuni iliyosajiliwa kama Jamii Forum kwa siku hiyo tarehe 13/12/2016.

Tulitafuta kwenye system iitwayo Saperion, ambayo ina scan taarifa za usajili kwa kipindi fulani. Tuliingiza jina la Maxmelo akatokea kwenye kampuni tatu kwa tarehe hiyo, ambazo sizikumbuki lakini moja ilikuwa ni Jamii Media

Masijala wanafanya hii search then wanakuletea majalada hayo

Wakili wa Jamhuri: Halafu ulifanya nini?

Shahidi: Nikajibu barua ya Mkurugenzi wa upelelezi juua ya majina ya wasajiliwa, namba za usajili, tarehe za usajili na wamiliki wa hisa za hizo kampuni tatu alizotokea Maxmelo (akimaanisha Maxence Melo)

Wakili wa Jamhuri: Ukiona barua nini kitakutambulisha kama ni yenyewe?

Shahidi: Nembo ya BRELA, muhuri na sahihi yangu mwenyewe

[Wakili wa Jamhuri anatoa nakala ya barua na kuomba ipokelewe na Mahakama, inapokelewa na Mahakama na hakimu kuitambua kama Exhibit P2]

Shahidi anapewa barua na kuisoma kujiridhisha kama ni yenyewe

Wakili wa Jamhuri anaishia hapo kwa maswali

Mtobesya ambaye ni wakili wa utetezi anaruhusiwa kuuliza maswali shahidi

Mtobesya: Kwenye hii barua kuna sehemu yeyote umeeonyesha uhusiano kati ya Jamii Media na JamiiForums?

Shahidi: Kwenye barua inauliza kuhusu Jamii Forum

Mtobesya: Kwa maana hiyo nitakuwa sahihi nikisema havina uhusiano (Jamii Media na JamiiForums) wowote?

Shahidi: Kisheria kila kampuni inasimama pekee. Lakini barua ilitaka kujua kama Jamii Forum inatokea sehemu ndio maana tukajibu hivi

Mtobesya: Kwenye lile angalizo la kwenye barua yako ni nini hasa kimeelezewa?

Shahidi: Mbali na nyaraka zile za usajili za awali kampuni imewasilisha baadhi ya form kutaka kufanya mabadiliko katika yale tuliyofanya awali kwenye usajili; Mabadiliko ya Wakurugenzi na wamiliki, ila kwenye barua nimeandika na kadhalika.

Mtobesya: Wakati wewe unaandika barua hii mlikuwa mmesha-attend mabadiliko hayo?

Shahidi: Ndio ila hatukufanya changes kwa sababu ya kasoro kadhaa. Maombi yalikuwa yamepokelewa ila yanashughulikiwa kujibu barua hiyo ya mabadiliko.

Mawakili wote wanasema hawana maswali ya ziada kwa shahidi, anaruhusiwa kuondoka.

Kesi itaendelea kesho, Jamhuri imesema inao mashahidi wawili wa kufunga ushahidi katika kesi hii hapo kesho.
 

Masamila

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
5,499
2,000
Duh, IQ yangu inachechemea sana, ngoja nisubirie ambao wako vizuri kwa IQ waje
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,542
2,000
Hawa watu badala ya kushughulikia matatizo ya wananchi wanang'ang'ania kuendesha kesi ambazo hazina tija kwa Taifa. Haya ndio madhara ya nchi kuendeshwa kwa mihemuko pasipo kuzingatia sheria na tija.
Badala ya kushughulikia na Mshukiwa, wao wanashughulika na Whistle Blowers, itafika kipindi hata watu wakiona jambo basi wanashindwa kulifichua hadharani maana wenye nchi yao watataka kupata undani wa mfichua uozo badala ya kuchunguza huo uozo wenyewe
 

Pancras Suday

Verified Member
Jun 24, 2011
7,814
2,000
Badala ya kushughulikia na Mshukiwa, wao wanashughulika na Whistle Blowers, itafika kipindi hata watu wakiona jambo basi wanashindwa kulifichua hadharani maana wenye nchi yao watataka kupata undani wa mfichua uozo badala ya kuchunguza huo uozo wenyewe
Refer back kwenye majengo ya Magu na nyufa kilichomtokea kijana wetu
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,762
2,000
Uzi kama huu hutawaona uvccm maana wao kila kitu inachofanya serikali wanafurahia hata kama kitu hicho kinaminya uhuru wetu wa kupata habari humu JF, wanaogopa tutawashambulia
 

yesse lambert

Member
Nov 26, 2017
30
95
At least, huyu shahidi mwanamama anajitambua kidogo na anajua akisemacho...

Lakini mashahidi wa kutoka polisi, kidogo weledi wao wa mambo unatia shaka sana...
vip huko bwana
:):):);););):(:(:(:mad::mad::mad:o_O
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom