Kisiwa kigombaniwacho na Kenya, Raisi Museveni asema aombe Msamaha wa Nini ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kisiwa kigombaniwacho na Kenya, Raisi Museveni asema aombe Msamaha wa Nini ?

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Bikra, May 16, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  May 16, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Baada ya wiki ya mabishano makali kati ya Kenya na Uganda, Rais Yoweri Museveni amesema kwamba alinukuliwa vibaya alipozungumzia swala la mipaka hasa inayohusu visiwa katika ziwa Victoria.
  Kiongozi huyo wa Uganda aliitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo aliteta kwamba hotuba yake haikugusia kisiwa cha Migingo kinachozozaniwa kati ya Kenya na Uganda.
  Rais Museveni alisema mzozo huo ni mdogo na waweza kutatuliwa kwa kufanya mazungumzo kati ya mataifa hayo mawili.
  Aidha amesema serikali yake iko tayari kuafikiana na matokeo ya upimaji mipaka unaondelea kuthibitisha mipaka ya kisiwa hicho.
  Rais Museveni alitupilia mbali madai kwamba alitumia matamshi yasiyokubalika kuhusu jamii ya Wajaluo nchini Kenya ambao aliwashutumu kwa kung'oa reli inayoelekea nchini Uganda.
  Ila, Rais Museveni alimtaka waziri wa ardhi nchini Kenya James Orengo kuomba msamaha kwa matamshi ambayo alisema yalikuwa yakuwadhalilisha watu wa Uganda.
  Wabunge nchini Kenya
  Serikali ya Uganda ililazimika kumtetea Rais Museveni baada ya matamshi yake kuhusu umiliki wa kisiwa cha Migingo kuzusha hasira kubwa nchini Kenya.
  Wabunge nchini Kenya wamekasirishwa na matamshi ya Rais Museveni na kuomba Umoja wa Afrika pamoja na Baraza la Usalama kuingilia kati mgogoro huo.
  Hivi majuzi akiwa kwenye ziara rasmi nchini Tanzania, Rais Museveni alisema ingawa kisiwa cha Migingo ni cha Kenya, maji yanayokizunguka ni ya Uganda.
  Huku akisikika mwenye hasira, kiongozi huyo wa Uganda alisema endapo sheria za kikoloni zilizotumika kupima mipaka ya Afrika Mashariki zitazingatiwa, Wakenya hawatoweza kuvua samaki katika eneo hilo.
  Lakini Mkurugenzi wa kituo cha habari cha serikali ya Uganda, Fred Opolot, alisema vyombo vya habari havikunukuu vilivyo aliyoyasema Rais Museveni.
  Aombe msamaha, kwa nini?
  Bwana Opolot pia alisema Rais Museveni hatoomba msamaha kufuatia shutuma aliwatusi jamii ya Wajaluo nchini Kenya.
  "Aombe msamaha, kwa nini?" aliuliza Bwana Opolot.
  Baadhi ya watu kutoka jamii hiyo wanashukiwa kung'oa sehemu za reli inayotumiwa kusafirisha mizigo hadi nchini Uganda.
  Rais Museveni aliwakemea katika hotuba yake kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  "Nimekuwa nikiwaambia Wajaluo ambao wamekuwa wakiandamana na kung'oa reli kwamba tukitekeleza utaratibu huu hakuna Mjaluo atavua samaki kutoka hapa."
  Hata hivyo Bwana Opolot alimtetea Rais Museveni akisema yaliyoripotiwa kuhusu Rais yalikuwa nje ya muktadha wa hotuba yake.
  Mjadala kuhusu migingo
  Kenya na Uganda zimeanza shughuli ya pamoja ya kupima mipaka ya kisiwa hicho ambacho kinasemekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya samaki katika ziwa Victoria.
  Shughuli hiyo itakamilika katika muda wa miezi miwili.
  Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema majuma machache yaliyopita, gazeti la serikali liliripoti kuwa rais alisema kisiwa kipo Kenya, na siku moja baadaye likashawishika kukanusha hizo habari.
  Hata hivyo, mjadala kuhusu Migingo haujapamba moto nchini Uganda kama ilivyo Kenya.
   
 2. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Kusema kweli baada ya kumsikia mzee mzima M7 kwenye BBC ndo niliona kwamba jamaa anazeeka vibaya!
   
Loading...