Kisiwa cha Mafia tushaamua, hatumtaki Bulji

Sep 21, 2011
20
8
Huyu mbunge wetu wa sasa nadhani mwenyewe keshajua. His time is up na nadhani its about time akatangaza kutogombea tena 2015.

Tushachoka na CCM wakitaka kulazimisha then bora tuwape wapinzani jimbo lakini as it is. We've had enough with Mr Shah. This does not mean kuwa tunataka Omari Kimbau awe mbunge wetu lakini kama akiweza na wengine sawa tuu

Kisiwa kinaendeshwa na NGO's tuuu , watu wamekatazwa kuvua, hakuna umeme, barabara mbovu, vituo vya afya navyo hatuna, kila kitu kigumu hapa kisiwani

lakini tushaamua. Hatumtaki huyu Mbunge wetu. Tushamchoka!!
 
Mkuu anza wewe hapo kwa kuweka bendera ya wapiganaji, na pia wasiliana na CDM makao makuu kwa ajili ya vifaa kama kadi za uachama. Itaamsha wananchi taratibu. Ukitumia muda wa saa 1 kila siku au siku 2, utakuwa umewasaidia wananchi wenzako. Naimani huyo mbunge akiona hali ya joto kama hilo atalazimika kuanza kutimiza wajibu wake.
 
Dah! Hali kisiwani hapo ni mbaya kiukweli. Kwa wale tuliofanikiwa kufika hapo ni mashahidi. Huko visiwa vidogo vinavyounda wilaya ya Mafia ni vigumu kuamini kama kweli viongozi wetu wanauchungu na nchi hii.

Mimi huwa najiuliza "kama Magamba wangetumia mtandao wa nyumba kumikumi kufanya kile wanachotakiwa kufanya badala ya kutumia mtandao huo kwa kurubuni wapiga kura, hali ingekuwa hivi? Mafia ni kielelezo dhahiri cha uchovu wa magamba. Kisiwa kidogo cha Juani pamoja na kuwa na historia ndefu tangu karne kadhaa nyuma kimesahauliwa.
 
Huyo Mbunge wenu Kimeo!

Nilishangaa siku alivyokuwa anatumika na akina Mtemvu kushabikia hoja ya UDA. Jamaa alitumia mda wake wote akiongea kwa jazba juu ya usafiri dar es salaam, Huku akisahau wananchi wake hawana usafiri wa uhakika wa boti ya kusafiria, akisahau kukumbushia ahadi aliyoitoa Rais Kikwete juu ya kukamilisha gati la mafia ifikapo februari 2011. Akisahau kukumbusha ahadi ya serikali kuipatia Mafia chuo cha ufundi, shule ya kidato cha Tano nk.

Mnachotakiwa hapo ni kuikataa CCM, sio mbunge pekee!

Hata huyo Omari kimbau mnaemsema si Kiongozi kama mnavyofikiria, mtakuja kulia mara mbili! Tuulizeni sisi mjini huku!
 
Mkuu si utangaze nia ya kugombea? Wakazi wengi wa Mafia wanaonekana wameichoka ccm, inavyoonyesha na wewe upo bado na mawazo ya hilo lichama lenu! Angalia upande mwingine!
 
Majimbo ambayo ccm ipo inabidi mteseke sana ili akili yenu ipate kupambanua mambo vizuri!endeleni kuteseka na ccm yenu ,wajinga ndio ,..!
 
Hii ni kutokana na ujinga wenu.sasa jielimisheni nyinyi wenyewe muda ukifika muwe na nguvu ya kusema hapana.anza sasa huu ndiyo muda wa mabadiliko.
 
Mliambiwa kumchagua, Kama hamumtaki Mbunge subiri 2015, Hauwezi mkataa mbunge kwenye JF
 
Kama wewe ni mzawa asilia wa Mafia, mbunge is very irrelevant, just think out of your box. Mafia ni kisiwa unaweza kujitenga katika masuala ya kiuchumi then ya kisiasa.

Usimlalamikie mtu ambaye ametumia Juhudi zake binafsi ili Apate Mkopo wa Shangingi,Alipwe Seating Allowance ili abwabwaje au ake kimya tu lakini bado atalipwa hiyo allowance.na akifanikiwa anaweza kuwa Waziri wa kuteuliwa na Raisi.

Hivi unategemea mtu aliyetumia pesa yake na uwezo wake binafsi ajali maslahi yenu huko Mafia, a good example ni Mbunge aliyejitoa siasa uchwara wa IGUNGA, the Richest man in TZ, lakini ukienda Igunga maendeleo hayapo,watu maskini,vumbi kila kona, shule hamna. So kwa wewe wa MAFIA tuliza ball usimsumbue mbuge mteuliwa wa CCM.

USHAURI:

Anzisha Mageuko ya kiuchumi na kisiasa. Fungua website/blogg na gazeti la kisiwa. Changisha wananchi0, elimisha wananchi juu ya mfumo wa uchaguzi na jinsi ya kulinda kura, (ukionyesha mapungufu), wananchi wakikuelewa. Karibisha Makamanda waje wakupe msaada wa Mageuko kisiwani kwenu.
 
Tumekusikia mzee. Usiniambie kwamba miaka yote ya ubunge wa baba yake Omar Kimbau yote hayo hayakufanyika halafu leo mnaurudisha ubunge kwa familia hiyo hiyo. Ni kurogwa au?
 
Je ni mawazo yako au ndio mawazo ya jumla ya wana wa Kilindoni.
Punguza ushabiki
 
Bulji hatukutaki umewekwa tu kwanza hatujakuchagua kwenye kura za maoni tulimchagua Omary kimbau tuachie jimbo letu
 
Si mafia tu, lipo Jimbo lingine la Nyang'wale mbunge wake katika michango yake Bungeni yeye anadai posho iongozwe na kuelezea kero za familia yake, Elimu yake sina hakika kama kamaliza la saba ingawa analazimisha hivi,kawalambisha chumvi na sukari wakamchagua,jimbo halina barabara inayopitika majira yote,maji ni miujiza, umeme ndo usiseme japo unapita jimboni kwake kwenda mgodi wa Kahama Mining
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom