Kisiwa cha Guam kinajipatia umaarufu sana

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau kisiwa cha Guam kimejipatia umaarufu mkubwa karibuni kufuatia mzozo unaozidi kukua baina ya DPRK na USA. Mzozo huo umefikia hatua ya DPRK kutishia kukishambulia kisiwa hicho kwa makombora.
Yafuatayo nimachache kuhusu kisiwa hicho;
a) Ni kisiwa kikubwa kabisa katika bahari ya Pacific.
b)Kisiwa hicho nimali ya USA
c) Wazaliwa wa kisiwa hicho ni raia wa USA lakini hawana haki ya kupiga kura kumchagua Rais wa USA.
d)Kisiwa kipo umbali wa maili 8,000 kutoka New York
e)Usafiri toka USA hadi kisiwani humo ni masaa 19 kwa ndege.
f) Idadi ya wakazi wa kisiwa hicho ni 160,000,asilimia kumi ni wanajeshi wa USA.
g) Kisiwa hicho ni kambi kubwa ya Jeshi la Anga na Maji.(robo ya kisiwa hicho ni mali ya Jeshi la USA)
h) Wakazi wa kisiwa hicho hawalipi kodi.
Karibuni.
NB: kombora moja limerushwa leo alfajiri kupitia anga ya Japan na kutua katika pwani ya kisiwa hicho cha Guam.
 
Back
Top Bottom