johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,853
- 141,772
Ukifuatilia kwa makini mwenendo wa Freeman Mbowe utagundua kuwa ni mtu anayejua anachokifanya. Tofauti na wanasiasa wengi ambao hutenda mambo kwa kubahatisha, kinafiki na wakati mwingine wakitaka waonekane wanausapoti uongozi wa juu.
Ukiangalia utendaji wa Mbowe kama KUB amekuwa upande wa serikali zaidi japo hili huwezi kulibaini kiurahisi. Tofauti na Dr Slaa alipokuwa akimsaidia KUB Hamad Rashid , Mbowe hajawahi kuibua hoja yoyote nzito ya kuibana serikali.
Hata kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu ambapo kanuni zinampa upendeleo KUB kuuliza swali la kwanza mara nyingi Freeman huwa hayupo bungeni.
Mambo ni mengi hata kumuengua Dkt. Slaa kinyemela 2015 na kumleta Lowassa ulikuwa ni mkakati wa kutaka kuhakikisha mtu makini hagombei.
Ikumbukwe hapa ni Mbowe huyu huyu aliyemtoa Dkt. Slaa bungeni ili agombee urais ilhali akijua kabisa huwezi kumshinda Rais wa CCM anapogombea muhula wa pili. Lengo la Mbowe lilikuwa ni kupunguza nguvu ya Dr Slaa kwani umaarufu wake aliujengea zaidi bungeni.
Niseme tu kwa kifupi, Mbowe na hata Zitto Kabwe wanaweza kuwa ni marafiki " wazuri" wa Dr Magufuli kuliko Ndugai na Musukuma.
Maendeleo hayana vyama!